Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-27 21:35:29    
Jumuiya ya kimataifa yazisaidia sehemu zilizokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi

cri
    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan jana alitoa taarifa kupitia msemaji wake akisema kuwa, amehuzunishwa sana na vifo vya watu wengi na hasara kubwa ya mali iliyosababishwa na tetemeko la ardhi na dhoruba lililosababishwa kutokana na tetemeko hilo, na kuelezea huruma kubwa kwa serikali na watu waliokumbwa na maafa. Rais Hu Jintao wa China jana aliwatumia salamu marais wa nchi zilizokumbwa na maafa. Kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake amewapa pole za dhati wananchi wa nchi hizo waliokumbwa na maafa, na kutoa rambirambi kwa watu walikufa katika maafa hayo. Malkia wa Uingereza Bibi Elizabeth II, Rais Jaques Chiraq wa Ufaransa, Rais Putin wa Russia na Malkia wa Uholanzi Bibi Beatrice pia wameeleza huruma zao kwa nchi zilizokumbwa na maafa.

    Wakati huo huo, jumuiya ya kimataifa imeanzisha kwa haraka kampeni ya kutoa misaada. Hivi sasa Umoja wa Mataifa umepeleka kikundi cha kutathimini maafa na uratibu wa kuokoa maafa kwa sehemu zilizokumbwa na maafa. Ofisi ya uratibu ya mambo ya mambo kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, watumishi wa Umoja wa Mataifa wameanza kutoa fedha za misaada ya dharura kwa watu wa Sri Lanka waliokumbwa na maafa.

    Chama cha msalaba mwekundu kilichoko Geneva pia kimetenga dola za kimarekani laki 8.7 kwa ajili ya nchi zilizokumbwa na maafa.

    China ikiwa jirani ya nchi zilizokumbwa na maafa inafuatilia sana hali ya sehemu zilizokumbwa na maafa. Wizara ya biashara ya China jana usiku ilitangaza kuwa, serikali ya China imeamua kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu kwa India, Indonesia, Sri Lanka, Maldives na Thailand. Hivi sasa wizara ya biashara ya China imeanzisha utaratibu wa kukabiliana na maafa ya dharura ili kutoa misaada ya dharura kwa wakati kwa nchi zilizokumbwa na maafa. Nchi ya Japan yenye uzoefu mkubwa wa kupambana na tetemeko la ardhi na dhoruba lililosababishwa nalo imepeleka kikosi cha matibabu kilichoundwa na watu 20 nchini Sri Lanka kutokana na ombi la nchi hiyo. Zaidi ya hayo, Japan itapeleka vikosi vya utoaji misaada kwa Indonesia, Thailand na Sri Lanka, na kutoa vifaa vya misaada ya dharura kwa nchi hizo. Kikundi cha matibabu cha Israel pia kimefika nchini Sri Lanka. Serikali ya Kuwait jana iliahidi kuwa itatoa misaada ya fedha kwa nchi zilizokumbwa na maafa.

    Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya na nchi kadhaa za Ulaya pia zimeamua kutoa misaada ya dharura kwa nchi zilizokumbwa na maafa. Umoja wa Ulaya unafanya mawasiliano na wenzi wao wa ushirikiano ili kuhakikisha misaada ya Umoja wa Ulaya iweze kufika kwa wakati sehemu zilizokumbwa na maafa. Zaidi ya hayo, nchi nyingi za Ulaya kama vile Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Ufaransa, Uingereza, Sweden, Austria na Ugiriki zimetoa misaada kwa nchi zilizokumbwa na maafa. Jana, idara husika ya Russia ilitangaza kuwa, Russia itapeleka ndege mbili za uchukuzi kupeleka vifaa vya dharura kwa nchi zilizokumbwa na maafa, na watoaji misaada wa Russia pia watafika huko sehemu zilizokumbwa na maafa.

    Jambo muhimu zaidi ni kuzuia maambukizi ya maradhi kutokana na maafa. Wataalamu Wanabainisha kuwa, hivi sasa sehemu zilizokumbwa na maafa zina ukosefu wa maji safi ya kunywa, zana za bafuni, chakula na makazi ya rahisi. Shirikisho la Chama cha msalaba mwekundu na chama cha hilari nyekundu limeamua kupeleka vifaa vya matibabu vitakavyotosheleza mahitaji ya watu laki moja kwa nchi ya Sri Lanka. Shirikisho hilo pia limeanzisha kikundi cha kukabiliana na hali ya dharura ili kufanya kazi wakati wa kutokea hali ya dharura katika sehemu zilizokumbwa na maafa.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-27