Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-15 14:37:44    
Watoto wa China wapenda kufanya utafiti wa saynasi

cri
Zamani, katika masomo ya shule za msingi nchini China, elimu ya sayansi ya mazingira ilikuwa inatolewa kwa wanafunzi na walimu tu. Miaka mitatu iliyopita, wizara ya elimu ya China ilizitaka shule za msingi za China kubadilisha njia ya zamani ya kuwafundisha watoto, ilisisitiza kuwa, wanafunzi waweze kupata elimu chini ya msaada wa walimu. Hivi sasa, mageuzi hayo yanafanyika katika sehemu nyingi nchini China. Matokeo mazuri ya mageuzi hayo yameonekana katika maonesho ya sayansi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya majaribio ya mkoa wa Shandong.

Shule ya msingi ya majaribio ya mkoa wa Shandong iko Ji Nan, mji mkuu wa mkoa huo. Katika maonyesho hayo mwandishi wa habari alivutiwa na Roboti moja yenye urefu wa sentimeta 40. Roboti hiyo ina ufagio na inaweza kufagia kwa kufuta mstari uliowekwa. Wagunduzi wa Roboti hiyo ambao ni wanafunzi watatu wa darasa la tano walimwambia mwandishi wa habari kuwa, wao ndiyo waliogundua na kutengeneza Roboti hiyo. Wanasema:

" roboti hiyo ilitengenezwa kwa makini sana"

" ina kifaa cha kutambua mwanga na umeme, kitu hiki kinafanana na macho ya binadamu, macho ya binadamu yanaweza kuangalia vitu, na macho ya roboti pia yanaweza kuangalia."

Guodong ni mmoja wa wagunduzi wa roboti hiyo. Alisema kuwa, wazo la kutengeneza roboti hiyo lilikuja siku moja wakati mama yake alikuwa anasafisha nyumba, mama yake alichoka sana. Wakati ule alifikiri kwamba, atatengeneza roboti moja ili kumsaidia mama kusafisha nyumba. Mpango wake uliungwa mkono na marafiki zake, hivyo walianza kutengeneza roboti hiyo."

Watoto walimwambia mwandishi wa habari kuwa, walipotengeneza roboti hiyo, walimu waliwapatia elimu ya mashine, umeme na kompyuta. Walipokutana na matatizo walisaidiana kuyaondoa kwa pamoja.

Profesa Ma Hongxu wa Chuo Kikuu cha ulinzi cha sayansi na teknolojia cha China alipoangalia roboti iliyotengenezwa na watoto alisema kuwa:

" naona kuwa, fikra ya watoto ni wazi. Kwenye kipindi cha kutafiti na kutengeneza roboti, watoto wameweza kuimarisha imani zao na kuongeza uwezo wao wa kutengeneza kitu kipya."

Mbali na roboti inayoweza kusafisha, majaribio mengine ya sayansi pia yalimvutia mwandishi wa habari. Mtoto mmoja aliwaonyesha watu wengine " Maputo ambayo hayawezi kuwa makubwa kwa kupulizwa." Mwanafunzi Wang Dequan wa darasa la nne aliipa puto moja ndani ya chupa, alipuliza puto hilo lakini halikuweza kujaa. Wanafunzi wengine walishangaa sana, Wang Dequan anasema:

" baada ya kupuliza puto, puto linatakiwa kujaa zaidi kuliko lilivyokuwa mwanzo, lakini hewa ndani ya chupa itawekea nguvu kwa puto, na nguvu hiyo inaongezeka haraka. Hiyo bila kujali unatumia nguvu kubwa kiasi gani kupuliza kujaza puto, haliwezi kubadilika kuwa kubwa."

Majaribio hayo yaliwafurahisha wanafunzi wengi sana katika maonesho hayo. Katika majaribio ya maputo ya hewa joto, mwandishi wa habari aliona kuwa, walimu wakiwaongoza wanafunzi kutengeneza Maputo ya hewa joto, wanafunzi walipangwa kufanya kazi mbalimabli, lakini mwanzoni kazi ilikuwa haiendi vizuri, baada ya kushindwa kwa mara kadhaa, wanafunzi hawakupoteza imani zao na wakaanza upya. Kutokana na jitihada za pamoja, mwishowe puto lenye hewa joto iliruka angani. Wanafunzi walifurahi sana na kusema:

" baada ya kushindwa tulikuwa na maoni ya kuacha, lakini sayansi inahitaji uvumilifu, hivyo tulipaswa kutatua matatizo bila kusita. Tuna imani kuwa, lazima tutengeneze Maputo ya hewa joto kwa mafanikio bila kujali kufanya jitihada kubwa."

Wanafunzi wengi walisema kuwa, katika shughuli hiyo walipata elimu kubwa, walikuwa na ndoto ya kuwa wanasayansi.

Kwenye maonesho hiyo, mwandishi wa habari alikuwa na maoni kuwa, watoto wana matumaunio makubwa ya kutafiti sayansi na dunia, katika siku za baadaye, wanasayansi hodari watatokana na watoto hawa.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-15