Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-14 15:46:57    
Wanawake wachukua nusu ya watu waliopewa tuzo ya Nobel

cri

 

    Tarehe 10 huko Stockholm mji mkuu wa Sweden na Oslo mji mkuu wa Norway, sherehe za kutoa tuzo ya Nobel kwa mwaka 2004 zilifanyika. Katika sherehe hizo, macho ya watu duniani yalivutiwa na wanawake watatu wenye rangi tofauti , ambao walichukua nusu ya tuzo za Nobel, na jambo ambalo halijawahi kutokea hapo awali.

    Akiwa mwanasayansi mwanamke pekee aliyepewa tuzo ya Nobel, bila shaka profesa Linda Bark ni mmojawapo wa wale waliopewa tuzo la fiziolojia au udaktari ya Nobel, anastahili kusifiwa ambaye aling'ara zaidi katika sherehe hiyo. Wakati alipopokea hati, medali na fedha za tuzo ya Nobel kutoka kwa mfalme Karl wa 16 wa Sweden, watu wote walimpigia makofi kwa muda mrefu na kwa furaha kabisa.

    Tokea mwaka 1901 katika sekta ya sayansi, kulikuwa na watu 494 kwa ujumla waliopewa tuzo ya Nobel, lakini miongoni mwao kuna wanawake 11 tu, na Bibi Bark ni mwanamke wa 11 kupewa tuzo hiyo. Jambo muhimu zaidi ni kuwa, wakati Bibi Bark alipotoa hotuba kwa wanawake vijana, alisema kwa utulivu na uthabiti kuwa, "Tafadhali kufuata ndoto zako!"

    Bila shaka, mwanamke mwingine aliyevutia watu katika sherehe ya kutoa tuzo ya Nobel ya mwaka huu ni mwandishi mwanamke wa Austria Bibi Yeririck, alipewa tuzo ya fasihi ya Nobel. Ingawa hakuhudhuria sherehe hiyo kutokana na yeye kuwa na "hofu mbele ya halaiki ya watu". Lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari, yeye alikuwa akitazama sherehe hiyo nyumbani kwake. Mwakilishi wa chuo cha fasihi cha Sweden alimsomea makala ya sifia kwa lugha ya Kijerumani. Yeye alipewa fedha za Kran elfu 1, na uso wake pia ulitokeza katika televisheni, kitu alichopoteza tu ni fursa ya kushikana mkono na mfalme wa Sweden.

    Bibi Maathai wa Kenya aliyepewa tuzo ya amani ya Nobel alikuwa mhusika muhimu pekee katika sherehe iliyofanyika huko Oslo. Yeye alivaa nguo nzuri yenye rangi ya manjano na alitabasamu sana. Lakini wakati alipomsimulia ndoto yake kuhusu dunia nzuri katika siku za usoni, aligusa hisia za watu. Alisema, "Natumai watoto wote wa Afrika wanaweza kuona viluwiluwi vikichezacheza mitono." Alisema kuwa, kabla ya miaka 50 iliyopita, wakati alipokuwa mtoto, alikuwa akiangalia viluwiluwi mtoni. Lakini hivi sasa mito ya Afrika imekauka, wanawake wanapaswa kwenda pahala mbali sana kuteka maji, na "watoto hawajui kuwa wamepoteza vitu vingi."

    Baada ya sherehe iliyofanyika huko Stockholm kumalizika, watu zaidi ya 1300, wakiwemo jamaa za mfalme, maofisa muhimu wa siasa, wanachama wa mfuko wa fedha wa tuzo ya Nobel pamoja na watu waliopewa tuzo za Nobel mwaka huo, walikwenda kwenye tume ya jiji ya Stockholm kuhudhuria tafrija. Waziri wa mambo ya sayansi na teknolojia wa China Bw. Xu Guanhua ambaye aliwahi kusoma nchini Sweden pia alihudhuria tafrija hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-14