Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-12 20:19:50    
Namna ya kupika vipande virefu vya nyama ya nguruwe kwa sosi tamu

cri

Mahitaji

Nyama ya nguruwe gramu 250, sosi tamu gramu 80, vitunguu maji gramu 250, mvinyo wa kupikia gramu 5, M.S.G gramu 2, tangawizi gramu 5,sukari gramu 20, chumvi gramu 1, wanga gramu 2, yai 1, mafuta gramu 150.

Njia

1. kata nyama iwe vipande vipande vyebamba, halafu vichanganye pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, yai lililokorogwa, wanga, halafu koroga kwa pamoja.

2. kata vitunguu maji viwe vipande vipande na uviweke kwenye sahani. Pigapiga tangawizi iwe laini na kuiweke kwenye bakuli na vitunguu maji gramu 2, kasha mimina kiasi kidogo cha maji.

3. Pasha moto mafuta mpaka yawe na joto la nyuzi 50 hivi, tia vipande vya nyama, vikorogekoroge mpaka viive kwa asilimia kama 80, kisha vitoe bila ya mafuta.

4. pasha moto tena, tia mafuta kidogo. Tia sosi tamu, maji yenye vitunguu maji na tangawizi, M.S.G, sukari, wanga wa maji, korogakoroga mpaka sukari iyeyuke na sosi tamu ibadilike na kuwa ya kunata, tia vipande vya nyama, vikorogekoroge mpaka vipande vya nyama vichanganyikane na sosi tamu sawasawa, vipakue na uviweke juu ya vipande vya vitunguu maji vilivyowekwa ndani ya sahani. Kitoweo hicho sasa kiko tayari.