Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-14 14:16:44    
Wakulima laki 4 wa sehemu ya milimani katika vitongoji vya nje ya Beijing watimiza "kupata ajira kwa kuhifadhi milima"

cri
Bi. Pei Deling mwenye umri wa miaka 39 ni mkulima wa kijiji cha Huang Yukou katika wilaya ya Mi Yun ya Beijing. Mwezi mmoja uliopita, aliteuliwa kuwa mlinzi wa misitu ya biolojia katika kijiji hicho kushughulikia kazi ya usimamizi na hifadhi ya misitu ya biolojia yenye hekta 328, na kutimiza "kupata ajira kwa kulinda misitu". Mapato yake ya mwaka mmoja yameweza kuongezeka kwa yuan elfu 5, na amekuwa mtu anayefaidika kutokana na utaratibu wa utoaji ruzuku kwa ulinzi wa misitu ya biolojia katika sehemu ya milimani hapa Beijing.

Mwandishi wetu wa habari alikwenda katika kijiji cha Huang Yu kutoka wilaya ya Mi Yun. Njiani aliwaona wasimamizi waliovaa alama nyekundu mikononi. Watu hao ni walinzi wa misitu, na pia ni wazima moto wa misitu hiyo. Wanabeba jukumu la kulinda na kutunza misitu ya biolojia katika sehemu hiyo.

Katibu wa tawi la Chama cha Kikomunisti cha China la kijiji hicho Bw. Wang Mingquan alijulisha kuwa, zamani wanavijiji hawakuwa na mapato mengine, waliishi kwa kutegemea matunda ya milimani, na kukata ovyo miti milimani. Baada ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji ruzuku kwa ulinzi wa misitu ya biolojia katika sehemu ya milimani hapa Beijing, wanakijiji hao wamekuwa na mwamko mkubwa wa kusimamia na kulinda misitu, na mapato yao yameongezeka dhahiri. Kutokana na takwimu, kijiji hicho kina familia 130 na watu 365. Katika mwaka wa kwanza, watu 56 walishiriki katika kazi hiyo, kila mtu alishughulikia eneo la misitu lenye hekta 321 na kupata malipo ya yuan 4768 kila mwaka kwa wastani. Mapato ya kila mkulima wa kijiji hicho yameongezeka kwa yuan 732.

Zamani, hakukuwa na utaratibu mzuri wa utoaji ruzuku kwa ulinzi wa misitu ya biolojia, kwa hiyo usimamizi na hifadhi ya misitu hiyo haukufanya kazi kama ilivyotarajiwa, na pia iliathiri maendeleo ya uchumi katika sehemu hiyo ya milimani pamoja na mapato ya wakulima. Utaratibu wa utoaji ruzuku kwa hifadhi ya misitu ya biolojia ulitolewa mwaka jana, ili kutekeleza "kupata ajira kwa kuhifadhi misitu, kuwapatia ruzuku wakulima kwa misitu wakulima kwa utaratibu, na kuanganisha kazi ujenzi na usimamizi". Baada ya kufanya utafiti wa makini, serikali ya Beijing iliamua wapa ruzuku walinzi wa misitu yuan mia 4 kila mwezi kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2010. Vijiji husika vinatarajiwa kuweka nafasi za walinzi kwa kufuata mazingira mwafaka.

Tume ya kilimo ya Beijing ilijulisha kuwa, kuna vijiji 1577 katika wilaya 10 za sehemu za milimani hapa Beijing, walinzi na wasimamizi elfu 42.99 wameteuliwa, makundi maalumu 1820 yameanzishwa, na usimamizi na hifadhi ya misitu ya biolojia yenye hekta milioni 9.12 unafanywa na walinzi wa wasimamizi husika. Katika vijiji yenye upungufu wa misitu ya biolojia, umetekelezwa utaratibu wa kubadilishana zamu za wasimamizi. Wasimamizi zaidi ya elfu 40 waliteuliwa kutoka kwa watu waliojiandikisha katika uchaguzi huo. Majina ya wasimamizi hao wote yalijulikana vijijini, wasimamizi hao walipewa mafunzo kabla ya kuanza kufanya kazi, na kusaini mikataba ya kubeba wajibu na shirika vijijini.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-14