Mwaka 2005 idadi ya wanafunzi watakaohitimu kutoka vyuo vikuu itafikia milioni 3, na idadi hiyo ni kubwa sana tangu China kufanya mageuzi ya elimu mwaka 1999, hivyo hali ya wanafunzi watakaohitimu kupata ajira si nzuri kama zamani. Habari kutoka wizara ya elimu ya China inasema kuwa, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi inaweka rikodi katika historia. Kutokana na hali hiyo, mawazo ya wanafunzi kujipatia ajira imebadilika.
Zamani sababu ya kwanza ya wanafunzi wa vyuo vikuu kupata ajira ilikuwa " mshahara na nafasi ya kuandaliwa". Lakini sasa wanafunzi wanazingatia zaidi siku za usoni kwa wenyewe, na kiwango cha kukadiri hali hii ni nguvu na utamaduni wa kampuni. Uchunguzi unaonesha kuwa, hivi sasa mataka ya wanafunzi wa vyuo vikuu wamepungua kiwango cha mshahara kuliko miaka miwili iliyopita. Kwa kawaida, mshahara wa kila mwezi kwa mwanafunzi aliyehitimu kutoka chuo kikuu ni Yuan 1500-3000, lakini wanafunzi wa 75% wanachagua mshahara wa chini ya Yuan 2000 kwa mwezi. Mbali na hayo, wanafunzi wengi walipochagua ajira, hawakulinganisha na masomo yao ya chuo kikuu, kama ajira hiyo ilikuwa nzuri wanafunzi wakaichagua. Hii inaonesha kuwa, wanafunzi wa vyuo vikuu hawataki kuzuiliwa katika masomo yao. Kwa wanafunzi wale ambao hawakupenda masomo yao, kuhitimu kutoka vyuo vikuu ni nafasi mpya ya kuchagua maisha.
Kuhusu ukubwa wa makampuni, wanafunzi walikuwa na mawazo tofauti. Kwa mfano, katika chuo kikuu cha viwanda cha Hefei, mkoani Anhui, mwaka 2004 31% ya wanafunzi waliohitimu walichagua makampuni yenye watu chini ya mia 5, 19% walisaini mkataba na makampuni yenye watu 500-1000, na 25% walichagua makampuni yenye watu 1000-3000. fikra ya zamani yaani " kampuni kubwa ni kampuni nzuri" imebadilika. Kwa kuwa makampuni madogo yana utaratimu wa uendeshaji wenye unyumbufu, na uwezo wa kila mmoja unaweza kuoneshwa, hivyo makampuni madogo yanakaribishwa zaidi kwa wanafunzi siku hadi siku.
Takwmi ya uchunguzi inaonesha kuwa, hivi sasa ajira zinazokaribishwa na wanafunzi waliohitimu kutoka vyuo vikuu ni kwamba, kampyuta, huduma ya habari, uchumi na mawasiliano. Makampuni hadari ya IT kama LENOVO China, Shenzhou China, Datang China, IBM Marekani, Microsoftware Marekani, HP Marekani yanakaribishwa sana na wanafunzi, na bila shaka ushindani kati ya wanafunzi waliotaka kupata ajira katika makampuni hayo ni vikali.
Habari nyingine zinasema kuwa, tangu China ijiunge na WTO, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na nchi nyingie yanaongezeka siku hadi siku, hivyo watu wenye uwezo wa lugha za kigeni wanahitajika sana. Hasa wanafunzi wao wanaosoma lugha ndogo, kwa mfano lugha za Arabia, Korea, Thailand, Italia, Hispania n.k wameagizwa na makampuni ya biashara.
Profesa wa chuo kikuu cha lugha ya kigeni cha Shanhai Bw. Li Shaozhu alisema kuwa, kutokana na mahitaji ya jamii, chuo hicho kitaweka masomo mapya ya lugha za kigeni nayo ni lugha za Persia, Indonesia.
Idhaa ya kiswahili 2005-01-04
|