Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-14 15:39:33    
Kampeni ya uchaguzi ya katibu mkuu wa Shirika la biashara duniani yaanza

cri

    Msemaji wa Shirika la biashara duniani jana huko Geneva alithibitisha kuwa, Ufaransa imemteua mfaransa Pascal Lamy aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Ulaya aliyeshughulikia mambo ya biashara kuwa mgombea wa katibu mkuu wa shirika la WTO. Kwa kuwa Bwana Lamy ana nguvu zaidi ya ugombeaji, hivyo ugombeaji wake unafuatiliwa zaidi.

    Katibu mkuu wa sasa wa Shirika la WTO Bwana Supachai Panitchpakdi ataachia wadhifa huo mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka kesho. Ili kuziwezesha nchi wanachama wote zishiriki ipasavyo mchakato wa uchaguzi wa katibu mkuu wa WTO, shirika hilo limeamua kutumia mwezi mmoja kuwateua wagombea, na kufanya majadiliano kwa miezi mitatu ili kutoa uamuzi. Kazi ya kuandikisha wagombea imeanza mwanzoni mwa mwezi huu na itakamilika mwishoni mwa mwezi huu. Toka mwezi Februari hadi Mei mwaka kesho, Baraza kuu la Shirika la WTO litasikiliza maelezo ya kila mgombea, na mwishoni mwa mwezi Mei litamthibitisha katibu mkuu mpya wa shirika hilo. Katibu mkuu mpya atashika madaraka kuanzia mwezi Septemba mwaka 2005.

    Mpaka sasa mbali na Bwana Lamy aliyeteuliwa na Ufaransa, wagombea wengine watatu wote kutoka nchi zinazoendelea kama vile balozi wa Brazil katika WTO Bwana Luiz Felipe de Seixas Correa, Balozi wa Uruguay katika WTO Bwana Carlos Perez del Castillo na waziri wa mambo ya nje wa Mauritius Bwana Jayen Cuttaree. Kutokana na duru jipya la mazungumzo ya pande nyingi kuitwa kuwa "Raundi ya maendeleo", hivyo watu fulani wanaona kuwa, ili kuelekeza mazungumzo hayo, katibu mkuu wa WTO atakayetoka nchi inayoendelea atakuwa mwafaka zaidi. Lakini watu wenye mawasiliano zaidi na WTO wanachambua kuwa, wagombea watatu kutoka nchi zinazoendelea ingawa wanaungwa mkono sana na nchi zao, lakini bado hawajaweza kuungwa mkono na watu wengi wa sehemu waliko. Brazil na Uruguay zote ni nchi za Latin Amerika, ni mgombea mmoja tu kati ya wagombea wa nchi hizo mbili ataweza kuchaguliwa. Na Bwana Cuttaree wa Mauritius pia anakabiliwa na ushindani kama huo katika sehemu aliko, kwani nchi ya Kenya hivi karibuni pia imesema iko tayari kumteua waziri wa biashara wake kugombea wadhifa wa katibu mkuu wa WTO.

    Aidha, wachambuzi wanaainisha kuwa, kutokana na kanuni isiyoandikwa rasmi za shirika la WTO, katibu mkuu wa WTO angechaguliwa kwa zamu kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Katibu mkuu wa sasa Supachai anatoka Thailand, kama kutokana na kanuni hiyo, katibu mkuu mpya anayetoka nchi iliyoendelea, ambapo Bwana Pascal Lamy kutoka nchi inayoendelea anaonekana kuwa na nguvu kubwa zaidi. Kwani ugombeaji wake umeungwa mkono na nchi wanachama wote 25 wa Umoja wa Ulaya, na huenda atapata tena uungaji mkono wa Marekani. Katika miaka ya hivi karibuni, Bwana Lamy kimsingi amedumisha mazungumzo na mashauriano na Marekani kuhusu mambo ya biashara. Habari zinasema kuwa, Bwana Lamy ana uhusiano mzuri binafsi na mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw Zurik, tarehe 7 mwezi huu Marekani ilikaribisha Bwana Lamy kugombea wadhifa wa katibu mkuu mpya wa WTO. Watu wengine wanachambua kuwa, kutokana na juhudi za Bwana Lamy za miaka ya hivi karibuni katika kuuhimiza Umoja wa Ulaya kufuta ruzuku za kilimo na kuziunga mkono nchi zinazoendelea kuwa na haki ya kupata madawa yenye bei ya chini, huenda nchi nyingi zinazoendelea hazitapinga kumchagua kuwa katibu mkuu wa shirika la WTO.

    Lakini wagombea kutoka nchi zinazoendelea pia wanaweza kupata nafasi ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa WTO. Kwani mazungumzo ya biashara ya Doha yaliyoanza mwaka 2001 yanafanyika kwa taabu sana. Ili kuyakamilisha mazungumzo hayo kabla ya mwishoni mwaka 2005, shirika la WTO linahitaji katibu mkuu mwenye uwezo na heshima. Wagombea wa nchi zinazoendela wanalingana na hali inayotakiwa, kuna uwezekano kwa mmoja kati yao kupata ushindi.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-14