Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-16 17:32:13    
Kampeni ya uchaguzi mkuu wa Iraq yaanza rasmi

cri

    Kazi ya kuandikisha wagombea wa uchaguzi mkuu wa Iraq ilimalizika jana alasiri ya saa za huko Baghdad. Kampeni ya uchaguzi mkuu imeanza rasmi jana na itafanyika kwa wiki 6.

    Msemaji wa Tume kuu ya uchaguzi ya Iraq Bwana Farid Ayar aliwaambia waandishi wa habari kuwa, vyama zaidi ya 70 vimejiandikisha kushiriki kwenye uchaguzi huo, tume hiyo imepata orodha 83 za maji ya wagombea pamoja na wagombea huru waliojiandikisha. Wagombea wapatao 3500 kwa ujumla watagombea viti 275 vya bunge la mpito la Iraq.

    Kutokana na katiba ya muda ya Iraq, uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 30 Januari utachagua bunge la mpito, baadaye bunge hilo litachagua serikali mpya ya mpito. Bunge la mpito linapaswa kutunga katiba ya kudumu kabla ya tarehe 15 Agosti, na kuipigia kura ya maoni ya raia kabla ya tarehe 15 Oktoba mwakani, kama itapitishwa, Iraq itafanya uchaguzi mkuu mpya kabla ya mwishoni mwa mwaka kesho kwa kufuata katibu ya kudumu, ili kuchagua bunge na serikali rasmi.

    Chama cha maafikiano ya kitaifa cha Iraq ambacho ni cha waziri mkuu wa serikali ya muda ya Iraq Iyad Alawi kimeshirikiana na vyama vingine na watu huru kuunda shirikisho kubwa la ugombeaji. Shirikisho hilo limetoa orodha ya wagombea 240. Bwana Alawi alitoa hotuba ya ugombeaji jana akisema kuwa, wataondoa hali isiyo ya haki kwenye jamii iliyokuwepo katika kipindi cha utawala wa rais wa zamani Saddam, kuacha siasa kali ya dini na madhehebu, kuzika yote yaliyopita, na kuijenga Iraq kuwa nchi yenye mshikamano, muungano na usitawi. Bwana Alawi alisema kuwa, kujenga upya kikosi cha askari polisi cha Iraq kutaiwezesha serikali kuyataka majeshi ya nchi nyingi yaondoke kutoka Iraq. Pia ameahidi kuimarisha usalama wa nchini na kupinga uingiliaji wa nchi za nje dhidi ya mambo ya ndani ya Iraq.

    Mbali na shirikisho hilo la ugombeaji linaloongozwa na Alawi, shirikisho lingine linaloundwa na vyama vikubwa vya madhehebu ya Shia limetoa orodha ya wagombea 228 iliyoidhinishwa na kiongozi mwenye athari kubwa kabisa la madhehebu ya Shia Ayatollah Ali Sistani. Vyama vikubwa vya kabila la wakurd vya sehemu ya kaskazini ya Iraq, na vyama vikubwa vya madhehebu ya Suni pia vimetoa orodha zao za wagombea kabla ya siku ya mwisho ya kujiandikisha.

    Wakati huohuo, hivi sasa bado kuna vyama 47 ambavyo vimetangaza kususia uchaguzi mkuu, na vyama hivyo vingi ni vya madhehebu ya Suni. Vyama kadhaa vya madhehebu ya Suni pamoja na chama cha Kiislamu vinashikilia kuahirisha uchaguzi mkuu kwa miezi 6 hadi hali ya usalama wa Iraq itakapokuwa nzuri na mchakato wa maafikiano ya kitaifa utakapopata maendeleo, ili watu wengi waweze kushiriki kwenye upigaji kura. Chama cha Kiislamu kimesema kuwa, kama uchaguzi mkuu hautaahirishwa, hakiwezi kuondoa uwezekano wa kususia uchaguzi mkuu mwishowe.

    Aidha, mshauri mkuu wa kisiasa wa kiongozi wa kundi linaloipinga Marekani la Moqtad Sadr alisema kuwa, sababu kubwa ya kundi hilo kutoshiriki na kutounga mkono uchaguzi mkuu ni kuwa utawala wa Marekani na Iraq kuendelea kuwakamata wasaidizi wa Sadr, kuzuia uhuru wa Sadr na kukataa kundi la Sadr kuanzisha upya ofisi yake huko Najaf. Ofisi ya Sadr tarehe 14 ilieleza wazi kuwa Sadr na wenzake kushiriki uchaguzi mkuu lazima kuhusihwe kwenye msingi wa kuhusisha na ratiba ya kuondoka kwa majeshi ya nje baada ya uchaguzi mkuu.

    Waziri wa mambo ya nje wa serikali ya muda ya Iraq Hoshyar Zebari tarehe 14 alisema kuwa, uchaguzi mkuu wa Iraq utakabiliwa na matatizo matatu makubwa yaani hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya itazuia au kuyumbisha mchakato wa uchaguzi; wapigaji kura hawatathubutu kupiga kura kwa kuofia kushambuliwa na magaidi; na namna ya kuhakikisha haki na uwazi wa uchaguzi mkuu. Hivyo ingawa kampeni za uchaguzi zimeanza, kama uchaguzi mkuu wa Iraq utafanyika kwa wakati uliowekwa au la, na usalama, uwazi na haki za uchaguzi huo utahakikishwa au la, bado ni masuala yanayofuatiliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-16