Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-22 16:49:51    
Namna ya kupika mabilingani na mchuzi wa saumu wenye pilipili ulio na ladha ya samaki

cri

Mahitaji

Mabilingani gramu 300, mayai 3, wanga gramu 100, vipande vya vitunguu saumu, tangawizi, vitungu maji gramu 50 kwa mbalimbali, pilipili nyekundu gramu 50, chumvi gramu 2, mchuzi wa soya gramu 5, sukari gramu 10, siki gramu 5, mvinyo wa kupikia gramu 5,MSG gramu 1, mafuta yaliyokwisha chemka gram 500.

Njia

1. menya mabilingani na uyaoshe, katakata katika vipande vyenye upana wa sm 2 na urefu wa sm 5, koroga mayai na kuyachanganya pamoja na wanga, kata pilipili nyekundu iwe vipandevipande.

2. Tia gramu 500 za mafuta yaliyokwisha chemshwa ndani ya sufuria, yapashe moto mpaka yawe na joto la asilimia 50-60. Chovya vipande vya mabilingani ndani ya mayai yaliyokorogwa, halafu vitie ndani ya mafuta, kaanga mpaka viwe vya rangi ya dhahabu, viopoe.

3. Tia kiasi kidogo cha mafuta, halafu tia vipandevipande vya pilipili nyekundu na vipande vya vitunguu maji na tangawizi ndani ya sufuria, vikaange kwa dakika chache. kisha mimina maji kidogo ndani ya sufuria hiyo, tia chumvi, M.S.G, mchuzi wa saumu, siki na mvinyo wa kupikia, koroga kidogo, halafu weka maji ya wanga, mpaka hapo ipakue na kumimina juu ya vipande vya mabilingani vilivyokaangwa, kitoweo hiki sasa kiko tayari.