Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-19 19:25:57    
Raia wa China watekwa nyara nchini Iraq

cri

    Ubalozi wa China nchini Iraq tarehe 18 ulithibitisha kuwa raia wanane wachina wametekwa nyara nchini Iraq na wanadiplomasia wa China wanafanya juhudi kadiri kwa wawezavyo kuwaokoa mateka hao.

    Habari hiyo ilitolewa kwanza na kituo cha televisheni al Jazeera cha Qatar. Kituo hicho tarehe 18 kilionesha sehemu ya video kuwa raia wanane wachina waliotekwa nyara wakiwa wamesimama mbele ya jengo moja wakinyanyua pasipoti zao za China na wanaume wawili wenye silaha waliofunika nyuso zao walikuwa wamesimama kando yao. Kutokana na video hivyo, tunaweza kuona kuwa hali ya mateka hao wenyewe inaonekana kuwa ni nzuri.

    Baadaye ubalozi wa China nchini Iraq ulithibitisha kuwa, mateka hao wa China walitoka mkoa wa Fujian,China na walikwenda nchini Iraq kufanya kazi ya vibarua kwenye makampuni ya ujenzi. Mwaka jana waliwahi kufanya kazi katika mradi wa ukarabati wa kiwanda cha nguo kilichoko mjini Najaf. Wiki iliyopita, raia hao wa China wasiopata ajira walipanda teksi kuondoka nchini Iraq, walitaka kurudi nyumbani kupitia Jordan, lakini walitekwa nyara wakiwa njiani kuelekea Amman, mji mkuu wa Jordan. Ubalozi wa China umeeleza kuwa utafanya juhudi kwa kadiri iwezekanavyo kuwaokoa mateka hao wachina. Ubalozi huo umewatuma watu kwenda kukutana na baraza la wazee waislam ambalo mwezi Aprili mwaka jana liliwahi kusaidia kuwaokoa raia wachina waliotekwa nyara nchini humo.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw. Kong Quan jana alieleza kuwa China inafuatilia sana tukio hilo na kutumai kuwa mateka hao wataachiliwa huru haraka iwezekanavyo. Wizara ya mambo ya nje ya China inafanya juhudi kubwa na kuchukua hatua mbalimbali za kuwaokoa mateka hao wachina. Bw Kong Quan alisema kuwa watu wa China wana upendo mkubwa kwa watu wa Iraq, kuwahurumia na kuwaunga mkono siku zote. Serikali ya China inaposhughulikia suala la Iraq pia inazingatia zaidi maslahi ya watu wa Iraq.

    Hili ni tukio la pili la kutekwa nyara kwa raia wa China lililotokea nchini Iraq. Mwezi Aprili mwaka jana, raia saba wachina kutoka mkoa wa Fujian walikwenda nchini Iraq kufanya kazi ya ujenzi. Walitekwa nyara na watu wenye silaha katika njia ya kuelekea Baghdad kutoka mji wa Mosul. Wakati huo kikundi cha kufufua ubalozi wa China nchini Iraq kilipopata habari hiyo, kilishughulikia kuwaokoa raia wa China mara moja. Kutokana na kusaidiwa na baraza la wazee waislam, raia hao wa China waliachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa saa 36. Wakati huo msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bw Kong Quan alisema kuwa katika mchakato wa kuwaokoa raia wa China, China haikufanya mazungumzo yoyote, na wala haikulipa fidia yoyote. Raia wa China waliachiliwa huru kutokana na juhudi zilizofanywa na pande mbalimbali. Uhusiano wa kirafiki wa muda mrefu kati ya watu wa China na Iraq ulifanya kazi muhimu. Aidha, msimamo wa China kuhusu suala la Iraq ulikubaliwa na watu wa hali mbalimbali nchini Iraq, ambapo marafiki wengi wa Iraq walifanya juhudi kubwa kabisa katika kuwaokoa raia 7 wa China.

    China siku zote inatetea kurejesha mamlaka kamili ya Iraq haraka iwezekanavyo ili kuwezesha wairaq waitawale Iraq wao wenyewe, na kuwawezenye wairaq waliokumbwa na vurugu za vita na balaa kubwa waishi maisha ya amani na utulivu. Kwa hiyo, serikali ya China na watu wake wana matumaini ya dhati kuwa kutokana na uhusiano wa kirafiki uliojengwa kati ya watu wa China na wa Iraq katika miaka mingi iliyopita, raia hao wanane wa China wataachiliwa huru mapema iwezekanavyo chini ya misaada ya marafiki na watu wa hali mbalimbali wa Iraq ili waweze kurudi nyumbani kukutana na jamaa zao.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-19