Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-14 21:21:12    
Mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia una makada laki 1.9 wa makabila madogo madogo

cri

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kamati inayoshughulikia mambo ya makabila madogo madogo ya mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia, hivi sasa mkoa huo una makada laki moja na elfu tisini wa makabila madogo madogo, ambao wanachukua robo ya makada wote wa mikoani, kiasi hicho kimezidi kile cha watu wa makabila madogo madogo ambao wanachukua asilimia 21 ya idadi ya watu wa mkoa huo.

    Zaidi ya hayo, makada wa makabila madogo madogo wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia wamepewa nyadhifa muhimu. Mkurugenzi wa kamati inayoshughulikia mambo ya makabila madogo madogo ya kamati ya kudumu ya watu wa mkoa huo Bwana Baren alifahamisha kuwa, hivi sasa, mwenyekiti wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia na wakuu wa wilaya tatu za makabila matatu ya Dawor, Ewenke na Elunchun ni wakazi wa makabila madogo, na nyadhifa nyingine nyingi katika sehemu zenye idadi kubwa ya watu wa makabila madogo pia zinashikwa na wakazi wa makabila madogo. Alisema kuwa, sera ya mikoa inayojjiendesha ya makabila madogo madogo ya China inatekelezwa vizuri sana katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia, watu wa makabila madogo madogo wamekuwa na haki ya kushughulikia mambo ya ndani ya makabila hayo.

    Mwenyekiti wa sasa wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia Bwana Yang Jing ni wa kabila la wamongolia. Tangu awe mwenyekiti amewaongoza watu wa makabila mbalimbali kuendeleza vizuri uchumi, na hali ya maisha ya wakazi wa mkoa huo imeinuka kidhahiri.

    Kwa mujibu wa sensa ya idadi ya watu iliyofanyika hivi karibuni, mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia una idadi ya watu milioni 23.79, kati yao watu milioni 5 ni wa makabila madogo madogo, kama vile kabila la Mongolia, Man, Hui, Russia, Dawor, Ewenke na Elunchun.

    Bwana Baren alisema kuwa, kuongezeka kwa idadi ya makada wa makabila madogo madogo mikoani kunatokana na kuboreshwa kwa sera ya makabila madogo madogo nchini China, na kuinuka kwa mwamko wa kushiriki katika mambo ya kisiasa kwa wakazi wa makabila madogo. Tangu China mpya iasisiwe, serikali ya China siku zote inatilia maanani kuwaandaa na kuwatumia makada wa makabila madogo madogo, na kuweka vifungu maalum katika katiba ya Jamhuri ya watu wa China na sheria ya mikoa inayojjiendesha ya makabila madogo madogo ya Jamhuri ya watu wa China. Bwana Baren alifahamisha kuwa, hivi sasa kiasi kikubwa cha makada wa makabila madogo wa mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia wamepata elimu ya juu, na karibu wote wamepata mafunzo maalum.

    Katika miaka zaidi ya 50 iliyopita, serikali ya China imetilia maanani sana elimu ya sehemu za makabila madogo madogo, watoto wote wa makabila madogo madogo wanapata elimu ya msingi bure. Hivi sasa, mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia umeunda mfumo kamili wa kutoa mafunzo kwa lugha ya kimongolia kuanzia elimu ya chekechekea hadi chuo kikuu: una shule za msingi zaidi ya 1600 na shule za sekondari zaidi ya 300 za makabila madogo madogo na vyuo vikuu zaidi ya 20. Kabla ya kuanzishwa kwa mkoa unaojiendesha wa kabila la wamongolia mwaka 1947, mkoa huo haukuwa na chuo kikuu hata kimoja.

    Mwanafunzi wa kabila la wamongolia anayesoma chuo kikuu Bwana Hasi alisema kuwa: elimu ni chanzo cha maendeleo ya kikabila, akiwa mwanafunzi wa kabila la wamongolia, siku zote anaona ufuatiliaji na uungaji mkono wa serikali kwa elimu ya makabila madogo madogo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-14