Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-29 18:52:25    
"Njia ya hariri" ya karne ya 21 inaanzia China

cri

    Mazingira ya njia ya hariri ya zamani ni ngamia, vilima vya mchanga na msafara wa wafanya-biashara, lakini kiini cha "njia ya hariri"ya karne ya 21 ni kufanya utafiti juu ya seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri wanaofugwa kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kimaendeleo.

    Utafiti wa seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri unahusiana na kuweza kuchukua nafasi ya kuongoza au la kwa China katika ushindani wa kimataifa kuhusu hakimiliki ya elimu ya gene, na kuhusiana na mahali pa kuanzia kwa "njia ya hariri"ya karne ya 21, ni kuanzia China au nchi nyingine. Watafiti wa syansi wa China ingawa wanakabiliwa na shida za aina nyingi zikiwemo za upungufu wa mtaji na teknolojia ya kimaendeleo, walimaliza utafiti kuhusu "ramani ya muundo"ya seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri mwaka uliopita, tarehe 10 mwezi Deseamba mwaka huu wametangaza kuwa China imepata mafanikio mapya muhimu katika utafiti na matumizi ya gene za wadudu wa nyuzi za hariri wanaofugwa na binadamu, hatua ambayo imethabitisha tena hadhi ya kuongoza kwa China katika utafiti wa seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri. Wanasayansi wa China wanaweza kusema kuwa "njia ya hariri"ya karne ya 21 inaanz1a China, kiwango cha sayansi na teknolojia cha sekta ya jadi ya uzalishaji wa nyuzi za hariri ya China kitainuka sana, na mabadiliko makubwa ya kimapinduzi yatatokea katika sekta ya uzalishaji wa nyuzi za hariri.

    Maendeleo ya teknolojia ya sekta ya uzalishaji wa nyuzi za hariri duniani, hususan maendeleo makubwa na wingi wa uzalishaji na ubora wa nyuzi za hariri yalitokana na kuenezwa kwa wadudu wa chotara wa nyuzi za hariri katika miaka ya 40 na kuboreshwa kwa mara tatu kwa watutu wa nyuzi za hariri katika miaka ya 80 ya karne ya 20. Katika muda wa miaka 20 hapo baadaye, ingawa watafiti wa sekta ya wadudu wa nyuzi za hariri wa nchi mbalimbali walijitahidi kila wawezacho, lakini maendeleo ya utafiti wa teknolojia ya kuzalisha wadudu bora wa nyuzi za hariri na teknolojia husika yalishindikana. Hivyo nchi inayotangulia kupiga hatua ya kimapinduzi katika utafiti wa seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri, itaweza kukwa mua na kuchangamsha upya maendeleo ya teknolojia ya sekta ya nyuzi za hariri, itakuwa nchi kubwa ya sayansi na teknolojia ya sekta ya nyuzi za hariri na kuanzisha njia mpya ya hariri.

    Kiongozi wa mpango wa mradi wa utafiti wa seti za gene za wadudu wa nyuzi za hariri ambaye ni mtafiti wa Taasisi ya Uhandisi ya China Bw. Xiang Zhonghuai alisema kuwa kukamilshwa kwa uchoraji wa "ramani ya muundo"ya wadudu wa nyuzi za hariri na utafiti wa gene zenye uwezo za seti za gene za watutu wa nyuzi za hariri, itafikisha China katika kilele cha maendeleo ya sekta ya uzalishaji wa nyuzi za hariri na kuipatia China nafasi kubwa ya kusafirisha nyuzi za hariri kwa nchi za nje. Hivi sasa nchini China kuna koo kiasi cha milioni 20 za wakulima, ambazo zinafuga wadudu wa nyuzi za hariri, wakati thamani ya sekta ya uzalishaji wa nyuzi na vitambaa vya hariri imefikia Yuan bilioni 70.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-29