Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-12-31 16:05:24    
Mwanamke wa Kenya aliyepata tuzo ya amani ya Nobel azungumzia maendeleo endelevu

cri

    Mwanamke aliyepata tuzo la amani la Nobel la mwaka 2004 Bi. Wangari Maathai jana katika sherehe ya kumkaribisha iliyofanyika Nairobi alisema kuwa, usimamizi mzuri wa maliasili, demokrasia na amani ni nguzo tatu za maendeleo endelevu.Bi. Maathai alishiriki kwenye sherehe ya kukabidhiwa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 2004 iliyofanyika huko Oslo, Norway tarehe 10, Desemba. Baada ya kutembelea Ujerumani, Uingereza na Marekani alirudi nchini Nairobi siku hiyo.

    Bi. Maathai katika sherehe alisema, usimamizi mzuri wa maliasili unamaanisha kuwa kugawanya maliasili kwa usawa ili kuzingatia maslahi ya watu waliowengi na kuondoa tofauti kati ya watu maskini na tajiri. Kwa njia hiyo, ndio binadamu wanaweza kupata amani na maendeleo; kama hakuna demokrasia, basi maliasili haziwezi kugawanywa kwa uswa. Alisema kuwa, "Amani ni msingi wa maendeleo. Nguzo hizo tatu ni kama miguu mitatu ya stuli ambayo haiwezi kukosekana hata mguu mmoja."

    Bi. Maathai ana umri wa miaka 64. Mwaka 2003 alikuwa naibu waziri wa mazingira na maliasili wa Kenya, na ni mmoja wa mawaziri wanawake 6 ya wa serikali ya Kenya. Mwaka 1997 alianzisha "harakati za kanda ya kijani", na kuwahamasisha wanawake wa Afrika kupanda miti karibu milioni 30 katika miaka karibu 30. Kampeni hiyo sio tu inalinda mazingira, bali pia inawapatia watu mamia ya maelfu ya watu ajira. Mnamo tarehe 8, Oktoba, mwaka huu, kamati ya Nobel ya Norway ilitangaza kuwa, itakabidhi tuzo ya amani la Nobel la mwaka 2004 kwa Bi. Maathai ili kumsifu kwa mchango wake aliotoa katika "maendeleo endelevu, demokrasia na amani". Hivyo Bi. Maathai amekuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika kupata tuzo ya amani la Nobel.

Idhaa ya kiswahili 2004-12-31