Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-22 21:15:52    
Barabara za kasi zaingia katika sehemu zilizo maskini kabisa nchini China

cri

    Kutokana na ujenzi wa miundo mbinu kuendelea kupanuka, barabara za kasi pia zinaingia katika mji wa Dingxi, mkoani Gansu na sehemu ya Xihaigu iliyoko katika mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia. Ujenzi wa barabara hizo umeweza kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi wa sehemu hizo mbili ambazo bado ziko nyuma kabisa nchini China kuondokana na umaskini.

    Mwezi Oktoba, mwaka 2002, barabara ya kasi inayounganisha wilaya mbili kati ya mji wa Dingxi na mji wa Lanzhou ilianza kutumika, ambayo ni barabara ya kwanza ya kasi mjini Dingxi. Inakadiriwa kuwa hadi mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu, barabara ya pili ya kasi, yaani barabara ya kasi ya Lanlin itakuwa imekamilika; pia katika sehemu ya Xihaigu, mkoani Ningxia, barabara ya kasi inayoanzia kutoka mji wa Yinchuan hadi wilaya ya Yanchi, mjini Wuzhong itakuwa imetumika kwa zaidi ya miaka miwili, na barabara ya kasi kati ya Yinchuan na Wuhan, ambayo itapita sehemu ya Xihaigu pia ujenzi wake unaendelea kwa kasi.

    Gavana mkuu wa kanda ya Shanxi na Gansu katika mwisho wa enzi ya Qing Zuo Zongtang aliwahi kumweleza mfalme wa Qing kuwa, sehemu ya Longzhong "ilikuwa maskini kabisa nchini China". Hapa Longzhong aliyoitaja ni pamoja na sehemu za Dingxi na Xihaigu za hivi sasa. Kwa kuwa hali ya huko ilikuwa mbaya, miundo mbinu ilikuwa mibovu, na kwa muda mrefu wakulima wa huko hawakuwa na chakula na nguo za kutosha, hivyo zilikuwa sehemu zilizo maskini kabisa nchini China. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, sehemu hizo mbili zilichukuliwa kuwa sehemu ya "maskini kabisa duniani" na shirika la fedha la kimataifa.

    Katika mwaka 1982, serikali kuu na baraza la serikali la China ziliamua kutenga fedha za Yuan za renminbi milioni 200 kwa miaka 10 mfululizo ili kuanzisha mradi muhimu wa kikanda wa kusaidia kuondoa umaskini katika sehemu hizo masikini kabisa nchini China, yaani kusaidia kanda ya ukame ya Gansu ya kati, sehemu ya Xihaigu ya Ningxia na njia ya sehemu iliyoko kando ya magharibi ya Mto Manjano (kwa ufupi ni "sehemu za magharibi tatu"). Katika mwaka 1993, baraza la serikali liliamua ongeza muda wa ujenzi wa "kanda za magharibi tatu" kwa miaka kumi zaidi ili kutimiza lengo la "kutatua halisi tatizo la upungufu wa chakula na nguo kwa wakulima na kuongeza mapato yao".

 

    Baada ya kutekeleza utoaji msaada katika kuondoa umaskini wa "sehemu za magharibi tatu", hasa kutokana na kusukuma mbele uendelezaji wa uchumi kwa sehemu za magharibi miaka ya karibuni, fedha nyingi zimetumika katika ujenzi wa miundo mbinu ya sehemu hizo kama vile ujenzi wa barabara.

    Kwa mfano, hadi mwishoni mwa mwaka 2003, urefu wa barabara inayotumika katika mji wa Dingxi ilikuwa na zaidi ya kilomita 2273, na vijiji zaidi ya 2,000 vimekuwa na barabara za kupitisha matrekta au malori ya kilimo; mabasi yanafika asilimia 98.5 ya wilaya, na mabasi yanafika asilimia 78.7 ya vijiji.

    Hivi sasa mradi mpya wa barabara ya kasi unaendelea kujengwa. Bw. Jingqiao anayeishi katika tarafa ya Xiangquan mjini Dingxi alisema kwa furaha kuwa, "zamani tukitaka kwenda mji wa Lanzhou ilitulibidi tupande mlima mkubwa, na ilituchukua saa 12. Hivi sasa kuna barabara ya kasi, hivyo inatuchukua saa moja tu, na viazi vyetu vinaweza kusafirishwa mjini kwa wakati na kuuzwa kwa bei nzuri."

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-22