Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-14 14:34:54    
Jumba la kwanza la makumbusho la hali ya viumbe lisilo kiserikali nchini China lafunguliwa wilayani Liping, mkoani Guizhou

cri
Jumba la kwanza la makumbusho la hali ya viumbe lisilo la kiserikali nchini China??jumba la makumbusho la hali ya viumbe la kabila la Wadong, lilifunguliwa tarehe 8 huko wilayani Liping, mkoani Guizhou. Jumba hilo ni jumba la tano la makumbusho hayo mkoani Guizhou, na pia ni jumba la pili la kabila la Wadong wilayani Liping.

Jumba hilo lilipendekezwa na kuanzishwa na wenyeji. Madhumuni yake ni kulinda utamaduni wa hali halisi ya viumbe ya kisehemu, kuurithi na kuuendeleza, pia kuboresha hali ya maisha ya wenyeji. Jumba hilo vilevile ni kituo cha kuchunguza hali ya viumbe ya kabila la Wadong, kuenzi lugha ya kabila hilo, kufahamu opera, muziki na sanaa za jadi za kabila hilo. Pia linatumika kwa ajili ya makongamano na maingiliano ya utamaduni na kuwaalika wataalam kufanya kazi katika jumba hilo la makumbusho, ili kuchunguza hali ya viumbe ya kabila la Wadong na utamaduni wake wenye historia ndefu.

Kijiji cha Wadong kiko ndani ya sehemu inayojiendesha ya kabila la Wamiao na kabila la Wadong, mkoani Guizhou. Huko kijijini kuna familia zaidi ya 500, na watu zaidi ya 2,300, ambao wote ni wa kabila la Wadong. Kijiji hicho kinahifadhi vizuri utamaduni wa hali halisi ya viumbe ya kabila la Wadong, pia kuna utamaduni wa pekee wa kabila hilo Dong. Neno Dimen, jina la sehemu hiyo ni matamshi ya lugha ya kabila. Maana yake ni mahala penye chemchemi, na ni mahala penye ustawi. Kwa mujibu wa nyimbo za kale za kabila la Wadong, watu wa kabila hilo walianza kuishi hapo tokea Enzi ya Tang, una miaka 1,000 iliyopita.

Katika sehemu ya kabila la Wadong, kila kijiji kina kikundi cha opera ya kabila la Wadong na kila sikukuu kinaonesha tamasha la opera hizo. Hivi sasa, kuna vikundi vya opera karibu 30 katika kijiji hicho, opera hizo ambazo zinahifadhi vizuri utamaduni wa hali halisi ya viumbe wa kabila la Wadong. Licha ya opera za Wadong, kijijini hapo kuna kumbu kumbu nyingine za kale kama vile kisima, barabara, majengo, na utamaduni usioonekana kama nyimbo za kabila la Wadong, na chakula maalum cha kijadi.

Mwanzoni dhana ya jumba la makumbusho la hali ya viumbe ni kukumbuka na kurudisha utamaduni wa kiasili. Lakini mpaka mwishoni mwa karne ya 20, jumba la makumbusho la hali ya viumbe limekuwa njia maalum ya kulinda na kuhifadhi urithi wa utamaduni. Hivi sasa, majumba ya makumbusho ya hali ya viumbe zaidi ya 300 yamejengwa duniani. Dhana ya jumba la makumbusho la hali ya viumbe kwanza ilijulikana katika mkoa wa Guizhou na halafu ikaenea sehemu nyingine nchini China. Mnamo tarehe 31, mwezi Oktoba, 1998, jumba la makumbusho la hali ya viumbe ya kabila la Wamiao mkoani Guizhou lilifunguliwa, ambalo ni la kwanza nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-14