Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-21 12:56:27    
Sherehe ya Kumwapisha Rais Bush Yafanyika Washington

cri
Tarehe 20 saa za mchana kwa saa za sehemu ya mashariki ya Marekani rais George Bush aliyeshinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba mwaka jana aliapishwa na kuwa rais kwa kipindi cha pili mfululizo nchini Marekani, na kuwa rais wa 55 wa Marekani. Hii ni sherehe ya kwanza ya kuapishwa rais tangu tukio la "Septemba 11" lilipotokea mwaka 2001, kwa hiyo usalama ulikuwa katika hali ya tahadhari sana.

Siku hiyo, hali ya hewa ilikuwa ya baridi, upepo ulivuma na theluji ilikuwa bado haijayeyuka. Asubuhi saa tatu watu elfu kumi hivi walianza kuingia kwenye uwanja wa kufanyia sherehe mbele ya jengo la bunge.

Hii ni sherehe ya kwanza ya kuapishwa rais iliyofanyika baada ya kutokea kwa tukio la "Septemba 11" mwaka 2001, askari polisi walikuwa wakivinjari na silaha kila baada ya mita mitatu katika barabara ya Pennsylvania toka jengo la bunge hadi ikulu, na mbwa wa polisi wakinusa huku na huko wakisaka mabomu, na kwenye mapaa ya maghorofa kando ya barabara iliyopitiwa msululu wa magari ya rais walipangwa wadunguaji.

Saa za mchana Bw. George Bush aliapishwa na jaji mkuu William Rehnguist, kisha alitoa hotuba ya dakita 19, akisema kuwa atajitahidi kulinda usalama wa taifa na kusukuma uenezi wa demokrasia duniani. Alisema,

"Kazi yangu tukufu ni kuilinda Marekani, kuwalinda wananchi wenzangu wasishambuliwe na magaidi?? Nyiye nchi za kirafiki za nchi yangu Marekani naona fahari kuwa rafiki yenu, nasadiki wosia wenu na nategemea misaada yenu??"

Rais Bush hakugusia masuala ya Afghanistan na Iraq, wala sera zake kuhusu mambo ya nje katika kipindi chake cha pili, lakini alisema, atasukuma mageuzi ya utaratibu wa huduma za jamii.

Kutokana na uchunguzi wa vyombo vya habari kuhusu maoni ya wananchi, wengi zaidi wana matumaini mema kuhusu utawala wa kipindi chake cha pili. Alasiri katika siku hiyo, pande mbili za barabara ya kufanyia maandamano walisimama watazamaji wengi. Kwenye kipito cha barabara hiyo mwandishi wa habari alimkuta Bi. Ann Culbelt, akisema,

"Natumai wananchi wa nchi yangu wote watakuwa kama mimi, kwamba wanaishi katika mazingira ya amani na usalama. Kwa mtazamo wa mbali mageuzi ya utaratibu wa huduma za jamii yananinufaisha. Nina umri wa miaka 39 sasa, natumai nitakapokuwa mzee nitapata huduma za kutosha."

Lakini uchunguzi wa vyombo vya habari pia waligundua kauli nyingine kuwa kiasi cha nusu walioulizwa wana wasiwasi kuhusu matatizo ya ndani ya nchi. Katika siku hiyo ya kumwapisha, jumuiya ya waliojitolea ya "Wampa Kisogo Bush" ilifanya harakati za kumlaani. Wanaharakati walisambaza karatasi wakiwaambia watu namna ya kutambua gari la Bush na barabara zitakazopitiwa na gari la Bushi na wakiona gali hilo likipita wamgeukie Bush kisogo kuonesha kumlaani. Mmoja kati ya waliojitolea Rebecca Cormeny alisema,

"Kwa kweli hakukuwa na haja ya kuanzisha vita dhidi ya Iraq. Huduma za jamii kwa wazee zimezorota, haki za mashoga zimenyimwa, na Bushi anawapunguzia tu watu matajiri kodi na aliingiza imani ya dini katika maamuzi yake ya siasa??"

Mkazi mmoja wa Washington, Bw. Vincent Virga alitundika bango kifuani likiandikwa "Vita sio njia pekee ya utatuzi wa matatizo", akiwaambia waandishi wa habari kuwa anataka kumfahamisha Bush kuwa sio wote wana fikra sawa naye. Alisema,

"Uhuru alioutaja ni uhuru wa watu wenye fikra sawa naye, ni uhuru wa Wakristo weupe. Marekani ni nchi yenye watu tofauti, lakini hakuwakilisha taifa zima."

Idhaa ya kiswahili 2005-01-21