Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-15 14:57:49    
Biashara kati ya Misri na Israel Yaanza Kupamba Moto

cri
    Sehemu ya viwanda nchini Misri inamaanisha kuwa kutokana na makubaliano kati ya Misri, Israel na Marekani sehemu ya viwanda itaanzishwa nchini Misri ili kuzalisha au kukamilisha bidhaa za viwanda. Kutokana na kanuni za mkataba wa QIZ bidhaa zote zilizozalishwa katika sehemu hiyo ambazo mitaji ya Israel haipungui asilimia 11.7, zitapata msamaha wa ushuru wa forodhani na hazina kiwango cha idadi.

    Waziri wa biashara na viwanda wa Misri Bw. Rashid na naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa viwanda na biashara wa Isreal Ehud Olmert na mwakilishi wa biashara wa Marekani Robert zoellick walisaini mkataba huo tarehe 14, na mkataba huo utatekelezwa baada ya kupitishwa katika bunge la umma la Misri. Kabla ya kutia saini, rais wa Misri Hosni Mubarak alikutana na Bw.Zoellick na Bw.Olmert na walijadiliana namna ya kutekeleza mkataba huo wa QIZ na kustawisha ushirikiano wa biashara kati ya nchi hizo tatu. Baada ya majadiliano yao, msemaji wa rais wa Misri, Maged abdel Fattah, alitangaza kuwa Misri inafurahia ushirikiano wa biashara kati yake na Israel na kutaka kusukuma mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Bw. Zoellick pia alisema kuwa, Marekani inapenda kusukuma mbele ushirikiano kati ya Israel na nchi za Kiarabu katika nyanja mbalimbali. Israel ilidai kuwa mkataba huo wa QIZ ni hatua ya kihistoira katika uhusiano kati ya Misri na Isreal.

    Baada ya Jordan, Misri ni nchi ya pili iliyotia saini mkataba wa QIZ na nchi za Isreal na Marekani. Mapema mwaka 1996 Marekani ilikuwa na mpango wa kusaini mkataba na nchi za Misri na Israel kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa biashara kati ya Israel na nchi nyingine pembezoni na kusukuma mbele mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati. Lakini kutokana na msukosuko wa Mashariki ya Kati, na Misri kuwa na tahadhari kuhusu ushirikiano na Israel, Misri ilikuwa haina hamu na mkataba huo. Marekani ilikuwa na kinyongo na msimamo huo wa Misri, na hii ndio sababu muhimu ambayo mazungumzo ya kuanzisha sehemu ya viwanda nchini Misri hayakuwa na maendeleo yoyote katika miaka mingi iliyopita. Marekani inashikilia kwamba mkataba wa QIZ ni hatua ya mwanzo katika kuanzisha sehemu ya biashara huria kati ya Marekani na Misri.

    Wachambuzi wanaona kuwa kusainiwa kwa mkataba wa QIZ kunamaanisha uhusiano wa "vita vya baridi" umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo. Mabadiliko ya msimamo wa Misri yanatokana na sababu nyingi. Kwanza, rais wa Marekani Bw. Bush ameshinda uchaguzi mkuu na kuendelea na kipindi kingine cha urais, uongozi wa Palestina umebadilika na Israel itatekeleza mpango wake wa upande mmoja, hali kama hiyo imeathiri hali ya siasa ya Mashariki ya Kati, kwa hiyo Misri inataka kubadilisha sera zake za mambo ya nje na kuweka uhusiano mzuri kati yake na Israel. Pili, matunda mazuri kutokana na Jordan kutia saini mkataba wa QIZ na Marekani yaliitia moyo Misri. Tatu uchumi wa Misri ulizorota katika miaka ya karibuni, hali ya maisha ya wananchi kiuchumi imebadilika kuwa mbaya kwa haraka, kwa hiyo serikali ya Misri inakabiliwa na tatizo la uchumi, na mkataba wa QIZ utailetea Misri nafasi za ajira laki mbili na nusu na kuingiza doda la Kimarekani bilioni 5 nchini humo.

    Wachambuzi wanaona kuwa Misri ni nchi ya kwanza ya Kiarabu kuwa na uhusiano na Israel, na kutokana na nafasi muhimu iliyonayo kijiografia na katika mambo ya kimataifa, uhusiano wa biashara kati ya Misri na Israel utaleta taathira kubwa ya kisiasa ya kikanda. Lakini wakati huo inafaa kutia maanani kuwa hivi sasa kelele za kupinga Israel nchini Misri zimekuwa kubwa, mustakbali wa mkataba wa QIZ kati ya Misri, Israel na Marekani utaathiriwa na mabadiliko ya hali ya kisiasa ya Mashariki ya Kati.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-15