Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-20 21:20:54    
<STRONG><FONT color=#31349c>Mfumo wa uchumi wa China</FONT></STRONG>

cri

    Kabla ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa mwaka 1949, China ilifanana na jitu dhaifu. Nchi hiyo iliyokuwa na watu zaidi ya milioni 500 na eneo la kilomita za mraba milioni 9.6 ilizalisha nyuzi tani laki 4.45, vitambaa mita bilioni 2.79, makaa ya mawe tani milioni 61.88, umeme kilowati bilioni 6, nafaka tani milioni 150 na pamba tani laki 8.49 kila mwaka. Huu ulikuwa msingi wa maendeleo ya uchumi wa Jamhuri wa Watu wa China.

    Baada ya ujenzi mkubwa wa kiuchumi kufuatana na mpango, hivi sasa China imekuwa nchi kubwa yenye nguvu ya kuendeleza uchumi wake, na maisha ya watu wa China pia yamefika kiwango kizuri cha kimsingi. Kuanzia mwaka 1953 hadi mwaka 2000, China imekamilisha mipango tisa ya "miaka mitano", na imepata mafanikio makubwa na kujenga msingi imara wa maendeleo ya uchumi wa taifa. Baada ya China kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango mwaka 1979, uchumi wa China umepata ongezeko kubwa ambalo halijawahi kuonekana hapo awali. Baada ya kuingia karne ya 21, uchumi wa China unaendelea kuongezeka kwa kasi. Mwaka 2002 thamani ya uzalishaji nchini China(GDP) ilifikia yuan za renminbi trilioni 10, ambayo imeongezeka kwa asilimia 8.

    Mageuzi ya mfumo wa uchumi wa China ni sehemu muhimu ya mageuzi. Miaka 30 baada ya Jamhuri ya Watu wa China kuasisiwa, serikali ya China iliendelea kutekeleza mfumo wa mipango. Shabaha za sekta mbalimbali za kiuchumi ziliwekwa na idara maalum yaani kamati ya mipango. Viwanda vilizalisha bidhaa kufuatana na mipango ya serikali, wakulima walipanda mazao kufuatana na mipango, na idara za biashara pia ziliingiza na kuuza bidhaa kufuatana na mipango. Na aina, kiasi na bei ya bidhaa pia viliamuliwa na kamati ya mipango. Mfumo huo uliuwezesha uchumi wa China uendelee kwa utulivu kufuatana na mipango na shabaha, lakini pia ulizuia ustawi wake na kasi ya maendeleo. Mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, viongozi wa China waliona tofauti kati ya uchumi wa China na duniani, walifanya sera muhimu ya kufanya mageuzi kuhusu mfumo uliotekelezwa kwa miongo kadhaa. Mwaka 1978, mageuzi yalianza kufanyika vijijini. Mfumo wa familia kusaini mkataba wa uzalishaji mazao ulianza kutekelezwa. Wakulima walikuwa na haki ya kutumia ardhi tena, waliweza kupanga kazi zao wenyewe na matumizi ya mazao yao, na kuamua aina na kiasi cha mazao waliyotaka kupanda. Na katika fani ya biashara ya mazao ya kilimo, wakulima pia walikuwa na haki ya kuchagua. Njia ya zamani ya mauzo ya pamoja na mauzo ya mipango imefutwa, bei nyingi za mazao ya kilimo haziamuliwi na serikali, na sera nyingi za vizuizi pia zimefutwa, wakulima wanaweza kufanya kazi mbalimbali, kuanzisha viwanda vijijini, na juhudi zao za uzalishaji zimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

    Mwaka 1984, mageuzi ya mfumo wa uchumi yalianza kutekelezwa mijini.

    Mwaka 1992, baada ya majaribio ya miaka zaidi ya kumi, serikali ya China ilikuwa na lengo wazi zaidi, yaani kujenga mfumo wa uchumi wa soko huria wa kijamaa.

    Mwaka 1997, serikali ya China ilizidi kusema kuwa uchumi usio wa kiserikali pia ni sehemu muhimu ya uchumi wa kijamaa wa China, na kutimiza rasilimali, teknolojia kuchangia ugawaji wa mapato ili mageuzi ya mfumo wa uchumi yaweze kupiga hatua kubwa zaidi.

    Hadi kufikia mwaka 2002, mageuzi ya pande mbalimbali yaliendelea kwa utaratibu na kupata mafanikio wazi. Kufuatana na mpango, ikifika mwaka 2010, China itaanzisha mfumo kamili wa uchumi wa soko huria la kijamaa; na ikifika mwaka 2020 mfumo uliokomaa utaanzishwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-20