Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-13 15:07:58    
Dunia yapaswa kufanya ushirikiano wa pande nyingi katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani

cri
    Mwaka 2004 ni mwaka wa tatu tangu kutokea kwa tukio la tarehe 11 Septemba 2001 nchini Marekani, lakini shughuli za ugaidi bado zinapamba moto duniani, na zimekuwa tishio kubwa jipya dhidi ya utulivu, usalama na maendeleo ya nchi mbalimbali duniani, na inazingatiwa sana na jumuiya ya kimataifa. Ushirikiano katika kupambana dhidi ya ugaidi limekuwa jambo muhimu katika uhusiano wa kimataifa.

     Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, matukio makubwa ya ugaidi ya aina mbalimbali yametokea moja baada ya nyingine katika sehemu mbalimbali duniani, kama vile milipuko mfululizo ya gari moshi yaliyotokea huko Madrid, Hispania, tukio la kutekwa nyaraka lililotokea huko Beslan, Russia, na mlipuko uliotokea huko Taba, Misri. Matukio hayo yote yameonesha umaalum ambao magaidi wanapenda kuona matokeo ya mauaji makubwa yanayoitingisha dunia nzima. Shughuli za ugaidi zimezidi kumwagika damu zaidi, na zimepamda moto zaidi kwa mbinu mpya siku hadi siku na kuendelea kupanua eneo duniani. Ingawa Marekani imeimarisha hatua za kupambana na ugaidi nchini humo kutokana na tukio la tarehe 11 Septemba, na pia inaendelea kuchukua hatua za kijeshi nchini Afghanistan na Iraq kwa kisingizio cha "kupambana dhidi ya ugaidi", Lakini shughuli za ugaidi zinaenea katika nchi na sehemu nyingine nje ya Marekani, na maisha ya maelfu ya watu yamepotea. Kutokana na kukamiliwa na hali halisi ya kuenea kwa ugaidi siku hadi siku, maneno aliyosisitiza mara kwa mara rais Bush wa Marekani "Marekani na dunia imekuwa na usalama zaidi" yanakosolewa zaidi na kutiwa mashaka mengi. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alisema: "Siku zote sidhani kuwa dunia imekuwa na usalama zaidi kuliko miaka miwili au mitatu iliyopita".

     Vyombo vya habari vimedhihirisha kuwa, utatanishi zaidi unaotokea katika hali ya mapambano dhidi ya ugaidi duniani unahusiana na sera ya makosa ya Marekani kuhusu suala la mapambano dhidi ya ugaidi, mapambano dhidi ya ugaidi yamekuwa chombo cha Marekani cha kurekebisha mikakati ya usalama wa nchi na kuimarisha hadhi yake ya Ubabe umwamba kote duniani. Kwa upande mmoja kutokana na Marekani kuacha mwelekeo sahihi wa mapambano dhidi ya ugaidi, kushikilia njia yake ya upande mmoja, na kuanzisha vita vya Iraq kwa, hayo yote yamezidisha migongano ya kitaifa na kidini, na kusaidia kukua na kuenea kwa ugaidi. Kwa upande mwingine, Marekani inafuata "vigezo viwili" katika mapambano dhidi ya ugaidi. Inapopambana na shughuli za ugaidi zinazotishia maslahi ya nchi hiyo, wakati inakaa kimya hata kuchochea shughuli nyingine za ugaidi zinazotishia nchi nyingine, matokeo ya mapambano dhidi ya ugaidi duniani hayaridhishi kama yaliyotarajiwa.

     Watu wenye busara wanaona kuwa, lazima kufanya ushirikiano wa pande nyingi wa kimataifa, kutokomeza chanzo cha kusababisha shughuli za kigaidi ili kupata ushindi katika mapambano dhidi ya ugaidi duniani.

     Wanabainisha kuwa, ushirikiano wa pamoja wa jumuiya ya kimataifa ni uhakikisho wa kimsingi kwa kupata ushindi katika mapambano dhidi ya ugaidi, pia ni njia pekee mwafaka. Kama alivyodhihirisha rais Hu Jintao wa China katika mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC uliofanyika mwezi Novemba kuwa, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuelekezwa na katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za sheria ya kimataifa zinazohusika, kuchukua hatua imara za pamoja kwa kupambana na ugaidi wa aina yoyote.

      Aidha, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za jumla, kutafuta chanzo cha ugaidi na kukitokomeza hatua kwa hatua. Hivi sasa migogoro kadhaa duniani haiwezi kutatuliwa kwa haki kwa muda mrefu, bali inapanda moto siku hadi siku, na imekuwa ikitoa nafasi kwa magaidi wachache kuzusha shughuli za ugaidi. Hayo yameonesha kuwa, sababu za kimsingi za shughuli za ugaidi bado hazijatokomezwa, hivyo kutegemea tu mbinu za kijeshi hakutaweza kuzuia kabisa ugaidi na kutokomeza kabisa ugaidi. Ni lazima mbinu za kidiplomasia, kielimu na kimsaada zitumike ili kupunguza na kutokomeza chanzo cha ugaidi na kuleta usalama kwa dunia.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-13