Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-19 20:47:32    
Ni watu gani wanaohitaji chanjo ya mafua

cri

    Kutokana na madhara makubwa ya mafua idara za afya za China zinazingatia sana kinga na tiba za mafua. Wizara ya afya ya China imeweka kinga na tiba za mafua kuwa ni moja ya maradhi muhimu ya kuambukiza katika kipindi cha mpango wa kumi wa maendeleo ya miaka mitano.

    Katika mkutano uliofanyika huko Geneva mwezi Machi mwaka 2004, Shirika la Afya Duniani lilitoa wito wa kutaka kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya matukio makubwa ya maradhi ya mafua. Je, ni watu gani wanaohitaji zaidi kupewa chanjo ya mafua?

    Jibu ni kuwa watu wa aina ya kwanza ni wale wenye umri wa zaidi ya miaka 60. Aina ya pili ni watu wenye matatizo ya moyo na mishipa ya damu, ugonjwa wa kisukari, kiungo cha mwili cha wengu kubadilika kuwa ya nyuzinyuzi, ugonjwa wa mshipa wa kupumua na wenye matatizo ya figo. Aina ya tatu ni watu wenye upungufu fulani katika kinga dhidi ya maradhi.

    Watu wengine wanaopendekezwa kutumia chanjo ya mafua ni wale ambao ni rahisi kuambukizwa mafua kutokana na kazi wanazofanya, kama vile madaktari na wauguzi; jamaa wa wagonjwa wa muda mrefu; watoto wa shule chekechea, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na wa vyuo vikuu; madereva na makondakta wa mabasi, wauzaji bidhaa wa madukani, wafanyakazi wa benki na polisi; watu wanaofanya kazi kwa pamoja na kukosa hewa safi, kama makarani wa maofisini. Lakini ukweli ni kwamba mtu yeyote mwenye hatari ya kuambukizwa mafua anaweza kupewa chanjo ya aina hiyo.

    Wakati mzuri zaidi wa kupewa chanjo ya mafua ni kabla ya makundi makubwa ya watu hayajaambukizwa mafua. Kwa watu wanaoishi katika sehemu ya kaskazini ya China, majira ya baridi na kuchipukia ni wakati wa maambukizi ya mafua, hivyo mwezi wa Septemba na Oktoba ni wakati mzuri zaidi wa kutoa chanjo ya mafua. Ni dhahiri kuwa watu wanaopata chanjo katika wakati ambapo watu wengi kuambukizwa mafua, pia wanaweza kujiepusha kuambukizwa mafua.

    Kuna baadhi ya watu ambao hawafai kupewa chanjo a mafua wakiwemo watu wanaojisikia vibaya baada ya kula mayai ya kuku na wanawake wajawazito waliopata ujauzito miezi michache iliyopita. Wagonjwa wenye homa, na wagonjwa wenye matatizo makubwa ya moyo na mapafu wasipewe chanjo ya mafua, mpaka itakapoonekana kuwa hali ya ugonjwa wao imetulia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-19