Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-16 17:45:54    
Mji wa Xi'an

cri

    Mji wa Xi'an katika enzi za kale uliitwa Chang'an na pia uliwahi kuitwa Xidu, Xijing, Daxingcheng, Jingzhaocheng, Fengyuancheng n.k. Mji huo ni mji ambao umewahi kuwa mji mkuu mara nyingi na kwa muda mrefu zaidi katika historia ya China. Umewahi kuwa mji mkuu wa enzi 12 zikiwemo Zhou ya Magharibi, Qin, Han ya Magharibi, Xin, Jin ya Magharibi(wakati mfalme Min aliposhika madaraka), Zhao ya Kwanza, Qin ya Kwanza, Qin ya Pili, Wei ya Magharibi, Zhou ya Kaskazini, Sui na Tang kwa miaka zaidi ya elfu 11, na pia umewahi kuwa mji mkuu wa mamlaka za mapinduzi ya wakulima yakiwemo mamlaka ya Chimei, Lulin, Daqi na Dashun. Kuanzia karne 11 K.K. hadi mwishoni mwa karne 9 b.k, mji huo ulikuwa kituo cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni nchini China.

  

    Mji wa Xi'an una historia ya zaidi ya miaka elfu 3. Matukio mengi yenye athari kubwa yamewahi kutokea huko. Karne 11 K.K., mfalme Wen wa dola la Zhou alijenga mji mkuu huko Fengjing magharibi ya Mto Feng, baadaye mtoto wake mfalme Wu aliposhika madaraka aliangusha utawala wa mfalme Zhou, na kumaliza Enzi ya Shang na kuanzisha Enzi ya Zhou ya Magharibi. Alijenga mji mkuu huko Haojing mashariki ya Mto Feng, baada ya hapo, mji wa Xi'an ulianza kuwa kituo cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni nchini China kwa muda mrefu. Mwaka 841 k.k., mjini Haojing ulikumbwa"mgogoro wa wananchi" ambao ulikuwa mgogoro mkubwa wa kwanza wa kumuondoa madarakani mfalme ulioanzishwa na wananchi. "Utawala mzuri wa kipindi cha Chengkang" mwanzoni mwa Enzi ya Zhou ulionesha ustawi wa jamii ya kitumwa ya wakati huo. Katika enzi ya Madola ya Kivita, Mageuzi yaliyoanzishwa na Shangyang wakati mfalme Xiaogong wa Dola la Qin aliposhika madaraka yalikuwa mageuzi makubwa yaliyoisukuma jamii ya China kuwa jamii ya kimwinyi. Katika enzi ya Tang, "utawala mzuri wa kipindi cha Zhenguan" na "utawala mzuri wa kipindi cha Kaiyuan" ulionesha kuwa jamii ya kimwinyi nchini China ilifikia kilele chake. Mwaka 138 k.k. katika enzi ya Han, mfalme Wu alimtuma Zhangqian kwenda sehemu ya magharibi ya China, na kuanzisha "njia ya hariri" iliyoanzia Chang'an na kuungana pamoja na Ulaya na Asia.

    Mwaka 582 katika enzi ya Sui, mfalme Wen alitoa amri ya kujenga mji mkuu mpya DaxingCheng (uko sehemu ya mji wa Xi'an wa sasa) kusini magharibi ya mji wa Chang'an uliojengwa katika enzi ya Han. Katika enzi ya Tang mji huo uliitwa Chang'an tena. Ujenzi wa mji huo uliendelea kwa miaka 72 kuanzia mwaka 582 wakati mfalme Wen wa Enzi ya Sui aliposhika madaraka hadi mwaka 654 wakati mfalme Gaozong wa Enzi ya Tang aliposhika madaraka. Eneo lake lilikuwa kilomita za mraba 84.1. Mji huo ulipangwa vizuri ambapo sehemu ya magharibi na ya mashariki zinalingana na uligawanywa katika sehemu tatu yaani sehemu ya kasri, ya serikali na ya nje. Ujenzi wa mji huo ulionesha ustawi wa jamii ya kimwinyi ya wakati huo, na pia una athari kubwa katika historia ya ujenzi na ya miji nchini China.

    Mji wa Xi'an uko katikati ya maeneo ya kiuchumi ya magharibi na ya mashariki ya China, na ni njiapanda kwa watu wa mikoa ya kaskazini magharibi kwenda mikoa ya kusini magharibi, mikoa ya sehemu ya kati na mikoa ya mashariki mwa China, pia ni mji mkubwa kwenye reli ya Longhai na ya Lanxin ambazo ni sehemu moja ya daraja la kuunganisha Asia na Ulaya. Pia uko katika sehemu muhimu ya kimkakati ya kuunganisha uchumi wa Mashariki na Magharibi ya China. Sehemu nzuri ya kijiografia na sababu ya kihistoria imeufanya mji huo kuwa kituo kikubwa cha maingiliano ya bidhaa katika sehemu ya kaskazini magharibi mwa China; na historia ndefu na maliasili nyingi za kiutamaduni zimeufanya kuwa mji wa kwanza miongoni mwa miji mikuu 6 ya kale nchini China, mmoja kati ya miji mikuu minne ya kale duniani, na mji maarufu wa kitalii. Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya watu wa China, mji wa Xi'an umepata maendeleo makubwa na kuwa kituo muhimu cha viwanda hasa viwanda vya ulinzi wa taifa, kituo cha utafiti wa sayansi na teknolojia na kituo cha elimu ya juu.

  

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-15