Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-05 20:38:10    
Mwanafunzi mmoja wa China anayetoka kwenye familia masikini kufaulu kusoma katika chuo kikuu

cri

Mwanafunzi Xiang Xiufeng mwenye umri wa miaka 17, anatoka wilaya ya Badong wa mkoa wa Hubei, katikati ya China. Sehemu hiyo inazungukwa na milima, hivyo uchumi wake bado uko nyuma. Baba yake ni mwalimu wa shule ya msingi, mshahara wake wa kila mwezi ni Yuan mia 8, mama yake anafanya shughuli za kilimo. Ingawa mapato ya familia yake si kidogo katika sehemu hiyo, lakini kutokana na kuwa afya ya wazazi wake si mzuri, wanahitaji kununua dawa na kuwapeleka hospitali; mbali na hayo, dada wawili wa Xiang Xiufeng wamekwenda chuo kikuu, ili kuwawezesha kusoma, wazazi walikopa pesa kutoka kwa watu wengine.

Mwaka huu Xiang Xiufeng alipata nafasi ya kusoma katika Chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai kwa matokeo mazuri ya mitihani. Baada ya kupata taarifa hiyo, familia yake ilifurahi sana, lakini baadaye walikuwa na wasiwasi. Kwa sababu mwanafunzi wa chuo hicho anapaswa kulipa ada ya masomo ya yuan elfu 7 kwa mwaka. Mbali na hayo, gharama za maisha ya kila mwaka inahitaji yuan elfu nne. Hivyo Xiang Xiufeng alihitaji zaidi ya yuan elfu 10 kila mwaka. Kwa familia yake, kiasi hiki ni kikubwa sana.

Wakati wazazi wake walipokuwa na wasiwasi, chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai kiliwaambia kuwa, ili kuwasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia masikini, chuo hicho kilianzisha " njia maalum" kwa wanafunzi hawa, yaani kwamba, baada ya kujiandikisha katika chuo kikuu, wanafunzi wanajaza fomu kuhusu hali zao halisi, baadaye wanaweza kusoma bila kulipa ada. Kuhusu ada zao za masomo, chuo kikuu kitafanya juhudi pamoja na wanafunzi ili kuzitatua. Baada ya kupata taarifa hiyo, familia yake ilitulia, na Xiang Xiufeng alikwenda Shanghai kusoma.

Rafiki wa Xiang Xiufeng ambaye anasoma mwaka wa tatu katika Chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai, alimwambia asiwe na wasiwasi kuhusu ada za masomo. Anasema:

" chuo kikuu kinawasaidia wanafunzi wanaotoka kwenye familia za masikini kuomba mkopo kutoka benki; mbali na hayo, chuo kikuu kitaondoa baadhi ya ada kwa wanafunzi hao."

Xiang Xiufeng anasema:

" sitaki kupeleka matatizo kwa watu wengine. Nataka nifanikiwe kuomba mkopo wa benki, na baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, nitalipa pesa hizo kwa jitihada zangu mwenyewe."wanaotoka kwenye familia masikini ni mkopo maalumu ulioanzishwa na serikali ya China, riba ya mkopo huo ni ya chini sana kuliko riba ya mikopo ya kawaida. Kila mwanafunzi anaweza kuomba mkopo wa yuan elfu 6 kila mwaka, baada ya mwaka mmoja au miaka miwili tangu wanafuzi walipohitimu kutoka chuo kikuu, wanapaswa kulipa mkopo ndani ya miaka 6.

Mwalimu wa chuo kikuu cha mawasiliano cha Shanghai Bw. Wei Tianhua alijulisha kuwa

" kutokana na hali ya chuo chetu, baada ya kufanya uchunguzi, tulifikiri kuondoa ada za masomo kwa wanafunzi kama Xiang Xiufeng. Mbali na hayo, ili kuwasaidia wanafunzi hawa kutatua tatizo la ghrama za maisha, chuo kikuu kinawashauri wanafunzi kuomba msaada wa maomo kwa chuo kikuu."

Mwalimu Wei alimwambia Xiang Xiufeng kuwa, kama akiwa na muda baada ya masomo, tangu kipindi cha pili cha masomo anaweza kujiunga na shughuli za mafunzo ya kazi ili kusaidia masomo. Baada ya kufanikiwa mafunzo ya kazi wanaweza kufanya kazi kadhaa, hivyo watatatua kimsingi matumizi ya maisha.

Wasikilizaji wapendwa, hivi sasa miongoni mwa wanafunzi milioni 10 wa vyuo vikuu vya China, asilimia 10 ni asilimiawanafunzi kutoka familia masikini. Serikali ya China imechukua hatua mbalimbali ili kuwawezesha wanafunzi hao kusoma katika vyuo vikuu. Naibu waziri wa elimu wa China Bw. Zhang Baoqing anasema:

" China ina uwezo kuhakikisha wanafunzi wanajiunga vyuo vikuu na kuwahakikisha kutosimamisha masomo kutokana na matatizo ya uchumi."

Idhaa ya kiswahili 2004-12-29