Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-16 20:58:55    
Palestina yakabiliana na uamuzi muhimu kuhusu mkakati wake kwa Israel

cri

    Siku za karibuni, mgogoro kati ya pande mbalimbali za Palestina kuhusu mkakati wa nchi hiyo kwa Israel umeonekana wazi. Kundi la wanasiasa wenye msimamo wa pole linaloongozwa na mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji ya chama cha ukombozi wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas waliona kuwa Palestina inapaswa kukomesha mapambano ya kisilaha dhidi ya Israel, lakini makundi yenye siasa kali, yakiwa ni pamoja na kundi la Hamas, yanapinga pendekezo hilo.

    Bw. Abbas siku zote anapinga vitendo vya kimabavu na kuunga mkono mazungumzo ya amani. Katika duru jipya la migogoro kati ya nchi hizo mbili iliyoanzia mwezi Septemba mwaka 2000 na kuendelea kwa miaka minne, alisema mara nyingi kuwa, matumizi ya nguvu yataathiri sana maslahi ya wa-Palestina, nchi hizo mbili zinapaswa kutatua migogoro kupitia mazungumzo, lakini msimamo wake haukukubaliwi na wa-Palestina wote. Baada ya migogoro ya miaka minne, wa-Palestina wameanza kupinga vitendo vya kimabavu na kuwa na matumaini makubwa ya amani, na Bw. Abbas amekuwa kiongozi wa nchi hiyo anayekaribishwa sana na umma hivi karibuni.

    Uungaji mkono kwa makundi yenye siasa kali umeanza kupungua na mkakati wake wa mapambano ya kisiasa umekuwa ukipingwa siku hadi siku. Aidha, hatua za kijeshi za Isreal za "kuangamiza mmoja mmoja" zimetoa pigo kubwa kwa makundi hayo, miundo yeke na viwanda vyake vya kutengeneza silaha vimeteketezwa, viongozi wake wamelazimishwa kujificha, na ni vigumu kwao kuanzisha tena mashambulizi makubwa dhidi ya Israel.

    Jumuiya ya kimataifa imetoa mazingira mazuri kwa Bw. Abbas kutekeleza sera yake ya kuleta amani, kuhimiza makundi mbalimbali ya wanamgambo wa Palestina kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel. Baada ya kutokea kwa mashambulizi dhidi ya Israel tarehe 12 mwezi huu, Israel ilisema haitaanzisha hatua kubwa ya kijeshi ya kulipiza kisasi, ili kukwepa kuharibu juhudi za Bw. Abbas kulinda hali tulivu ya kisiasa ya nchini Palestina. Marekani, Umoja wa Ulaya na Russia zilimwunga mkono Bw. Abbas kwa nija ya kutoa taarifa ya kisiasa na kuahidi kutoa misaada ya kiuchumi kwa Palestina. Inayofuatiliwa sana ni kwamba Misri inayokuwa na athari kubwa kwa makundi ya siasa kali ya Palestina inamwunga mkono haradhani Bw. Abbas na kuimarisha juhudi zake za kusuluhisha mgogoro kati ya nchi hizo mbili.

    Hivi karibuni, maendeleo muhimu ya hali ya siasa ya Palestina ni kwamba, baadhi ya makundi yenye siasa kali na athari kubwa yalipokataa mwito wa Bw. Abbas wa kusimamisha vita, pia yalijiwekea nafasi ya kufanya usuluhishi. kiongozi wa kundi la Hamas Bw. Khaled Mashal alipohojiwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC tarehe 13 mwezi huu, alisema kuwa kundi la Hamas halitakubaliana na Israel kuhusu kusimamisha vita, isipokuwa Palestina itafanya upigaji kura wa maoni ya raia au pande mbalimbali za nchi hiyo kufikia makubaliano kuhusu suala hilo. Kiongozi mmoja wa kundi la Jihad la Palestina alitaka utawala wa Palestina na pande mbalimbali za nchi hiyo kuweka mfumo kuhusu mapambano ya kisilaha na kisiasa, ili kusawazisha misimamo ya pande mbalimbali.

    Habari zinasema kuwa, idara ya mamlaka ya utawala wa Palestina hivi sasa inafanya juhudi kuweka utaratibu wa ushirikiano na makundi yenye siasa kali, kuruhusu makundi hayo kushiriki kwenye mchakato wa utoaji sera wa idara hiyo, ili kubadilisha kwa ushirikiano wake katika suala la kusimamisha vita. Wachambuzi wanaona kuwa, kama Bw. Abbas akiweza kutumia hali nyingi nzuri ya ndani na nje na kufikia makubaliano na makundi mbalimbali ya wanamgambo kuhusu kutimiza lengo la kusimamisha vita, hali hiyo itasaidia sana kurejea kwenye mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili na kuanzisha tena mchakato wa amani.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-16