Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-11 21:32:18    
Nchi za Afrika zajitahidi kutafuta njia ya kuondoa migogoro ya kisehemu

cri
    Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika jana liliitisha mkutano wa wakuu huko Libreville, mji mkuu wa Gabon. Hii ni mara ya kwanza kwa baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika kuitisha mkutano wa wakuu tangu kuanzishwa kwake mwaka jana. Vyombo vya habari vinaona kuwa, kuitishwa kwa mkutano huo kumeonesha kuwa, nchi za Afrika zinaimarisha siku hadi siku nia ya kuufanya Umoja wa Afrika uelekeze mambo ya kanda hiyo. Umoja wa Afrika ukiwa Jumuiya kubwa kabisa na yenye heshima kubwa kabisa kwa nchi za Afrika, hadhi yake muhimu inainuka siku hadi siku.

    Ofisa husika wa Umoja wa Afrika alifahamisha kuwa, viongozi wa nchi 13 za Afrika miongoni mwa nchi wanachama 15 pamoja na maofisa wa serikali za nchi kadhaa wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili. Mkutano huo hasa unajadili mgogoro wa Cote d'ivoire, kusikiliza ripoti ya rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini aliyeuwakilisha Umoja wa Afrika kufanya usuluhishi kuhusu mchakato wa amani ya Cote d'ivoire. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo atatoa ripoti kwenye mkutano huo kuhusu mchakato wa amani ya Darfur, Sudan. Kwenye mkutano huo, wajumbe pia watajadili mgogoro wa sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

   Vurugu za kivita zilizokuwepo kwa muda mrefu zimekuwa kikwazo sugu cha kuzuia maendeleo ya jamii na uchumi wa Bara la Afrika na kuleta umaskini na hali duni barani Afrika. Nchi nyingi za Afrika zimepoteza vitu vingi vikubwa. Tarehe 25 mwezi Mei mwaka jana, Umoja wa Afrika ulianzisha Baraza la amani na usalama badala ya muundo wa Umoja wa nchi huru za kiafrika ulioshughulikia kazi ya kuzuia na kutatua migogoro. Baraza la amani na usalama linaundwa na nchi wanachama 15, na limekuwa shirika kuu moja la Umoja wa Afrika. Baraza hilo lina madaraka ya kupelekea jeshi la kulinda amani kwa nchi wanachama wake ili kuingilia migogoro ya kijeshi, mauaji makubwa na vitendo vya kukiuka haki za binadamu. Pia lina madaraka ya kuitisha mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika ili kujadili masuala makubwa kama migogoro ya kikanda.

    Kuanzishwa kwa Baraza la amani na usalama na kupiga hatua kubwa kwa Umoja wa Afrika katika ujenzi wa miundo yake, na kuonesha nia imara ya nchi mbalimbali za Afrika ya kushirikiana na kujikakamua, kutegemea nguvu za ushirikiano kutatua migogoro, kulinda amani na usalama wa sehemu hiyo na kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa sehemu hiyo. Tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwezi Julai mwaka 2002, Umoja wa Afrika siku zote unafanya juhudi kupunguza na kuondoa migogoro ya aina mbalimbali ya kanda hiyo, na kuimarisha uwezo wake wa kuelekeza mambo ya sehemu ya Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, Umoja wa Afrika umejitahidi kushiriki katika usuluhishi wa migogoro ya Darfur na sehemu ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na kupeleka wachunguzi wa usimamishaji vita na majeshi ya kulinda amani, vitendo vyake halisi vimeonesha tena nia yake imara ya kutaka kutatua migogoro ya sehemu ya Afrika kwenye eneo la Afrika na kuziacha nchi za Afrika zenyewe zishughulikie mambo yao zenyewe.

    Umoja wa Afrika uliposisitiza kuelekeza utatuzi wa migogoro barani Afrika ulisema kuwa, Jumuiya hiyo haiachi kazi ya Jumuiya ya kimataifa. Maofisa wa Umoja wa Afrika siku zote wanasisitiza kuwa, kuziacha nchi za Afrika kutatua migogoro ya kisehemu kwenye eneo la Afrika hakumaanishi kuwa Umoja wa Afrika hautaki misaada ya Jumuiya ya kimataifa, tena hakumaanishi kuwa Umoja wa Afrika utafanya kazi badala ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala yanayohusika. Jumuiya za kimataifa pamoja na Umoja wa Mataifa zimefanya kazi kubwa kabisa katika kuusaidia Umoja wa Afrika kupunguza na kuondoa migogoro ya kanda ya Afrika, kama vile kutoa fedha zinazohitajika kwa dharura kwa Umoja wa Afrika katika kulinda amani ya sehemu ya Afrika, kutoa uhakikisho wa utoaji huduma na kuwaandaa walinzi wa amani. Maofisa wa Umoja wa Afrika wamesema kuwa, Umoja wa Afrika ukifanya kazi ya kuelekeza katika utatuzi wa migogoro ya kisehemu utasaidia kutumia ipasavyo juhudi za kujiamulia za nchi za Afrika na nguvu yake ya kijiografia, ambapo nchi za Afrika zinafanana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, Umoja wa Afrika unaweza kutumia "njia ya kiafrika" kutatua vizuri zaidi masuala mbalimbali.