Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-30 18:42:46    
Wanyama na mimea nchini China

cri

   

    Ili kulinda maliasili ya wanyama na mimea adimu, China imeanzisha hifadhi 1146 za misitu na wanyama pori zenye eneo la hekta milioni 88.13. Hifadhi 15 za kimaumbile zikiwemo hifadhi za Wolong na Jiuzhaigou mkoani Sichuan, Mlima Changbai mkoani Jilin, Mlima Dinghu mkoani Guangdong, Mlima Fanjing na hifadhi ya Maolan mkoani Guizhou, Mlima Wuyi mkoani Fujian, Hifadhi ya Shennongjia mkoani Hubei, mbuga za Xilinguole mkoani Mongolia ya Ndani, kilele cha Bogeda mkoani Xinjiang, hifadhi ya Yancheng mkoani Jiangsu, hifadhi ya Xishuangbanna mkoani Yunnan, Mlima Tianmu na Visiwa vya Nanji mkoani Zhejiang, hifadhi ya Fenglin mkoani Heilongjiang zimewekwa kwenye mfumo wa kimataifa wa hifadhi ya maumbile. Na hifadhi ya Zhalong mkoani Heilongjiang, hifadhi ya Xianghai mkoani Jilin, Ziwa la Dongting ya Mashariki mkoani Hunan, Ziwa la Boyang mkoani Jiangxi, Kisiwa cha ndege mkoani Qinghai, Bandari ya Dongzhai mkoani Hainan na hifadhi ya Mipu huko Hongkong zimewekwa kwenye orodha ya sehemu za ardhi oevu muhimu duniani.

    China ni moja ya nchi zenye aina nyingi zaidi za wanyama pori duniani, ambayo ina aina 4400 za wanyama wenye uti wa mgongo. Idadi hiyo inachukua zaidi ya asilimia 10 duniani. Na miongoni mwa aina hizo, kuna aina 500 za wanyama na aina 1189 za ndege. Wanyama adimu wakiwemo Panda, kima wenye manyoya ya rangi ya dhahabu, tiger wa kusini ya China, kwale wa rangi ya kahawia, korongo wenye ngeu kichwani, pomboo wenye mapezi meupe na mamba wa Mto Yangtse wanajulikana duniani. Panda ambao ni wanyama wanene na watulivu wanapendwa na watu wengi. Korongo wenye ngeu kichwani ni ndege wenye urefu wa mita 1.2 na manyoya meupe. Kichwa chao chenye ngeu kinafanana na moto unaong'ara. Pomboo wenye mapezi meupe ni aina moja ya nyangumi waishio ndani ya maji baridi ambao wako wa aina mbili tu duniani. Pomboo mmoja wa aina hiyo aliyekamatwa katika Mto Changjiang mwaka 1980 alivutia macho ya wanasayansi wengi duniani.

  

    China pia ni nchi yenye maliasili nyingi za mimea. Ina aina elfu 32 za mimea ya ngazi ya juu. Mimea mingi inayoota katika kanda ya baridi, ya fufutende na ya joto ya kizio cha kaskazini inaweza kuonekana nchini China. Kuna aina 7000 za miti, ambazo aina nyingi zinapatikana China tu. China ina aina zaidi elfu 2 za mimea ya chakula na elfu 3 za mimea ya dawa.

Idhaa ya Kiswahili 2004-12-30