Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-20 20:34:23    
Vivutio vya mji maarufu wa kauri Jindezhen

cri
Kwa lugha ya kiingereza, herufi za neno "kauri" na "China" ni sawasawa, huu ni ufafanuzi mzuri kabisa kuhusu historia ndefu ya China ya kutengeneza vyombo vya kauri na ustadi mzuri wa utengenezaji huo. Ustadi mzuri wa China wa utengenezaji wa vyombo vya kauri umewawezesha watu duniani kufurahia vyombo murua vya sanaa na kuandika historia inayong'ara ya vyombo vya kauri vya China. Kutokana na hayo, miji mingi imejulikana nchini na ulimwenguni kutokana na shughuli za utengenezaji wa vyombo vya kauri, kati ya miji hiyo mji wa Jingdezhen ni maarufu zaidi. Leo tunawaongoza kwenda Jingdezhen kutembelea.

Mji wa Jingdezhen uko katika sehemu ya kaskazini mashariki ya mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China. Kabla ya miaka zaidi ya 290, wakati mmisionari wa Ufaransa Pere d'Entrecolles alipofika kwa mara ya kwanza kwenye mji wa Jingdezhen aliona kuwa mji huo uko katika eneo la tambarare liliyozungukwa na milima midogomidogo, ambapo mito miwili iliyotiririka kutoka milimani inakusanyika pamoja kwenye sehemu hiyo na kuwa bandari nzuri yenye urefu wa zaidi ya kilomita moja. Ukiingia ndani ya bandari hiyo kwanza unaweza kuona umbo wa mji huo unaokumbwa na moto na moshi unaopeperuka juu popote pale mjini, na usiku mji huo unaonekana kama mji unaokumbwa na moto.

Jingdezhen ni mji unaotegemea shughuli za aina moja tu za utengenezaji wa mikono wa vyombo vya kauri, matanuri ya kutengenezea vyombo vya kauri yapo karibu kila mahali kwenye kando ya mto, ambayo yanachoma moto vyombo vya kauri kila siku bila kuzimwa kwa zaidi ya miaka elfu mbili. Vyombo vya kauri ni kama roho na maisha ya mji huo, kama vyombo vya kauri visingelikuwepo, basi hata mji wa Jingdezhen usingekuwepo.

Kutokana na vyombo vya kauri, mji wa Jingdezhen unaonekana na sura nzuri na utajiri. Mji huo wenye idadi ya watu milioni 1.4 kama miji mingine ya China ilivyo, una barabara pana na nyumba za ghorofa, lakini historia yake ndefu ya utengenezaji wa vyombo vya kauri inaonekana dhahiri zaidi na vyombo vyake vya kauri vinawavuta sana watalii wa nchini na ng'ambo.

Shughuli za utengenezaji wa vyombo vya kauri katika mji wa Jingdezhen zilianza miaka 2000 iliyopita. Hivi sasa mabaki ya matanuri makubwa ya kale ya utengenezaji wa vyombo vya kauri bado yanahifadhiwa vizuri mjini humo na sehemu za pembezoni mwa mji huo. Hali ya kuvutia zaidi ni kuwa, hapo awali, mji huo uliumbika siku hadi siku kutokana na matanuri ya utengenezaji wa vyombo vya kauri, ambapo matanuri yalikuwa kiini cha mji. Mwenyeji wa huko Bwana Zheng Peng akifahamisha alisema:

Katika sehemu ya mji mkongwe, hatuwezi kuonanjia au hata kichochoro hata kimoja kilichonyooka. Katika kichochoro cha Pengjialon, gofu la tanuri linaonekana dhahiri, na majengo ya huko yote yamepangwa kwa kuzunguka tanuri hilo. Hivi sasa katika sehemu ya mji mkongwe, majengo yaliyopangwa namna hiyo yako karibu kila mahali, ambayo yanaonesha usitawi wa viwanda vya utengenezaji wa vyombo vya kauri katika zama za kale huko Jingdezhen.

Katika mji wa Jingdezhen, vyombo vya kauri vinaonesha kuwa ni mali na utamaduni kwa wenyeji wa huko, na pia vinauhusiano wa moja kwa moja na maisha ya wakazi wa huko. Matofali ya matanuri ya utengenezaji wa vyombo vya kauri kila mwaka hubadilika upya, yaliyoachwa yanakuwa vifaa vya ujenzi wa nyumba za wakazi. Mpaka sasa nyumba nyingi zilizojengwa kwa matofali yaliyotumika kujengea matanuri ya kauri, bado yako katika sehemu ya mji mkongwe wa Jingdezhen. Bwana Zheng alisema:

Matofali hayo ni magumu sana ambayo ni vifaa vizuri vya ujenzi wa nyumba, nyumba zilizojengwa kwa matofali hayo ziko mjini Jingdezhen tu, na huwezi kuziona katika sehemu nyingine kote duniani.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-20