Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-15 14:52:46    
Vyombo vya Kauri vya Qinghua

cri

    Qinghua ni jina maalumu la aina moja ya vyombo vya kauri. Msanii huchora michoro juu ya vyombo vibichi vya ufinyanzi kwa rangi ya cobalt, halafu hupaka kauri; baada ya kukauka vinawekwa ndani ya tanuri lenye nyuzi joto kuanzia 1,200 C hadi 1,300 C. Vyombo vya kauri hupakwa rangi za buluu na nyeupe zisizopauka daima. Vyombo vya kauri vya Qinghua vilianza kutengenezwa katika vipindi vya Enzi ya Tang na Song mwaka (618-1279). Katika kipindi cha Enzi ya Ming (mwaka 1368-1644), vyombo hivi vilikuwa vikiendelezwa na kustawisa katika miaka ya 1940 hadi 1950 vilianza kufufua. Toleo hili linachapisha habari za vyombo vya kauri vya Qinghua vilivyotengenezwa katika kipindi cha Enzi ya Qing (mwaka 1644-1911) kutoka majimbo ya Shandong, Henan, Hebei, Jiangxi na Zhejiang.

    Wasanii hutumia rangi nzito na nyeusi ya cobalt kuchora picha za binadamu, wanyama, mito na milima kwa kufuata mapokeo ya uchoraji wa Kichina.

    Wafinyanzi na wasanii wengi wenye ufundi wa kuenyeji hutoka vijijini; kwa hivyo, hawakupata nafasi kubwa ya kuandikwa katika historia. Lakini, vyombo vya kauri vya Qinghua vilivyotengenezwa nao vinapendwa sana na wananchi.