|
Tarehe 12 msaidizi wa kiongozi kijana wa Fatah aliyeko gerezani nchini Isreal, Bw. Marwan Barghouti, alitangaza kuwa Bw. Marwan Barghouti ameamua kujitoa kutoka kwenye uchaguzi mkuu wa mamlaka la Palestina na alitoa wito wa kuwataka watu wa Palestina wamchague mgombea pekee wa Fatah, mwenyekiti wa kamati ya utendaji ya Fatah, Mahamoud Abbas. Bw. Marwan Barghouti kwa mara kadhaa alibadilisha nia yake kuhusu kushiriki au kutoshiriki kwenye uchaguzi mkuu, hili ni suala la kujiuliza sana.
Tarehe mosi mwezi huu, Bw. Barghouti alighairi uamuzi wake wa kutoshiriki katika uchaguzi mkuu, na kwamba katika siku ya mwisho ya kujiandikisha kugombea katika uchaguzi huo, alitangaza kugombea wadhifa wa mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina. Kutokana na kuwa kabla ya hapo Fatah ilikuwa imekwisha tangaza kumpendekeza Abbas kuwa mgombea pekee wa Fatah, na Bw. Barghouti pia aliwahi kusema kuwa alimwuunga mkono Abbas. Mabadiliko hayo ya ghafla ya Bw. Barghout kutaka kushiriki kwenye uchaguzi yalisababisha mtafaruku ndani ya chama cha Fatah. Vingozi wa Fatah walilaani kuwa mabadiliko ya Barghouti yalisababisha mfarakano ndani ya Fatah na kuvifaidisha vikundi vingine. Hali ambayo Braghouti hakutegemea kutokea ni kuwa vikundi kadhaa ndani ya Fatah ambavyo vilimwunga mkono hapo awali, kama vile Arafat Martyrs Brigades, watu wa Palestina waliofungwa na Isreali na kamati ya uongozi wa Fatah iliyoasisiwa na Barghouti pia vilimgeuka na kumpinga Bw. Barghouti kushiriki katika uchaguzi. Ili kumshawishi Barghouti asigombee katika uchaguzi huo, Fatah iliwahi kutuma wajumbe mara kadha kwenda gerezani kuonana na Barghouti na kumtishia ajitoe kutoka uchaguzi huo wakimwambia kuwa vinginevyo atatimuliwa kutoka Fatah. Safari hii sababu ya Bw. Barghout kujitoa kutoka uchaguzi mkuu ndiyo inatokana na shinikizo hilo kubwa linalotoka kutoka ndani ya Fatah.
Wachambuzi wanaona kuwa Barghouti kwa kweli hana nia ya kushiriki kwenye uchaguzi huo bali ana lengo lingine kwa kutumia suala hili. Katika msimamo wa kisaisa, Barghouti anashikilia kwamba mapigano ya kijeshi ni njia muhimu ya kupambana na mashambulizi ya Isreal, na haifai kuyaacha. Lakini anaona kuwa viongozi wa Palestina wanajaribu kubadilisha njia hiyo, anataka kuwakumbusha viongozi hao wasifuate suluhu na Isreal kwa kutangaza kushiriki kwenye uchaguzi mkuu huo. Kadhalika, Barghouti pia anataka kuwalazimisha viongozi wazee kuacha madaraka na kuwapa viongozi vijana haki ya kutoa maoni. Imefahamika kuwa Barghouti aliwahi kumwandikia barua Abbas yenye matakwa tisa na kusema kwamba endapo ataridhia matakwa hayo tisa atajitoa kutoka uchaguzi huo. Ofisa mmoja wa Fatah aliwahi kusema kuwa matakwa ya Barghouti ni pamoja na kuifanya sehemu ya mashariki ya Jerusalam iwe mji mkuu wa Palestina, kutatua tatizo la wakimbizi wa Palestina kwa haki, kuwaachia huru wafungwa wa Palestina, Isreal isimamishe kuwaua watu wenye silaha wa Palestina na iondoe jeshi lake kutoka sehemu ya ukingo wa magharibi wa Mto Jordan. Habari kutoka kituo cha redio cha Isreal zinasema kuwa Abbas kimsingi amekubali matakwa hayo.
Barghouti ana ushawishi mkubwa miongoni mwa raia na hasa watu maskini wa Palestina. Takwimu zilizotangazwa hivi karibuni zinasema kuwa kiasi cha watu wanaomwunga mkono karibu sawa na watu wanaounga mkono Abbas, wote wawili wanapata asilimia 40 hivi. Lakini Abbas ana sifa ambazo Barghouti hana. Kwanza Abbas ni kiongonzi mkuu wa Palestina kwa sasa, na ana msingi imara zaidi wa kisiasa wa kushiriki kwenye uchaguzi huo, mbali na hayo Isreal imetangaza mara nyingi kuwa haitamwachia huru Braghouti. Pili wengi wa Palestina wamechoka na migogoro inayoendelea kwa muda wa miaka minne kati ya Isreal na Palestina, watu wanataka amani na Abass anayetetea kufanya mazungumzo ya amani anaweza kuwaletea maisha ya utulivu. Tatu, Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zinamuunga mkono zaidi Abbas na kutoa ahadi kuwa kama Abbas akishinda katika uchaguzi huo zitatoa misaada mingi kwa Palestina.
Maoni ya vyombo vya habari yanasema kuwa kutokana na yaliyotajwa, uamuzi wa Barghouti kujitoa kutoka kwenye uchaguzi na kumwachia Abbas ni kitendo cha busara kwa ajili ya umoja wa Fatah na hata utulivu wa kisiasa nchini Palestina.
Idhaa ya kiswahili 2004-12-13
|