Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-28 11:20:54    
Tangazo

cri
    Mwaka mpya 2005 utawadia hivi karibuni. Tukiwa tunaagana na mwaka 2004, tunapenda kuwashukuru kwa uungaji mkono wenu kwa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa. Kutokana na uungaji mkono wenu, tumetiwa moyo na kuchapa kazi zaidi kwa kuvifanya vizuri zaidi vipindi mbalimbali vya Idhaa ya Kiswahili ya CRI, na kuwahudumia wasikilizaji wetu ili wafurahie zaidi matangazo yetu kwenye masafa mafupi na vipindi vyetu vya aina mbalimbali vilivyoko kwenye tovuti ya Kiswahili kwenye mtandao wa internet. Lakini bado tunatakiwa kuongeza juhudi katika kazi zetu, ili tuweze kuboresha zaidi matangazo yetu.

    Katika mwaka 2005, tutaendelea na kazi kama kawaida. Pia tunapenda kuwaarifu kuwa, mwaka kesho tutachapisha gazeti dogo la "Daraja la Urafiki", ambalo litakuwa na mkusanyiko wa barua, makala na mashairi tutakayoyapokea kutoka kwa wasikilizaji wetu, na tutamtumia kila msikilizaji tutakayeendelea kuwasiliana naye, ni matumaini yetu kuwa gazeti hilo dogo litaimarisha zaidi mawasiliano na urafiki kati ya Radio China kimataifa na wasikilizaji wake, na kuongeza mawasiliano kati ya wasikilizaji wetu wa sehemu mbalimbali.

    Karibu mtuletee barua, makala, mashairi mafupi, hadithi, hata maoni na mapendekezo yako ili tuweze kuandaa na kuchapisha vizuri zaidi gazeti hilo kutokana na mapendekezo yenu. Mkipata nafasi, msisite kutembelea na kusikiliza vipindi vyetu kwenye tovuti yetu katika mtandao wa internet, anuani yake ni www.cri.cn, chagua Kiswahili, utavutiwa mara moja.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-28