Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-10 20:41:23    
Pande mbili za kusini mwa Sudan zasaini makubaliano ya amani kwa pande zote

cri
    Makamu wa rais wa Sudan Osman Ali Taha na kiongozi wa jeshi la upinzani la chama cha ukombozi wa umma cha Sudan Bw John Garang tarehe 9 walisaini makubaliano ya amani huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, hii imeonesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 21 kusini mwa Sudan vimemalizika.

    Marais wa Sudan, Kenya, Tanzania, Uganda, Somalia, Djibouti na Algeria pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell, mjumbe maalum wa serikali ya China ambaye pia ni msaidizi wa waziri wa mambo ya nje Bwana Lu Guozeng na wajumbe wa nchi mbalimbali walishuhudia kwa pamoja historia hiyo.

    Makubaliano ya amani ya pande zote yaliyosainiwa jana yakiwa ni pamoja na nyongeza 8 za makubaliano ambayo yalifikiwa kati ya pande hizo mbili katika miaka miwili iliyopita. Makubaliano hayo yanaeleza kuwa, baada ya kusimamishwa rasmi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Sudan itapita muda wa mpito wa miaka 6, baada ya muda huo kumalizika, majimbo ya kusini mwa Sudan yatapiga kura za maoni ya raia kuhusu kujipatia uhuru au la. Katika muda wa mpito, pande hizo mbili pamoja zitafaidika madaraka kwa pamoja katika serikali kuu na mamlaka ya mitaa. Na asilimia 52 ya maofisa watatoka serikali ya Sudan, asilimia 28 kutoka chama cha ukombozi wa Sudan, na asilimia 20 kutoka vikundi vingine vya kisiasa nchini. Kiongozi wa chama cha ukombozi wa Sudan BW John Garang atakuwa makamu wa kwanza wa rais wa Sudan. Katika kipindi cha mpito, pande mbili pia zitagawana kwa usawa maliasili ya nchi hasa mafuta ya nchi hiyo.

    Sudan ni nchi yenye eneo kubwa kabisa barani Afrika, zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa nchi hiyo ni waumini wa dini ya kiislamu, lakini wakazi wa kusini mwa nchi hiyo wengi ni waumini wa dini za jadi za kiafrika na dini ya kikristo. Mwaka 1983, serikali kuu ya Sudan ilivunja serikali iliyojiendesha ya kusini mwa nchi hiyo, na kutekeleza sheria ya kiislam kote nchini Sudan. Hatua hiyo ilipingwa vikali na wakazi wa kusini mwa nchi hiyo, na vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka tokea hapo, na kuendeleza kwa miaka 21, na kuwa vita iliyodumu kwa muda mrefu kabisa barani Afrika.

    Kutokana na usuluhishi wa Jumuiya ya IGAD pamoja na Marekani na Jumuiya ya kimataifa, pande mbili zilizopambana za Sudan zilifanya mazungumzo ya amani nchini Kenya kuanzia mwaka 1994. Tokea nusu ya pili ya mwaka 2003, maendeleo makubwa yalipatikana katika mazungumzo ya amani ya Sudan, pande mbili zilifikia makubaliano kuhusu mpango wa usalama wa kipindi cha mpito, ugawaji wa maliasili ya mafuta na ugawaji wa mali, ugawaji wa madaraka ya serikali na hadhi kuhusu sehemu tatu za kusini ya kati zenye ugomvi. Tarehe 31 Desemba mwaka jana pande hizo mbili zilisaini tena makubaliano ya usimamishaji vita wa daima na makubaliano ya utekelezaji wa makubaliano ya amani. Mpaka hapo masuala yote ya mazungumzo ya amani ya Sudan yaliweza kutatuliwa.

    Wachambuzi wanadhihirisha kuwa, ingawa mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili yameshakamilika, lakini mchakato wa amani wa nchi hiyo nzima bado utakabiliwa na changamoto, kwani kama makubaliano hayo yaliyofikiwa na pande hizo mbili baada ya majadiliano magumu, yatatekelezwa kihalisi au la, ni jambo ambalo bado linafuatiliwa.

    Aidha, chama cha ukombozi wa umma cha Sudan bado kinaongoza vikundi vya upinzani visivyojulikana, kama vikundi hivyo vitakubali makubaliano ya amani au la, nalo pia ni jambo ambalo bado linafuatiliwa.

    Rais Omar hassan Al Bashir wa Sudan alisema tarehe 31 Desemba mwaka jana kuwa, wakati suala la Darfur la Sudan litakapotatuliwa mwishoni, ndipo Sudan nzima itakuwa na amani ya kweli.