Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-20 20:42:19    
"Super-market ya upendo"unapendwa na watu

cri
Tarehe 14 mwezi Januari mkazi wa wilaya ya Kunwen, mji wa Weifang akichukua cheti alichopewa na serikali ya wilaya alifika "Super-market ya upendo" iliyoko katika wilaya hiyo kuchagua vitu alivyotaka kununua, baada ya kutembelea humo ndani alinunua mfuko mmoja wa unga wa ngano wa kilo 25. Alisema, "mimi na mke wa mtoto wangu tulipunguzwa katika viwanda vya serikali, hivyo tunaishi maisha yenye shida ya kiuchumi, baada ya ombi letu kuidhinishwa na serikali ya wilaya, tuliruhusiwa kununua vitu vya mahitaji katika duka hilo.

Tangu wilaya ya Kunwen kuanzisha harakati ya kuwasaidia wanamji wenye shida maishani mwao mwanzoni mwa mwaka uliopita, kundi la wakazi wenye shida ya kiuchumi limekuwa maalimu. Hapo zamani, vitu vilivyochangishwa na serikali kwa wakazi wenye shida ya kiuchumi mara nyingi havikuwa vitu vilivyohitajiwa sana na watu wa kundi hilo, na mara kwa mara shughuli hizo za kuchangisha mchango zinafanyika kabla ya siku kuu muhimu au wakati wanapokabiliwa na shida ya dharura, lakini watu hao wenye shida wanasumbuliwa na ukosefu wa vitu vyingi vya mahitaji ya lazima. Je, tunaweza kuanzisha utaratibu mwafaka na wa muda mrefu wa kuwasaidia wakazi wenye shida ya kiuchumi? Viongozi wa wilaya waliona bora kuanzisha "supa maketi ya upendo" kuacha wakazi wenye shida wachague vitu wanavyovihitaji badala ya mtindo wa zamani wa kupewa vitu vilivyochangishwa.

Wakazi wenye shida wanaosaidiwa hawakukaa bure, wanafanya kazi ya huduma kwa wakazi walioko katika makazi yao ili kuonesha shurani yao. Hivi sasa katika wilaya ya Kuiwen vimeanzishwa vikundi 17 vya doria vilivyoundwa na wazee hao wanaojitolea, wakati wazee hao zaidi ya 110 wanajitolea kufanya usafi katika maeneo ya makazi yao. Familia karibu 200 za wilaya ningine ya Weiwan wanaopewa msaada wa kiwango cha chini kila mwezi, mara kwa mara zinafanya kazi za huduma za kujitolea zikiwa ni kufanya doria, kug'oa majani na kuweka usafi katika makazi yao. Babu Li mwenye umri wa miaka 68 mwaka huu, ambaye anapewa msaada wa kiwango cha chini kila mwezi, kwa kawaida mzee akifikia umri huo anakaa nyumbani wala siyo vizuri kushiriki kazi za kujitolea, lakini hataki kukaa nyumba, kinyume chake kila siku anafanya doria katika eneo la makazi yao na kuchunga usalama wa nyumba za majirani.

Vitu vyote vilivyoko katika "supa maketi ya upendo" vilitokana na michango ya wakazi wa maeneo yao. "supa maketi ya upendo" ya kwanza ilianzishwa katika wilaya ya Kuiwen, katika muda wa mwezi mmoja baada ya kutolewa wito wa kuchangisha michango, "supa maketi ya upendo" hiyo ilipata kampyuta 11, televisheni 4, baiskeli 11, unga wa ngano tani 5.5, nguo zaidi ya elfu 3 pamoja na vitu vingine vinavyohitajiwa na wanafunzi vyenye thaamani ya yuan laki 1 na elfu 30 kwa jumla.

Hivi sasa wilaya hiyo imeanzisha "supa maketi ya upendo" 7 zikiwahudumia wakazi wenye shida zaidi ya 2,100. Kiongozi wa wilaya hiyo Bw. Wang Yuanbang alisema kuwa lengo la kuanzisha "supa maketi ya upendo" za aina hiyo ni kutoa misaada kwa wakazi wenye shida na kutoa nafasi kwa wasamaria kutoa upendo wao kwa watu wenye shida.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-20