Tetemeko la ardhi na dhoruba lililosababishwa na tetemeko hilo kwenye eneo la bahari la Sumatra, Indonesia limeathiri nchi kadha wa kadha za Kusini mashariki ya Asia na kusini ya Asia, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 24. Baada ya kutokea kwa maafa hayo, kazi ya kuokoa maafa ilianza kwa pande zote. Wataalamu wanaona kuwa, maafa hayo makubwa yameleta uharibifu mkubwa sana kwa sehemu zinazokumbwa na maafa, kazi ya kuokoa maafa inakabiliwa na changamoto kubwa.
Kwanza, mazingira ya afya ya sehemu zilizokumbwa na maafa yamezidi kuwa mabaya. Nchi za India na Sri Lanka zenye idadi kubwa ya watu, miili ya watu wengi waliokufa kutokana na maafa hayo bado haijashughulikiwa, lakini halijoto ya nchi hizo mbili kwa sasa ni zaidi nyuzi 30 juu ya sentigredi, hivyo miili mingi imeanza kuharibika. Jumuiya moja ya utoaji misaada imeripoti kuwa, katika sehemu ya kusini mwa India, miili iliyoharibika imechafua mfumo wa utoaji maji wa huko, hasa katika sehemu za wakazi maskini, watu wengi hawana la kufanya ila tu kutumia maji yaliyochafuliwa, kama katika siku kadhaa zijazo mfumo wa afya na kukinga maradhi hautaweza kuanzishwa, basi huenda maradhi yakuambukiza yataanza kuenea. Ofisa wa Umoja wa Mataifa pia ameonya kuwa, lazima kuchukua tahadhari kuhusu uwezekano wa kuibuka kwa maradhi ya maambukizi. Ofisa mwandamizi wa kamati ya chama cha msalaba mwekundu amesema kuwa, hivi sasa changamoto kubwa inazikabili sehemu zilizokumbwa na maafa ni maji machafu kuambukiza maradhi, hasa maradhi ya malaria, kuhara na maradhi ya mfumo wa hewa. Ili kuepusha mazingira ya afya yasizidi kuwa mabaya, maji safi ya kunywa na chakula, makazi ya usalama na zana za bafuni zote zinahitajika kwa dharura, lakini nchi kadhaa za Asia ya kusini kama Sri Lanka siku zote zina ukosefu wa vitu hivyo.
Aidha, katika hali ambayo barabara, majengo ya utoaji umeme na mawasiliano ya habari yameharabiwa vibaya, namna ya kupeleka haraka vifaa vya misaada kwa watu wengi wanaokumbwa na maafa ni changamoto inayoikabili kazi ya kuokoa maafa. Maafa hayo yameathiri vibaya nchi nyingi za Asia ya kusini na Asia ya kusini mashariki, ambapo takriban Sri Lanka nzima imekumbwa na maafa, na sehemu nyingi za India pia zimeathiriwa vibaya. Katika hali hiyo ngumu kupeleka vifaa vya misaada kunahitaji siku kadhaa hata wiki kadhaa; kama chakula na madawa hayataweza kupelekwa kwa haraka na kwa wakati, watu wengi watakabiliwa na tishio la vifo. Wataalamu wanaona kuwa, hata kama wakiwepo watoaji misaada wenye uwezo mkubwa na vifaa vya kutosha vya misaada wakishirikiana na serikali za nchi zinazokumbwa na maafa na jumuiya zinazohusika, wakitaka kupeleka kwa haraka vifaa vya misaada, pia ni kazi ngumu sana.
Aidha, kazi ya kuokoa maafa pia inakabiliwa na changamoto ya kukumbwa na tetemeko la ardhi linaloweza kutokea wakati wowote. Wataalamu wa Idara ya hali ya hewa ya India jana walisema kuwa, kuanzia usiku wa tarehe 26 hadi asubuhi ya tarehe 27, matetemeko ya ardhi yalitokea tena mara 15 hadi 20 kwenye sehemu ya bahari ya Sumatra, Indonesia hadi sehemu ya bahari ya visiwa vya Andaman na Nicobar vya India. Wataalamu wa India wametabiri kuwa, katika siku kadhaa zijazo, tetemeko kubwa kiasi la ardhi huenda litatokea tena kwenye sehemu ya bahari ya mashariki ya India, sehemu za pwani za India huenda zitashambuliwa tena na dhoruba litakalosababishwa na tetemeko la ardhi. Wataalamu wamewashauri wakazi wa pwani wakae macho na kuondoka kwa haraka sehemu zenye hatari.
Ingawa kazi ya kuokoa maafa inakabiliwa na taabu mbalimbali, lakini nchi zinazokumbwa na maafa na jumuiya ya kimataifa zimejitahidi kuchukua hatua kwa kuokoa maafa, tuna imani kuwa chini ya juhudi za pamoja za nchi mbalimbali, binadamu watashinda maafa hayo ya kimaumbile.
Idhaa ya kiswahili 2004-12-28
|