Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-21 20:49:12    
Michoro ya Milima na Mito

cri

    Picha za kuchora za milima na maji ni moja ya michoro ya Kichina, ambazo ni picha zenye maudhui ya milima, mito na mandhari ya kimaumbile. Picha za aina hiyo zilikuwa zinaendelea polepole wakati wa enzi za Wei, Jin na Enzi sita ( yaani Enzi ya Wu 222-280, Enzi ya Jin ya Mashariki 317-420, Enzi ya Song 420-479, Enzi ya Qi 479-502, Enzi ya Liang 502-557 na Enzi ya Chen 557-589 ), kwa wakati huo milima na mito ilikuwa mingi zaidi, sehemu zenye mandhari nzuri na milima na mito ilikuwa ya kupendeza sana, hasa katika kipindi cha ustawi cha Enzi ya Tang, kwa kuwa amani ilidumu kwa miaka mingi, wachoraji walipata wakati wa kuchora picha hizo za kuonesha mazingira ya maumbile. Tangu hapo picha za milima na mito zilitenganishwa na picha za watu na kulitokea makundi mawili, la kaskazini na la kusini. Wachoraji wa sehemu ya kaskazini walikuwa ni wachoraji huria zaidi na wachoraji wa kusini walikuwa wanachora kwa utanashati zaidi.

    Enzi ya Song ilikuwa ni kipindi cha kukua kwa ustadi wa kuchora picha zenye mandhari ya milima na mito, kulikuwa na namna nyingi za uchoraji, wachoraji maarufu walijitokeza mmoja baada ya mwingine na wakawa walimu muhimu walioigwa na wachoraji wa vizazi vilivyofuata.

    Picha zenye mandhari ya milima na mito zimegawanyika katika sehemu nne, za wino wa maji, za kijani nyeusi, za wekundu hafifu na za dhahabu. Katika kipengele cha maonyesho ya sanaa huzingatia kuchagua nafasi mwafaka na kudhihirisha dhana za usanii. Picha nyekundu hafifu za milima na mito ni za rangi hafifu, nayo hupakwa juu ya msingi wa maumbo ya milima na mito yaliyochorwa kwa kutumia wino na mito. Picha nyeusi-kijani za milima na mito ni picha ambazo rangi zake kuu huwa ni samawati na kijani ya madini. Picha za milima na mito za rangi ya dhahabu ni picha zilizochorwa kwa unga wa dhahabu, kupakwa rangi ya dhahabu au kutiwa rangi ya dhahabu juu ya msingi wa milima na mito meusi-kijani ili michoro hiyo iwe na hulka ambayo huonekana adhimu katika kijani na dhahabu. Picha za wino na maji ni picha zinazochorwa kwa maji na wino tu, wachoraji wanapochora huzingatia njia za kutumia brashi na kutumia ipasavyo ufanisi wa njia za kutumia wino. Picha hizo zimechukua ustadi muhimu katika historia ya picha za kijadi za kichina.

    Hivi sasa kwenye sekta ya uchoraji wa picha za kichina, wachoraji wengi wamewahi kuchora picha za kichina, na wengi miongoni mwao wamepata mafanikio makubwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-21