Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-18 16:00:46    
Abbas achukua hatua za kuwazuia watu wenye siasa kali kuishambulia Israel

cri
Ili hali kati ya Palestina na Israel isiendelee kuwa mbaya, mamlaka ya utawala wa Palestina hivi karibuni imechukua hatua nyingi mfululizo ili kuwazuia watu wenye silaha wa Palestina kuendelea kuishambulia Israel. Maoni ya jamii yanaona kuwa hatua hizo zitapima uwezo na heshima kwa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Abbas.

Baada ya mkutano wa baraza la serikali na kamati ya usalama ulioitishwa na Abbas na waziri mkuu Ourei, jana Abbas aliamrisha jeshi la usalama la Palestina lililopo katika sehemu ya Gaza kuchukua hatua za kuwazuia watu wenye siasa kali wa Palestina kuishambulia Israel, na kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kushambulia vituo vya ukaguzi vya Israel. Waziri mkuu Qurei pia alisema kuwa nia ya viongozi wa Palestina kusimamisha vitendo vya mashambulizi ni "thabiti", yeyote anayekwenda kinyume cha amri ataadhibiwa.

Ofisa mmoja anayeshughulikia usalama wa Palestina alidokeza kuwa ikiwa ni moja kati ya hatua za kudhibiti wenye siasa kali serikali ya Palestina inatumai kuwaingiza watu wenye silaha kwenye jeshi la ulinzi la Palestina kwa kufanya mazungumzo nao. Jana Bw. Abbas alisema wazi kuwa atawaingiza askari wa Al-Aqsa Martyrs Brigade iliyo chini ya Fatah kwenye jeshi la ulinzi la Palestina. Imefahamika kuwa kesho Bw. Abbas atakwenda kwenye sehemu ya Gaza na kufanya mazungumzo na vikundi mbalimbali kuhusu utatuzi wa matatizo ya usalama nchini Palestina na kusimamisha mashambulizi dhidi ya Israel.

Habari nyingine zinasema kuwa mageuzi ya jeshi la usalama la Palestina pia yamepangwa katika ajenda. Kwa mpango Abbas anataka kuvigawa vikosi 12 vya jeshi la usalama la Palestina kuwa nguvu za aina tatu yaani polisi wa umma, upelelezi na jeshi la usalama la taifa ili kumaliza hali ya kujitawala ya vikosi hivyo na kuimarisha uongozi na mshikamano wa kijeshi na kuleta tishio kubwa zaidi kwa vikundi vyenye siasa kali vinavyozidi kuwa na nguvu siku hadi siku.

Wachambuzi wanaona kuwa vikwazo vitakuwa vingi mbele ya malengo hayo ya Bw. Abbas.

Baada ya Abbas kutoa amri kwa jeshi la usalama la Palestina kuzuia vikundi vya siasa kali kushambulia Israel, chama cha Hamas, harakati ya ukombozi wa watu wa Palestina pamoja na "Brigades" mara moja walitangaza kupinga. Msemaji wa Hamas aliyeko Gaza Bw. Abu Zuhri alisema, Abbas anataka kudhoofisha mapambano ya halali ya watu wa Palestina dhidi ya Israel. Harakati ya ukombozi ya watu wa Palestina inasema kuwa itaendelea mashambuzi yake dhidi ya Israel mpaka nchi hiyo iondoke kutoka sehemu ya Palestina. "Brigades" pia ilikataa kujiunga na jeshi la usalama la Palestina, lakini ilisema kuwa itaendelea na mazungumzo na Fatah. Wachambuzi wanaona kuwa sababu ya vikundi hivyo kukataa maagizo ya Abbas kusimamisha mashambulizi na kujiunga na jeshi la usalama la Palestina ni kuwa mapambano yao ya kijeshi sio tu aina moja ya kupinga ukaliaji haramu wa Israel, na pia ni aina yao ya kudumisha athari zao za kisasa. Wanaona kuwa ukaidi wa vikosi hivyo pia ni kwa ajili ya kujiinulia uzito katika mgawo wa madaraka, kwa hiyo vikundi hivyo havijafunga kabisa mlango wa kufanya mazungumzo na Abbas.

Licha ya vizuizi humo nchini Palestina, Abbas pia anakalibiliana na shinikizo kutoka Israel. Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon siku chache zilizopita alifanya mashambulizi makali katika sehemu ya Gaza ili kumlazimisha Abbas achukue hatua kali dhidi ya vikundi vyenye siasa kali vya Palestina. Ingawa kutokana na kusuluhishwa na Misri na nchi nyingine Israel imesema kuwa itasimamisha vitendo vyake vya kijeshi kwa muda ili kumpa muda Abbas.

Wachambuzi wanaona kuwa kuvizuia vikundi vyenye siasa kali vya Palestina, kusuluhisha vema uhusiano kati yake na vikundi hivyo limekuwa tatizo kubwa mbele ya Abbas tokea ashike wadhifa wa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina. Kuweza au kutoweza kutatua tatizo hilo katika mazingira ya kushinikizwa kutoka ndani na nje ya nchi ni muhimu sana kwa mustakbali wa Abbas na pia kwa mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-18