Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-17 16:44:13    
Raia wa Kawaida Wazingatiwe Kupewa Utamaduni

cri
Kupeleka sahani za video zenye michezo ya kuvutia na kupeleka vitabu kwenye sehemu za ujenzi wanazokaa wajenzi watokao vijijini, kufanya tamasha la wasanii wakubwa pamoja na wajenzi hao na kuwaandalia wafanyakazi hao madarasa ya sanaa za michezo huko walipo??Shughuli hizo zilizofanywa na Wizara ya Utamaduni na Wizara ya Kueneza Utamaduni zilichangamsha maisha ya utamaduni ya wajenzi waliotoka vijijini na kuwafurahisha?? Waziri wa utamaduni wa China Bw. Sun Jiazheng hivi karibuni alisema kuwa raia wa kawaida lazima wapewe macho kupewa utamaduni. Alisema, katika mwaka 2005 wizara ya utamaduni itatilia maanani maisha ya utamaduni ya vibarua wanaotoka vijijini zaidi ya milioni 100 mijini.

Bw. Sun Jiazheng alisema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa taifa wa wakuu wa idara za utamaduni. Alisema, kazi ya utamaduni katika mwaka 2003 ilipata mafanikio makubwa, lakini pia kulikuwa na matatizo matatu muhimu, nayo ni mfumo wa huduma za utamaduni miongoni mwa umma bado haujakamilika, na maisha ya utamaduni vijijini yalikuwa duni. Pili, Usimamizi wa soko la utamaduni haujaimarika na hasa usimamizi katika ngazi ya shina. Tatu, uongozi na huduma za idara za utamaduni haujafikia kiwango kinachotakiwa.

Bw. Sun Jiazheng aliongeza kuwa katika mwaka 2005 wasanii wanapaswa kujiunga na maisha na mazingira halisi, wawajali vichipukizi na maandishi mapya ili kustawisha zaidi utungaji wa michezo ya sanaa. Ujenzi wa "jumba la taifa la tamthilia", "jumba la taifa la makumbusho" na ukarabati wa "kasri la kifalme la Beijing" utaendelea, na kujitahidi kukamilisha mfumo wa huduma za utamaduni miongoni mwa umma, kuendelea na mageuzi ya mfumo wa utamaduni kwa kina zaidi, na kuharakisha maendeleo ya mashirika ya utamaduni na kuendelea kuliweka soko la utamaduni katika hali ya kufuata sheria na kukamilisha mfumo wa soko la utamaduni hatua kwa hatua, kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika juhudi za kuhalalisha klabu za mtandao wa tovuti na kupambana vitendo vya kurudufu na biashara haramu ya sahani za video. Kuendelea na juhudi za kutangaza utamaduni wa China duniani, na kustawisha maingiliano ya kiutamaduni na nchi za nje katika ngazi za juu na kuhifadhi kumbukumbu za urithi wa utamaduni na hasa kumbukumbu za kale katika sehemu ya Magenge Matatu ya Mto Changjiang.

Bw. Sun alisema, mwaka huu ni mwaka wa mwisho wa "Mpango wa Kumi wa Miaka Mitano ya Maendeleo" na pia ni mwaka muhimu wa mageuzi ya mfumo na ujenzi wa utamaduni wa China. Naibu waziri wa kueneza utamaduni Bw. Li Congjun alisema kuwa huduma zetu za utamaduni hazijaweza kukidhi mahitaji ya umma, hata Beijing kwa wastani kila mmoja hajapata kuangalia filamu moja kwa mwaka. Maendeleo makubwa ya ujenzi wa utamaduni hayawezi kupatikana bila kuwa na shinikizo na kufanya juhudi kubwa katika miaka 20 ya mwanzo ya karne hii na kuzikomboa na kuziendeleza nguvu za utamaduni.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-17