Ofisa wa Umoja wa Afrika ambaye yuko mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria kusuluhisha mgogoro huko Darfur, Sudan jana alithibitisha kuwa umoja huo umewaamrisha wakaguzi wake kusimamisha kwa muda shughuli za kusimamia usimamishaji wa vita huko Darfur nchini Sudan, ili kuchunguza tukio kuhusu kushambuliwa kwa helikopta moja ya umoja huo. Ofisa huyo alieleza, mashambulizi hayo yanaonesha kuwa mgogoro kati ya pande mbalimbali bado unaendelea na mazungumzo ya amani ya duru jipya yanakabiliwa na hatari ya kuvurugika.
Habari zinasema kuwa helikopta hiyo iliyokuwa imewabeba wakaguzi wa kusimamia usimamishaji wa vita wa Umoja wa Afrika tarehe 19 ilipokuwa ikitekeleza majukumu katika sehemu ya kusini mwa Darfur, ilishambuliwa kwa silaha kutoka ardhini na watu wasiojulikana, lakini helikopta hiyo na watu waliokuwa kwenye ndege hiyo wote hawakujeruhiwa. Ofisa wa Umoja wa Afrika alieleza kuwa uchunguzi unafanyika ili kuangalia nani alihusika na shambulizi hilo.
Siku hiyo, ujumbe wa serikali ya Libya ulianza kufanya usuluhishi kuhusu kutuliza mgogoro wa Darfur. Kabla ya hapo, mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo na viongozi wengine wa Afrika walieleza kushirikiana katika usuluhishi na kuzisaidia pande mbalimbali kuokoa mchakato wa amani.
Kutokana na mpango wa Umoja wa Afrika, serikali ya Sudan na makundi mawili ya upinzani ya Darfur tarehe 11 yalianza kufanya mazungumzo ya amani ya duru la tatu. Kama ilivyokuwa kwa mazungumzo hayo yaliyopita, mazungumzo ya duru hilo yalipoanza yaliendelea kwa vikwazo.
Wakaguzi wa Umoja wa Afrika walioko katika sehemu ya Darfur tarehe 17 walitoa taarifa ikieleza kuwa pande zote zinazopambana nchini Sudan zote zilikiuka mkataba wa kusimamisha vita na mgogoro kati yao bado unaendelea. Siku hiyo, Umoja wa Afrika ulitoa onyo la mwisho kwa pande hizo mbalimbali na kuzitaka zisimamishe mgogoro ndani ya 24. Umoja huo pia ulieleza kuliomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua zinazostahili kwa upande ambao hautekelezi mkataba wa kusimamisha vita.
Taarifa hiyo inasema kwa kuwa wakaguzi wa Umoja wa Afrika ni wachache, ni vigumu sana kueleza ni upande upi unachochea mgogoro huo. Habari nyingine zinasema kuwa kwa kuwa makundi ya upinzani siku zote yanatumai kuliwasilisha suala la Darfur katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ili Marekani na nchi nyingine za magharibi ziingilie kati mgogoro huo na kulifanya suala hilo kuwa la kimataifa, kwa hiyo haiwezi kuondoa uwezekano wa kitendo cha makundi ya upinzani cha "mwizi kupiga mayowe ya kukamata mwizi mwingine" kwa lengo la kuchochea mgogoro huo na kuharibu mazungumzo ya amani ya Abuja, ili kuulazimisha Umoja wa Afrika kuliwasilisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kama malengo ya makundi ya upinzani yatafanikiwa, mazungumzo ya amani ya Abuja ya duru hilo yatakabiliwa na hatari ya kuvurugika na suala la Darfur pia litakuwa gumu zaidi.
Idhaa ya Kiswahili 2004-12-21
|