|
Kutokana na mwaliko wa mamlaka ya utawala wa Palestina, Ujumbe wa uchunguzi wa China uliongozwa na balozi Yao Kuangyi tarehe 9 ulishuhudia uchaguzi wa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina, na kumaliza kazi hiyo kwa mafanikio. Tarehe 11, waziri wa mambo ya nje wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Nabil Shaath pia aliisifu kazi maalum uliyoifanya ujumbe huo wa China katika uchaguzi mkuu wa Palestina.
Balozi Yao Kuangyi alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari kuhusu hali ya uchaguzi mkuu wa Palestina alisema kuwa, anaona kuwa huo ni uchaguzi mkuu wenye mafanikio. Pia alisisitiza kuwa, mafanikio hayo yanategemea juhudi za mamalaka ya utawala wa Palestina na uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa.
Balozi Yao alisema: "Kwa ujumla, uchaguzi huo ulifanyika vizuri, ambapo wapigaji kura walitumia haki zao za kidemokrasia bila ya matatizo yoyote. Mafanikio hayo yanatokana na sababu mbili muhimu: Kwanza, baada ya kufariki dunia kwa mwenyekiti wa zamani wa mamlaka ya utawala wa Palestina Yasser Arafat, kazi za pande zote za mamlaka hiyo zilifanyika kwa utaratibu. Pili, uchaguzi huo ulipata uungaji mkono mkubwa wa jumuiya ya kimataifa. Licha ya China, ujumbe wa usimamizi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na wa Marekani vilevile ulishuhudia uchaguzi huo. Kutokana na hali hizo, uchaguzi huo uliendelea vizuri."
Balozi Yao alieleza kuwa, Ujumbe wa uchunguzi wa China wenye watu 6 uliwasili huko Ramallah, tarehe 8, Januari, mwaka huu. Wakati wa uchaguzi huo, walitembelea vituo 20 vya kupigia kura vilivyoko karibu na ukanda wa Gaza, kando ya magharibi ya mto Jordan na Jerusalem ya mashariki, na kupata habari za pande zote kuhusu hali halisi ya uchaguzi huo. Pia balozi Yao alidokeza kuwa, wakati wa uchaguzi huo, ujumbe wa usimamizi wa China vilevile ulifanya mawasiliano ya undani na ujumbe mwingine wa uchunguzi wa kimataifa ambao pia ulisifu sana uchaguzi huo.
Balozi Yao alisema: "Ujumbe wa uchunguzi wa China uliwasiliana na wasimamizi kutoka jumuiya mbalimbali za kimataifa na nchi kadhaa zikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Marekani. Wote wanaona kuwa, huo ni uchaguzi uliokuwa na haki na wa kidemokrasia na ulifanyika vizuri."
Kabla ya Ujumbe wa Uchunguzi wa China kurudi nchini baada ya kumaliza kazi, waziri wa mambo ya nje wa Mamlaka ya Utawala wa Palestina Bw. Nabil Shaath tarehe 11 alikutana na ujumbe huo. Balozi Yao alieleza kuwa, kwenye mazungumzo hayo, Bw. Shaath alitoa shukurani kwa uungaji mkono wa serikali ya China kwa wapalestina, na kusifu kazi maalum wa ujumbe huo wa China katika uchaguzi mkuu wa Palestina. Pia alieleza kuwa, suala la Mashariki ya Kati halitatatuliwa bila ya China kushiriki , na Palestina inatumai kuwa China itatoa mchango mkubwa zaidi katika shughuli hiyo.
Balozi Yaoalisema: " Leo nimekutana na waziri wa mambo ya nje wa Palestina Bw. Nabil Shaath. Bw. Shaath anatumai kuwa China itaendelea kuunga mkono mapambano ya haki ya wapalestina. Ikiwa ni nchi kubwa na nchi mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, China itatoa mchango wake na kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuondoa migogoro kati ya Palestina na Israel na kurejesha mazungumzo ya amani kati yao."
Vilevile Bw. Shaath alisisitiza kuwa, muda mfupi baada ya Bw. Mahmoud Abbas kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina, rais Hu Jintao wa China salamu za pongezi kwa wakati, ambayo ni hatua muhimu ya kuunga mkono viongozi wapya wa Palestina, na vilevile inatia moyo harakati ya wapalestina ya kulinda maslahi ya taifa.
Kwenye mazungumzo hayo, Balozi Yao alisisitiza kuwa, serikali ya China inazingatia sana uchaguzi huo wa Palestina, na imepeleka ujumbe wa uchunguzi katika uchaguzi mkuu wa Palesitina ili kuunga mkono wananchi wa Palestina.
Ujumbe wa wachunguzi wa China uliondoka kutoka Palestina tarehe 11.
Idhaa ya Kiswahili 2005-01-12
|