Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-29 16:50:29    
Kababu

cri

Mahitaji

Nyama ya kamba-mwakaje gramu 150, nyama ya kidari cha kuku gramu 100, chengachenga za mkate mweupe uliotolewa magamba gramu 75, kiasi kidogo cha mvinyo wa kupikia, chumvi iliyo safi, unga wa pilipili manga, M.S.G, vipande vya vitunguu maji na tangawizi na mayai yaliyopigwapigwa.

Njia

1. baada ya kuondoa magamba, ngozi na kano, ponda nyama ya kuku na ya kamba kwa mgongo wa kisu mpaka iwe laini, halafu ichanganye pamoja na mvinyo wa kupikia, chumvi, unga wa pilipili manga, M.S.G, vipande vya vitunguu maji na tangawizi na mayai yaliyopigwapigwa na kabla ya kuvikorogakoroga usisahau kutia kidogo mafuta.

2. sukuma nyenzo hizo zilizokwisha korogwa ziwe bonge moja kubwa, kisha liweke kwa nguvu ndani ya dishi ili nyenzo hizo zishikamane.

3. kutokana na bonge hilo tengeneza kababu zenye kipenyo cha sm.2.5 hivi kwa kuzifinyafinya, halafu viringisha kababu moja moja juu ya chenga chenga za mkate.

4. tia kababu zilizoambatana na chengachenga za mkate katika mafuta ya uvuguvugu na zikaange kwa dakika 5 kwa kutumia moto mdogo. Kababu zinapopanuka, endelea kuzikaanga kwa moto mkali. Mpaka rangi ya kababu inapokuwa ya hudhurungi, zipakue na kuzitia kwenye sahani.

Kitoweo hiki ni kitamu na rangi na ladha yake ni nzuri.