Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-21 21:05:07    
Sekta ya biashara ya rejareja yaimarika katika ushindani

cri
Bibi Su Adai, ambaye anafanya kazi katika kampuni moja mjini Shanghai, shughuli anazopenda zaidi katika nyakati za mapumziko ni kutembelea madukani. Anasema kuwa mjini Beijing kuna maduka mengi makubwa, kuna ushindani mkali kati ya maduka ya kichina na wafanyabiashara wa kigeni, ambao unanufaisha wateja wa kawaida kama yeye, alisema,

"Mimi nikiwa mteja ninaona kuwa kampuni za kigeni kuingia kwenye sekta biashara ya rejereja kunatunufaisha. Wafanyabiashara wa kigeni na wa kichina wanatuletea bidhaa nyingi zaidi, tunaweza kuchagua bidhaa tunazopenda; kutokana na ushindani kati ya wafanyabiashara wa nchini na wa kigeni bei za bidhaa zitakuwa za nafuu zaidi, na tutaweza kupata bidhaa kwa bei rahisi."

Katika siku za usoni, ushindani kati ya maduka ya wafanyabiashara wa China na wa nchi za kigeni wa kuvutia wateja hautakuwa katika miji mikubwa kama Beijing, Shanghai na Guangzhou tu, bali ushindani huo utaenea hadi miji mingi ya wastani na midogo. Kutokana na ahadi ilizotoa China wakati ilipojiunga na Shirika la Biashara Duniani, WTO, toka tarehe 11 mwezi Desemba mwaka huu, sekta ya biashara ya rejareja itakuwa wazi kwa wafanyabiashara wa kigeni, ambao wataweza kufungua maduka katika miji yote ya China na kwa idadi wanayotaka.

Sekta ya biashara ya China ilianza kufungua mlango katika mwaka 1992. Hadi hivi sasa zaidi makampuni ya 40 kati ya makampuni makubwa 50 ya kimataifa yameanzisha matawi yake nchini China; na zaidi ya maduka 2000 makubwa yamefunguliwa na makampuni ya nchi za.

Kampuni ya Wal-mart ya Marekani, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa miongoni mwa kampuni za biashara ya bidhaa ya rejareja duniani, ingawa ilichelewa kufungua maduka yake hapa nchini, lakini imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika shughuli zake. Hivi karibuni, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Wal-mart duniani alitembelea tena China, alisema kuwa anafurahia maendeleo iliyopta Wal-mart nchini China na kuwa na imani na mustakabali wa kampuni hiyo nchini China.

"Katika miaka minane iliyopita Wal-mart iliwekeza vitega-uchumi na kufungua matawi katika miji mingi ya China. Ninawaambia kwa furaha kuwa Wal-mart sasa inaimarika kwa haraka nchini China, mauzo yetu yanaongezeka, idadi ya wafanyakazi inaongezeka na idadi ya matawi yetu pia inaongezeka. Hivi karibuni nilihudhuria sherehe ya uzinduzi ya tawi la Wal-mart mjini wuhan, hili ni tawi letu la 40 nchini China. Mwaka huu tutaendelea kufungua matawi yetu nchini China."

Habari zinasema kuwa katika mwaka 2005, Wal-mart itafungua matawi zaidi ya 10 nchini China.

Ni dhahiri kuwa kampuni yenye imani juu ya maendeleo yake nchini China siyo Wal-mart peke yake. Washindani wakubwa wa Wal-mart, ambao ni Carrefour ya Ufaransa na Metro, makampuni hayo makubwa ya kimataifa pia yana mipango mikubwa ya maendeleo nchini China. Kampuni ya Carrefour, ambayo iliingia nchini China mapema zaidi, imesema kuwa idadi ya matawi yake nchini China itazidi 100 katika miaka mitatu ijayo.

Kampuni za nchi za kigeni hususan makampuni makubwa ya kimataifa ya biashara ya bidhaa rejareja kuingia nchini, kutaleta shinikizo na changamoto kubwa kwa maduka mengi ya China. Kwa maduka mengi ya China, yaliondokana na usimamizi wa uchumi wa kimpango muda si mrefu uliopita, na bado ni muda mfupi tu kwa maduka hayo kupiga hatua ya maendeleo katika mazingira ya uchumi wa kimasoko, na hayajapata uzoefu mkubwa. Kwa maduka binafsi yaliyoibuka hivi karibuni, ingawa yana ari kubwa ya kujiimarisha katika sekta ya biashara, lakini yanakabiliwa na matatizo mengi ya upungufu wa mitaji na ufanisi.

Kutokana na kukabiliwa na changamoto kutoka kwa maduka makubwa ya kampuni za kigeni, maduka ya China yamechagua njia ya kujirekebisha na kukuza nguvu na uwezo wake. Shanghai Brilliance (Group) Co. Ltd ni kampuni iliyoanzishwa kutokana na wazo hilo katika mwezi Aprili mwaka 2003.

Baadhi ya wataalamu wa uchumi pia wametoa mawazo yao juu ya maendeleo ya maduka ya China katika siku za usoni. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti kuhusu makampuni ya kimataifa Bw. Zhang Xiaoyu alisema kuwa hali bora ya makampuni makubwa ya kimataifa ni majina yao maarufu yaliyojulikana sana duniani. Ikilinganishwa na makampuni hayo, maduka ya China bado yako nyuma sana. Anaona kuwa maduka ya rejareja ya China yanapaswa kuongeza sifa zao, na jambo la kwanza linalotakiwa kufanywa ni kuongeza sifa na imani ya watu.

"Ninaona kuwa hata kama maduka ya rejareja hata yameunganishwa kuwa kampuni kubwa namna gani, yanapaswa kuzingatia mambo mawili, la kwanza yasiuze bidhaa hafifu au za bandia, pili ni kuboresha usimamizi wake."

Bwana Zhang alisema kuwa kampuni kama ya Wal-mart inajali sana bidhaa inazonunua. Kwani endapo inauza bidhaa hafifu au za bandia, basi sifa yake itafifia kwa haraka.

Takwimu zinaonesha kuwa pamoja na maendeleo ya uchumi wa China, ambapo pato la wastani kwa mtu ni zaidi ya dola za kimarekani 1,000 uwezo wa mchina wa kununua bidhaa umeongezeka kwa mfululizo. Hivyo katika mazingira ya soko la biashara ya rejareja lenye ushindani mkubwa, kampuni inayoweza kuwapatia wateja bidhaa bora kwa bei nafuu na huduma nzuri, itawavutia wateja wengi.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-21