Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-30 16:20:41    
Kwa nini Russia na Ulaya, Marekani zilitoa maoni tofauti kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Ukraine

cri
    Matokeo yenyewe yanaonesha kuwa, mgombea wa chama cha upinzani Bw. Viktor Yushchenko amemshinda waziri mkuu Bw. Viktor Yanukovisch kwa asilimia 7.8. Kuanzia tarehe 27, viongozi wa Poland, Marekani, Ujerumani, Latvia na Georgia kwa nyakati tofauti walimtumia Bw. Yushchenko pongezi kwa simu, na kueleza kuwa wanakubali matokeo hayo ya uchaguzi. Umoja wa Ulaya na shirika la NATO yalipokaribisha matokeo hayo yalieleza pia kuwa yataendelea kuimarisha uhusiano kati yao na Ukraine, na yataharakisha mchakato wa kuiingiza Ukraine Umoja wa Ulaya na iwe mwanachama mpya wa shirika la NATO. Lakini kwa upande mwingine, wachunguzi wa nchi za Umoja wa Jamhuri Huru waliona kuwa, uchaguzi huo ulikiuka taratibu katika sehemu nyingi, kama vile ulipuuza haki za walemavu na wazee. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bw. Aleksandr Yakovenko tarehe 29 alisema kuwa, wachunguzi wa Umoja wa Ulaya walitumia vigezo tofauti katika uchaguzi mkuu wa Ukraine, na kuufumbia macho ukiukaji wa taratibu uchaguzi huo.

    Wachimbuzi wa kimataifa waliona kuwa, maoni tofauti ya Russia na Ulaya, Marekani kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Ukraine yanatokana na maslahi yao yenyewe. Ni dhahiri kamba, serikali za Russia na nchi nyingi za Umoja wa Jamhuri Huru zinamwunga mkono kisiasa Bw.Yanukovisch ambaye anaipendelea Russia na kushikilia msimano wa umoja kwa nchi za Umoja wa Jamhuri Huru; na nchi za Ulaya na Marekani zinamwunga mkono kithabiti Bw. Yushchenko ambaye anapenda zaidi nchi za Magharibi. Mgombea yeyote kati yao akishika madaraka, ataathiri sana maslahi ya watu wanaomwunga mkono mgombea mwingine katika mambo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.

    Vyombo vya habari vimeona kuwa, serikali na wachunguzi wa Russia na nchi nyingi za Umoja wa Jamhuri Huru hawakumlaumu moja kwa moja mgombea wa chama cha upinzani Bw. Yushchenko, bali walikosoa ukiukaji wa taratibu katika uchaguzi huo. Mwenyekiti wa tume ya shirikisho la Russia Bw. Sergei Mironov alieleza hadharani kuwa, Russia inapenda kushirikiana na rais yeyote anayechaguliwa na watu wa Ukraine. Kwa hivyo, makosa yaliyotolewa na Russia kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu huo hayataathiri Russia kupokea matokeo rasmi ya uchaguzi wa Ukraine.

    Aidha vyombo vya habari vimeona kuwa, wakati tume ya uchaguzi mkuu wa Ukraine ilipotangaza matokeo ya hatua ya kwanza ya upigaji kura, haijatangaza mgombea nani ameshinda kwa rasmi, wala haijaamua vipi matokeo ya rasmi yanatangazwe, na hata rais Kuchima wa hivi sasa hajatoa maoni kuhusu upigaji kura upya wa duru la pili na matokeo yake. Bw. Yushchenko akiwa mgombea wa urais anayetangazwa kupata kura nyingi zaidi tarehe 28 aliitaka serikali ya hivi sasa ijiuzulu, na pia alitoa mwito akiwataka watu wanaomwunga mkono kulizingira jengo la serikali. Waziri mkuu Yanukovisch tarehe 29 alisisitiza tena kuwa, hataondoka madarakani, na alipeleka malalamiko kwenye shitaka kwenye tume ya uchaguzi mkuu wa Ukraine, akiitaka tume hiyo kubatailisha matokeo ya upigaji kura huo. Kwa hivyo, hali iliyopo hivi sasa nchini ukraine bado ina utatanishi.

    Vyombo vya habari vimeona kuwa, kutokana na hali ya utatanishi nchini Ukraine, misimamo ya kidiplomasia ya Russia na Ulaya, Marekani hivi karibuni inahitilafiana, na pande hizo mbili zitazidisha nguvu kuishawishi serikali mpya katika siku za usoni. Wakati huo, athari kutoka nje itaathiri migongano ya kisiasa nchini Ukraine. Kutokana na hali iliyopo hivi sasa, nguvu mbalimbali nje ya Ukraine zitaendelea kupambana kwa lengo la kujipatia maslahi makubwa zaidi nchini humo.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-30