Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-15 14:55:22    
Marekani na Iraq zafanya chini juu kuweka mazingira ya usalama kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Iraq

cri
    Waziri mkuu wa serikali ya muda ya Iraq Iyad Alawi tarehe 14 alisema kuwa, msaidizi mwandamizi wa Abu Mussab al Zarqawi, kiongozi wa kundi la Al Qaeda nchini Iraq aliuawa na polisi wa Iraq, na wasaidizi wengine wawili wamekamatwa. Aliongeza kuwa viongozi wakuu wa utawala wa zamani wa Iraq watahukumiwa kuanzia wiki ijayo. Siku hiyo mwenyekiti wa baraza la pamoja la majemadari wakuu wa jeshi la Marekani Bwana Richad Myers aliitembelea Iraq kwa ghafla, yote hayo yameonesha kuwa Marekani na Iraq zafanya chini juu kuweka mazingira ya usalama kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Iraq.

    Bwana Alawi hakufahamisha lini au wapi wasaidizi wa Al Zarqawi waliuawa au kukamatwa, lakini alisisitiza kuwa, hili ni pigo kubwa kwa kundi la Al Zarqawi. Jeshi la Marekani nchini Iraq na serikali ya muda ya Iraq siku zote zinamlaani Al Zarqawi kuwa ni mpangaji na mzushi wa mashambulizi ya kimabavu yanayotokea kwa mfululizo nchini Iraq, jeshi la Marekani limetoa donge nono la dola za kimarekani milioni 25 kwa kumkamata, na bila kujali chochote lilipiga mabomu mara kwa mara na kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Fallujah ambako ilisemekana kuwa Al Zarqawi alijificha huko, lakini mpaka sasa halijaweza kumuua au kumkamata adui huyo wa Nambari ya kwanza machoni mwa jeshi la Marekani. Safari hii hotuba aliyoitoa Bwana Alawi kwenye bunge ni kama inataka kuonesha kwa watu wa nje kuwa, Zarqawi atafika mwisho wake katika kuzusha mashambulizi na vurugu.

    Katika hotuba yake kwenye bunge, Bwana Alawi alitangaza pia kuwa, mahakama husika itaanza kuwahukumu viongozi wakuu wa utawala wa zamani wa Iraq wiki ijayo. Lakini hakueleza wazi kuwa rais wa zamani Saddam atahukumiwa hivi karibuni au la. Wachambuzi wanaeleza kuwa, Alawi alitoa taarifa kama hiyo mwaka mmoja tangu kukamatwa kwa Saddam na jeshi la Marekani, na kutaka kupunguza shinikizo kubwa kutoka nchini na nje inayolikabili jeshi la Marekani nchini Iraq na serikali ya muda ya Iraq kuhusu suala la kumhukumu Saddam, pia ni kujaribu kupitia kazi ya kuwahukumu viongozi wakuu wa utawala wa zamani kufichua na shutuma za "uhalifu" wa utawala wa zamani ili kudhoofisha makundi yanayoipinga Marekani kisiasa, kiroho na ari, na kuwawezesha raia wa kawaida kuongeza chuki kwa utawala wa zamani, ili kupata uungaji mkono wao kwa utawala mpya na kuweka hali mwafaka kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwanzoni mwa mwaka kesho nchini Iraq.

    Jenerali Myers wa Marekani tarehe 14 aliitembelea Baghdad kwa ghafla, hii pia ilifuatiliwa na watu. Mwezi Aprili na Mei mwaka huu aliwahi kufanya ziara mara mbili nchini humo. Tarehe 15 mwezi Novemba, wakati jeshi la Marekani lilipoanzisha mashambuzi makubwa dhidi ya Fallujah, Bwana Myers alikwenda kufanya ukaguzi nchini Iraq. Watu waliona kuwa tarehe 14 mwezi huu alipoitembelea Iraq ndipo makundi ya kuipinga Marekani yalipoanzisha tena mashambulizi ya kimabavu tena nchini Iraq. Tangu kuanzishwa kwa vita vya Iraq, vifo vya askari wa jeshi la Marekani nchini Iraq vimefikia 1300. Kutokana na kukaribia kwa uchaguzi mkuu wa Iraq, na hali ya usalama wa Iraq bado haijawa nzuri, jeshi la Marekani limepanga kuongeza askari elfu 12 nchini Iraq ili kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Iraq unafanyika bila vikwazo. Ndiyo maana watu wanaweza kuona kuwa ziara hiyo ya Bwana Myers na msafara wake ni kwa ajili ya kulipiga jeki jeshi la Marekani nchini Iraq, ili kuwatuliza askari wa jeshi hilo. Inasemekana kuwa, Bwana Myers alifika huko pamoja na nyota wa michezo na michezo ya sanaa wa Marekani ili kuwatia moyo askari wa jeshi la Marekani walioko kwenye hali yenye tishio la kuuawa, aidha kwa kupanga mikakati mipya ya kuyapinga makundi ya kuipinga Marekani na kufanya maandalizi ya kuongeza askari wa Marekani nchini humo.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-15