Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-11 16:20:19    
Hifadhi ya mazingira ya asili kwenye kilele kirefu cha kwanza cha mlima duniani

cri
Duniani kuna milima na vilele vingi visivyo vya kawaida, lakini kilele cha mlima wa Himalaya kinachojulikana kwa jina la Zhumulangma, ambacho ni kirefu duniani, ni kilele kitakatifu machoni mwa watu, na kila wanapokumbuka kilele hicho hukumbuka pia makundi makubwa ya yak na paa yaliyoko chini ya mlima, pamoja na aina ya maua mazuri ya Xuelian yanayochanua kwenye kilele chenye theluji. Lakini katika muda wa nusu karne toka binadamu afike kwa mara ya kwanza kwenye kilele cha Zhumulangma katika miaka ya 50 ya karne iliyopita, takataka zilizotupwa huko na binadamu zimechafua ardhi hiyo safi. Ili kurejesha usafi wa kilele cha Zhumulangma, katika miaka ya karibuni watu waliojitolea wa sehemu mbalimbali nchini walifanya shughuli nyingi za kuhifadhi mazingira safi ya asili ya kilele cha Zhumulangma.

Tarehe 10 mwezi Septemba mwaka 2004 kijana Xu Zhiwei pamoja na watu 27 wengine waliojitolea kutoka sehemu mbalimbali nchini walianzisha kikundi cha kwanza cha watu waliojitolea, kisha wakafunga safari kuelekea kilele cha mlima Himalaya kilichoko kwenye umbali wa kilomita 130 wakitaka kuweka usafi kwenye kilele cha Zhumulangma.

Siku hiyo walifika kwenye wilaya ya Dingkou mkoani Sichuan, ambayo iko chini ya kilele cha mlima cha Zhumulangma. Walifika kwenye kambi zilizojengwa kwenye sehemu yenye urefu wa mita 5,200 kutoka kwenye usawa wa bahari ambapo mahema, malazi, chupa za oxygen na takataka zilizotupwa na watu zilikuwa nyingi kuliko walivyotarajia. Jambo lililowatia wasiwasi mkubwa ni kuwa takataka hizo zitaweza kuoza na kutoweka baada ya kupita muda wa zaidi ya miaka elfu moja kutokana na hali ya hewa ya huko kuwa kavu na yenye baridi kali.

Vijana walikuwa na pilikapilika ya kufanya usafi. Kwa kuwa vijana wengi waliojitolea walitoka kwenye sehemu ya tambarare, hawakuweza kuzoea hali ya huko ya uwanda wa juu. Muda mfupi baadaye, mwanamke mmoja bibi Liu Xiaolin alikuwa hajisikii vizuri.

"Ghafla nilijisikia vibaya, tumbo langu liliniuma sana kiasi cha kunifanya nitokwe na machozi. Ninaposhiriki kwenye shughuli hizo, huenda ni kutegemea ari ya kubeba jukumu la fahari, sikujali maumivu, lakini nilisikia maumivu makali baada ya kumaliza kazi."

Ili kuhakikisha afya ya watu wanaojitolea kufanya usafi, shughuli za kufanya usafi kazi hiyo ilifanyika katika eneo la karibu yao ya chini. Lakini takataka zilizotupwa hapa na pale ziliwafanya wasiweze kupumzika, katika siku ya pili baada ya kufika kwenye kambi yao kuu iliyoko mwanzoni mwa mlima, walipanda juu hadi kwenye kambi la No. 2 iliyoko kwenye urefu wa mita 6,500 juu ya usawa wa bahari.

Oxygen iliyoko katika hewa ya kambi ya No. 2 ni kiasi cha 40% ya hewa ya sehemu ya tambarare, wakati ule halijoto ya huko ulishuka na kufikia nyuzi 20 chini ya sifuri na upepo ulizidi nyuzi 7. vijana watano walifikia kwenye kambi ya No. 2 baada ya siku 3. Hali mbaya ya aina mbalimbali zikiwemo baridi kali, upungufu wa hewa ya oxygen ziliwaathiri watu watano akiwemo Xu Zhiwei.

"Takataka zingekuwa nyingi kama tungechukua vitu vingi vya mahitaji, kwa hiyo kifungua kinywa chetu kilikuwa ni kikombe kimoja cha kahawa na keki moja. Kazi zetu ni nyingi lakini chakula tunachokula ni chocolate na jelly, chakula cha usiku tunakula tambi zinazopikwa haraka, hivyo tulipungukiwa sana na nguvu mwilini."

Katika siku 6 tulizokuwa katika kambi ya No. 2, akina Xu Zhiwei walikusanya tani 2 za takataka, kila yak alitakiwa kubeba mifuko 4 hadi 5 ya takataka, wanyama hao wanaojulikana kuwa na nguvu nyingi walitembea katika hali ya kuyumbayumba kutokana na uzito wa mizigo waliyobeba. Vijana wale waliobaki katika kambi kuu ya chini vilevile walijitahidi sana, takataka walizokusanya katika siku hizo 6, zililundikwa pamoja na kuwa kama kilima.

Kila mahali walipofika vijana hao waliojitolea kukusanya takataka, watalii waliokuwa huko huvutiwa kushiriki katika shughuli zao. Hususan ni kuwa kikundi kimoja kilichoundwa na wapandaji wanane waliotoka Israel na Marekani, walipoona vijana wa China waliojitolea kukusanya takataka kwenye mahali penye urefu wa kwenda juu kwa zaidi ya mita 6,000 kutoka usawa wa bahari, waliwaoneshea vidole gumba na kushiriki katika shughuli zao. Hawakuwa na mifuko ya kuwekea takataka, hivyo walitumia mifuko yao ya kulalia, wakati walipowakabidhi vijana wale mifuko minane ya takataka, waliwapa zawadi ya bendera za taifa, moja ya Israel na moja ya Marekani. Walisema kuwa moyo wa wachina hao waliojitolea kuhifadhi mazingira ya asili ni mfano wa kuigwa, na wanastahili kuungwa mkono na watu wengine.

Katika siku 7 walizokuwa huko, Xu Zhiwei na wenzake walikukusanya zaidi ya tani 8 za takataka, ambazo nyingi zake zilipelekwa kushughulikiwa na kiwanda cha kuteketeza takataka kilichoko huko Tibet, na baadhi ya nyingine kidogo zilichukuliwa na vijana hao waliojitolea hadi Beijing, ambazo zilioneshwa kwa watu katika miji mitatu ya Beijing, Shanghai na Guangzhou. Katika mji wa Beijing peke yake, watazamaji walizidi laki moja.

Kutokana na mpango uliowekwa, katika miaka michache ijayo serikali ya China itapeleka maelfu ya wataalam wa hifadhi ya mazingira katika sehemu ya Zhumulangma kufanya upimaji na usawazishaji ili kuifanya sehemu hiyo iwe sehemu safi zaidi duniani.

Hivi sasa Bw. Xu Zhiwei na wenzake wamerejea katika maisha yao ya zamani na kuendeleza na shughuli zao. Bw. Xu Zhiwei mwenye umri wa miaka 35 mwaka huu ni mwanakiwanda, ambaye ametumia muda mwingi katika hifadhi ya mazingira ya asili, hivi sasa ameanzisha klabu ya hifadhi ya mazingira na tovuti ya hifadhi ya mazingira, ambapo zaidi ya wanachama elfu 3 wamejiandikisha.

        

Idhaa ya kiswahili 2005-01-11