Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-12 21:42:59    
Oparesheni yafanya tabasamu iwe nzuri zaidi

cri

    Ugonjwa wa kupasuka kwa midomo na taya ni ugonjwa wa kawaida baada ya kuzaliwa, si kama tu linaathiri sura na uwezo wa kuongea kwa watu wenye ugonjwa huo, bali pia lina athari mbaya kiroho kwa watu hao. Kwenye sehemu za kaskazini za China, kwa wastani mtoto mmoja kati ya watoto wachanga 600 anazaliwa na ugonjwa huo.

    Kutokana na takwimu husika, kutibu ugonjwa huo kunahitaji karibu yuani elfu 7, na familia maskini za China hazidumu kugharamia matibabu hayo, hivyo watu wengi wenye ugonjwa huo hawajapata matibabu mazuri. Ili kuwasaidia watu hao maskini, mwaka 1999, jumuiya moja ya hisani ya kimataifa iitwayo "garimoshi la tabasamu (Smile Train)", ikishirikiana na shirika kuu la hisani la China, ilianzisha mradi wa kutoa oparesheni bure kwa wachina maskini wenye ugonjwa huo.

    Leo tutaeleza kidogo kuhusu mradi huo kwa kumzungumzia mgonjwa mmoja.

    Wasikilizaji wapendwa, ukisikiliza wimbo huu wa kuvutia, unaweza kuamini kuwa mtoto huyu alikuwa hawezi kuongea kama kawaida, na hata kushindwa kutabasamu? Mtoto huyo anaitwa Liu Yang, aliwahi kuwa na ugonjwa wa kupasuka kwa midomo na taya. Akisaidiwa na jumuiya ya hisani ya kimataifa na shirika kuu la hisani la China, mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano tu amepata uso mpya mwenye tabasamu na kuanza maisha mapya.

    Jumuiya ya "garimoshi la tabasamu" ni jumuiya ya hisani ya kimataifa ambayo makao makuu yake yako nchini Marekani, lengo lake ni kuondoa ugonjwa wa kupasuka kwa midomo na taya duniani, na kusaidia kuboresha maisha ya watu wenye ugonjwa huo. Mwezi Machi mwaka 1999, jumuiya hiyo na shirika kuu la hisani la China zilifikia makubaliano kuwa, jumuiya hiyo itatoa fedha, na shirika kuu la hisani la China litachukua hatua na kuanzisha mradi huo kwa ushirikiano. Ili kutekeleza mradi huo, shirika kuu la hisani la China lilichagua hospitali zaidi ya 110 kwenye sehemu zenye watu wengi wenye ugonjwa huo, na kutoa mafunzo maalum kwa madaktari ili kuinua kiwango chao cha kufanya oparesheni ya kutibu ugonjwa huo; mradi huo pia ulianzisha utafiti husika, ili kutafuta chanzo cha ugonjwa huo na matibabu yake bora.

    Bw. Liu Zhao jie ni baba wa Liu Yang. Tokea siku alipozaliwa mtoto wake, alikuwa na matumaini makubwa kuwa iko siku, Liu Yang ataweza kuwa na sura nzuri na ya kupendeza kama watoto wengine wa kawaida. Kutokana na umaskani wa familia yake, matumaini yake hayakutimizwa. Wakati Bw. Liu alipojua kuwa mradi wa kutoa oparesheni bure kwa wachina maskini wenye ugonjwa huo unafanyika katika maskani yake, mara moja alimpeleka mtoto wake kwenye hospitali ya huko iliyochaguliwa ili kupata matibabu. Baada ya oparesheni, Liu Yang alikuwa na sura mpya. Bw. Liu alifurahia sana kuona tabasamu ya mtoto wake. Akisema kuwa,

    Oparesheni ilifanywa vizuri, mtoto wangu ataongea kama kawaida, nakushukuru sana.

   Kutokana na maelezo, watoto wenye ugonjwa huo wanapaswa kufanyiwa oparesheni mbili, moja ni kurekebisha midomo na nyingine ni kurekebisha taya. Aidha, baadhi ya oparesheni zinahitaji marekebisho ya ziada. Wakati wa kufanya marekebisho hayo, madaktari watatoa mafunzo ya lugha na matibabu ya kisaikolojia ili kuwasaidia kurejea kwenye maisha ya afya na kuwa na furaha kama watu wa kawaida baada ya oparesheni.

    Tokea mradi huo ulipoanzishwa katika mji wa Cangzhou mkoani Hebei mwaka 2001, watu zaidi ya 1000 wenye ugonjwa huo wamepata matibabu. Mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya midomo ya hospitali ya umma ya Cangzhou Bi. Zhao Shijun ni daktari mkuu anayefanya oparesheni ya kurekebisha ugonjwa huo, alipohojiwa na mwandishi wa habari, alisema,

    anaweza kumaliza oparesheni 7 kama hiyo kwa siku, ingawa anachoka sana baada ya kufanya oparesheni hizo, lakini anafurahia kuwaponesha watoto wenye ugonjwa huo na kuishi maisha ya kawaida.

    Shirika kuu la hisani la China lilidokeza kuwa, kuanzia mwaka 1999, Jumuiya ya "garimoshi la tabasamu" kwa jumla imetoa mchango wa yuan milioni 160 kwa wachina wenye ugonjwa huo, na mpaka sasa watu zaidi ya elfu 60 wamepata matibabu. Ofisa wa shirika kuu la hisani la China anayeshughulikia mradi huo Bw. Chang Hanying alisema kuwa, mradi huo unaendelea vizuri na umeleta matokeo mazuri sana. Akisema,

    Wakati mradi huo ulipoanzishwa, kulikuwa na watu wengi wazima waliokuwa na ugonjwa huo, wakiwa ni pamoja na watu wenye umri wa miaka 20 hadi 30, hata watu wenye umri wa 50 hadi 60, ambao hawakupata matibabu kutokana na umasikini. Lakini hivi sasa wagonjwa wengi waliofanyiwa oparesheni hiyo ni watoto wachanga.

    Bw. Chang Hanying alisema kuwa, mpaka sasa, watu wengi wenye ugonjwa huo kwenye sehemu zenye mawasiliano mazuri wamepata matibabu. Alidokeza kuwa, mwaka 2005 shirika hilo litafanya shughuli kubwa ya uhamasishaji, na kueneza habari ya kutoa matibabu bure kwa watu wenye ugonjwa huo kwenye sehemu za mbali na sehemu maskini, ili kuwasaidia watu wote wenye ugonjwa huo wapate matibabu mazuri kwa wakati.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-12