Mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran kuhusu suala la nyuklia la Iran yalifanyika tarehe 13 huko Brussels, pande mbili zinataka kutafuta njia ya kudumu ya kutatua suala la nyuklia la Iran kwa mazungumzo hayo. Ingawa Umoja wa Ulaya na Iran zina matarajio makubwa na mazungumzo hayo, lakini bado mazungumzo hayo yanakabiliwa na matatizo kadhaa makubwa.
Tatizo la kwanza, yaani ni suala moja muhimu la mazungumzo ya kutatua suala la nyuklia la Iran, ni kama Iran itasimamisha daima shughuli za urainum nzito au itasimamisha shughuli hizo kwa muda.
Mwezi uliopita Iran na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zilifanya mazungumzo na kufikia makubaliano huko Paris. Iran iliahidi kuwa katika kipindi cha kufanya mazungumzo na Umoja wa Ulaya kuhusu suala la nyuklia, itasimamisha shughuli zote zinazohusika na urainum nzito. Umoja wa Ulaya una matarajio ya kupata uhakikisho kutoka kwa Iran kuwa itatumia nyuklia kwa matumizi ya kiraia, lakini Iran inataka kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika siasa, uchumi na ufundi kwa mazungumzo hayo. Umoja wa Ulaya unaitaka Iran isimamishe daima shughuli za urainum nzito, lakini Iran inasisitiza kuwa Iran inaahidi kusimamisha shughuli za urainum nzito kwa muda tu, na kushikilia haki yake ya kuendeleza na kutumia nyuklia kwa amani.
Kutokana na hali ya hivi sasa, Iran haitaki kurudi nyuma katika suala hilo. Kabla ya mazungumzo ya tarehe 13, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Hamid Reza Asefi alisema wazi kuwa, kusimamisha daima shughuli za uranium nzito hakupo kwenye ajenda ya mazungumzo hayo, na Iran inasisitiza kusimamisha shughuli za urainum nzito kwa muda.
Tatizo la pili ni msimamo wa Marekani. Katika suala la nyuklia la Iran, msimamo wa Marekani ulikuwa wazi sana tangu mwanzo ambao inaona kuwa Iran siku zote inatengeneza kwa siri silaha za nyuklia. Kwa hivyo Marekani siku zote inalishawishi shirika la nishati ya atomiki duniani kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ili kutimiza kuiwekea Iran vikwazo. Hata kama baada ya Iran na Umoja wa Ulaya kufikia makubaliano ya kusimamisha shughuli zote zinazohusiana na uranium nzito kwa muda, Marekani inaona kuwa Iran inachelewesha wakati kwa kufikia makubaliano hayo na Umoja wa Ulaya, na Iran haitaacha kihalisi mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia. Marekani pia inasema kuwa itashikilia kwa upande mmoja haki yake ya kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Hivyo Marekani inafuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Iran. Watu wengi wanaona kuwa, kuna matatizo makubwa katika kutatua kikamilifu suala la nyuklia la Iran bila ya kushirikisha kwa Marekani.
Tatizo la tatu ni muda wa mazungumzo. Pande mbili hazikuthibitisha muda wa kuendelea na mazungumzo. Lakini Iran imesema kuwa ina matarajio kuwa mazungumzo hayo yanaweza kupata maendeleo katika miezi mitatu. Mwakilishi wa Iran kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia Bw. Hassan Rohani tarehe 12 kabla ya kwenda Brussels alisema kuwa, mazungumzo hayo yakipata maendeleo, Iran itaendelea kufanya mazungumzo. Lakini kama mazungumzo hayo hayatapata maendeleo katika miezi mitatu, Iran itaacha kufanya mazungumzo. Umoja wa Ulaya hautaki kuthibitisha ratiba ya muda wa miezi 3 wa mazungumzo. Baadhi ya maofisa wa Umoja wa Ulaya walisema kuwa, mazungumzo hayo yanahitaji muda mrefu zaidi.
Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa Iran na Umoja wa Ulaya zinakabiliwa na matatizo hayo, bado kuna umuhimu kwa Umoja wa Ulaya kutaka kutatua suala la nyuklia la Iran kwa mazungumzo ya kisiasa, ambayo yatasaidia kutatua kikamilifu suala la nyuklia la Iran.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-14
|