|
Zaidi ya siku 20 zimepita tangu yatokee maafa ya mawimbi makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi (tsunami) baharini Hindi. Kutokana na msaada wa jumuiya ya kimataifa na juhudi za serikali na wananchi wa Indonesia, watu wa Banda aceh, mji ulioathirika vibaya na maafa ya tsunami, sasa wameanza kuishi kama kawaida. Sokoni zimeanza kujaa bidhaa, bei ni za kawaida, na hospitali pia zimeanza kazi tena.
Sokoni ndizi na machungwa yaliyochumwa katika muda mfupi zimelundikana, wateja wamekuwa wengi wakichagua mahitaji au kukubaliana bei.
Hilo ni soko moja la uwanjani lililosalimika karibu na barabara moja mjini Banda aceh. Ndani ya mitaro pembeni mwa barabara hiyo yamejaa matope na takataka zilizoletwa na maji ya bahari, hali hiyo inawafahamisha watu kuwa eneo hilo limewahi kukumbwa na maafa makubwa. Pande mbili za barabara kila baada ya mita 10 hivi alisimama askari mmoja mwenye silaha begani na kitambaa kilichofunika mdomoni akielekeza magari yanayopita. Hali ya sokoni ilikuwa tulivu, wateja walikuwa wengi wakichagua wanachohitaji na kukubaliana bei.
Raia mmoja wa huko aliyejitokeza katika uokoaji mwenye asili ya China aliwaambia waandishi wa habari akisema kuwa kabla ya tsunami kutokea, huko mjini kulikuwa na masoko zaidi ya 40, sasa yaliyobaki ni matatu tu, mengine yote yamekuwa vifusi. Baada ya tsunami kutokea bei za bidhaa ziliwahi kupanda juu na baadhi ya vitu vya lazima kwa maisha havikupatikana. Kutokana na hali ya kawaida ya jamii kurudia siku hadi siku na mawasiliano kupatikana, maisha ya watu wa Banda aceh yamekuwa ya kawaida, na bei zilizopanda zimeanza kupungua.
Tsunami sio tu imeleta janga kubwa kwa vifo vya watu wengi na mali nyingi, na pia watu wengi walipata ugonjwa wa pepopunda na magonjwa mengine. Kutokana na uharibifu wa hospitali, juhudi za kurudisha kazi ya hospitali na kuwaokoa wagonjwa hao ni za lazima na za haraka. Katika siku hizo waokoaji wa jumuiya ya kimataifa wakiwemo watu wa vikundi vya matibabu vya China walifanya juhudi usiku na mchana wakipigania kurudisha kazi ya hospitali ya Banda aceh. Baada ya tsunami kutokea, matope kiasi cha nusu mita yalijaa hospitalini, watu hawakuweza kuingia. Lakini tarehe 16 waandishi wa habari walipokuja huko, waliona matope yamepungua sana, nyumba nyingine zimeanza kutumika, mbali na baadhi ya nyumba zilizokuwa zimesafishwa kabla ya hapo. Kutokana na juhudi za waokoaji wa jumuiya ya kimataifa nyumba za hospitali zimekuwa safi, sakafu ya tarazo inang'ara tena. Hivi sasa vitanda vya hospitali vinavyoweza kutumika vimefikia 120, na vingine zaidi ya 30 vitatumika hivi karibuni.
Kazi ya kutafuta na kuwaokoa watu waliokumbwa na janga inaendelea, barabarani mara kwa mara kuna magari yaliyobeba askari yakipita kwa kasi, askari mmoja wa jeshi la majini la Indonesia aliwaambia waandishi wa habari kuwa kila siku wanakwenda kwenye viunga vya Banda aceh kutafuta watu ambao hawajulikani walipo na kusafisha takataka, ingawa hali ya huzuni inawakumba, lakini askari huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba "Yote yatapita, na mambo yatakuwa sawa."
Idhaa ya kiswahili 2005-01-17
|