Kutokana na takwimu, watalii waliokufa na kupotea wengi walikuwa nchini Thailand, Maldives na Sri Lanka hasa Thailand. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Thailand jana ilitangaza kuwa mawimbi hayo makubwa yameua watu 1800, na kati yao 473 ni watalii kutoka nchi za nje, hadi sasa hawajafahamika uraia na hadhi zao.
Kutokana na takwimu, watalii waliokufa na kupotea wengi wanatoka nchi 30 za Marekani, Uingereza, Australia, Ujerumani, Uswisi, Denmark, Norway, New Zealand na Canada, na kati yao wengi waliokufa wanatoka Uswisi, Norway, na Ujerumani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi jana ilibaini kuwa hivi sasa watalii wa Uswis 1500 wamepotea nchini Thailand, waziri mkuu wa Uswis alitangaza kuwa Januari mosi ni siku ya maombolezo ya taifa, na bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kuomboleza.
Chansela wa Ujerumani jana pia alitangaza kuwa hivi sasa Wajerumani wasiopungua 26 wamekufa na wengine zaidi ya 1000 wamepotea. Isitoshe, watalii wa Norway kiasi cha 800 hawajulikani walipo nchini Thailand. Watalii wa New Zealand zaidi ya 300 walipotea nchini Thailand. Kadhalika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ilitangaza kuwa Wafaransa 20 walikufa na wengine 90 walipotea.
Kwa sababu mawimbi makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi yalitokea katika siku ya Krismasi, watalii wengi walikuwa kwenye likizo katika nchi za Asia ya Kusini Mashariki na ya Kusini ambapo hali ya hewa ni nzuri. Kutokana na mandhari nzuri, huduma bora na hali ya hewa, kila mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka mpya watalii wa nchi za Magharibi humimika sana nchi za sehemu hizo hasa Thailand na Maldives. Siku ilipotokea tetemeko la ardhi na mawimbi makubwa hali ya hewa ilikuwa nzuri, watalii wengi waliochukuliwa na mawimbi walikuwa wakiota jua kwenye ufukwe au kucheza michezo baharini kama ya kupiga mbizi.
Tarehe 26 baada ya tetemeko la ardhi na mawimbi makubwa kutokea serikali na raia wa nchi nyingi walishikwa na wasiwasi. Ofisi za ubalozi zaidi ya 20 nchini Thailand zilituma maofisa kwenda sehemu ya kusini ya kivutio ya Thailand kwa ndege iliyoandaliwa na wizara ya mambo ya nje ya Thailand kuwasaidia watalii wa nchi zao kurudi nyumbani. Na nchi nyingi za Magharibi zimewatahadharisha raia kwamba wasimamishe utalii wao katika sehemu zilizoathirika vibaya na maafa.
Baadhi ya nchi za Magharibi zinaona kuwa waliopotea hawana tumaini lolote la kuwa hai, kwa hiyo, idadi ya waliokufa hakika itaongezeka.
Idhaa ya kiswahili 2004-12-30
|