Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-22 20:13:27    
Ni chaguo la mtu kuamua utaratibu wa maisha yake

cri

    Miaka minne iliyopita nchini China kulikuwa na watu saba waliofanya mazoezi ya Falungong walijichoma moto katika uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing. Tukio hilo lilisababisha kifo cha binti mmoja na mama yake, na pia kubadilisha maisha ya washiriki wengine pamoja na maisha ya familia zao. Hivi sasa miaka minne imeshapita, washiriki wale wamejitoa katika tukio lile? Hali ya hivi sasa ya watu hao pamoja na familia zao ikoje? Katika kipindi hiki cha leo, tunawaeleza jinsi maisha yao ya sasa yalivyo.

    Katika sehemu ya kiunga cha mji wa Kaifeng, Henan katikati ya China kuna nyumba moja ya huduma ambayo imejengwa vizuri ikiwa na tuta moja la mboga. Sauti hiyo ya muziki ndiyo ilitoka katika nyumba hiyo. Mwanamke Hao Huijun na binti yake Chen Guo, ambao walishiriki tukio la kujichoma moto kwenye uwanja wa Tian'anmen, hivi sasa wanaishi katika nyumba hiyo.

    Msichana Chen Guo ni mmoja kati ya watu wanaosikitisha zaidi miongoni mwa watu walioshiriki katika tukio lile. Yeye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo cha muziki cha China, anapenda kupiga gambusi, ambayo ni ala ya muziki ya jadi ya China. Baada ya kujichoma moto, mikono yake ilipoteza uwezo wake, na kumfanya asiweze kupiga ala ya muziki anayoipenda. Hivi sasa, Chen Guo kila siku baada ya matibabu, anapenda kusikiliza muziki. Kutokana na msaada wa wauguzi wa huko anafanya mazoezi ya kuandika maneno, kutumia kompyuta, hivyo anaishi maisha ya furaha. Hivi sasa matarajio yake makubwa ni kuwekewa mikono ya bandia na kusawazisha sura yake ili aweze tena kufanya maonesho mbele ya watu.

          

kabla na baada ya Chen Guo kujichoma moto kwenye Uwanja wa Tian'anmen

    Msichana Chen Guo na mama yake waliungua sana baada ya kujichoma moto, na wamekuwa na uchungu mwingi iwe kwa miili au kwa hisia zao. Kutokana na kusaidiwa na serikali na sekta mbalimbali za China, wameona hali halisi ya dhehebu ovu la Faungong, sasa si waumini tena Falungong na kujuta sana juu ya imani yao ya zamani.

    Kutokana na kuwa wamekuwa walemavu, Hao Huijun na Chen Guo wanategemea wauguzi wa huko katika maisha yao, na wanaridhika kuhusu maisha yao ya hivi sasa. Hao Huijun anataka kufanya kazi yoyote kwa ajili ya jamii kadiri anavyoweza. Alisema,

    "Mara tu baada ya kujitoa kutoka kwenye kundi la Falungong, niliona nitakuwa mzigo kwa jamii, nikataka kuandika makala, nikaandika baadhi ya hadithi ndogo za jadi pamoja na hadithi za watoto, niliomba wauguzi waniandikie hadithi hizo."

    Nia na tarajio la Hao Huijun na binti yake inaonekana kuwa ni kutaka maisha mazuri. Katika familia nyingine ya watu walioshiriki pamoja kujichoma moto, matarajio hayo yameanza kutimizwa hatua kwa hatua.

    Wang Jindong, ambaye alijichoma moto na kuwashirikisha watu wengine kujichoma moto, hivi sasa anatumikia kifungo gerezani, nyumba yake iko katika sehemu moja mjini Kaifeng, yeye na mkewe pamoja na binti yake walikuwa wakiishi huko. Ingawa nyumba yao haikuwa nzuri, lakini walikuwa na matarajio kuhusu maisha yao ya siku za baadaye. Binti yake Wang Juan aliolewa mwaka 2003 na mwaka jana alipata mtoto wa kiume. Hivi sasa furaha kubwa ya Wang Juan na mama yake He Haihua ni kumlea mtoto ili akue vizuri na awe na afya njema.

    He Haihua na Wang Juan pia walifanya mazoezi ya Falungong, alipozungumzia mabadiliko ya maisha yake tangu afanye mazoezi ya Falungong hadi kuyaacha, Wang Juan alisema,

    "Zamani nilifanya mazoezi ya Falungong, na mambo tuliyoongea watu wa familia yetu pia yalihusu Falungong, tulihisi kuwa katika shinikizo tusiloliona, tulikuwa tunaona si vizuri kufanya shughuli tunazotakiwa kuzifanya. Hivi sasa tumejitoa katika kundi la Falungong, tunaishi kwa furaha na tunaweza kujiburudisha kadiri tunavyotaka. Hivi sasa tunataka kuishi maisha ya kawaida."

    Baada ya He Haihua na Wang Juan kuondokana na udhibiti wa kiroho wa Falungong, wanawasaidia watu wengine wanaofanya mazoezi ya Falungong kujitoa katika dhehebu hilo ovu kwa kutumia mambo ya familia yao. Wang Juan alisema,

    "Baada ya sisi kuondokana na madhara ya Falungong, tulitaka kwa hiari yetu kuwasaidia watu wengine wanaofanya mazoezi ya Falungong kujitoa katika dhehebu hilo ovu na kuishi maisha ya kawaida. Njia muhimu tuliyotumia ni kuwafahamisha kwa mambo ya familia yetu." He Haihua alisema,

    "Kwa sababu watu wengi wanasema Wang Jindong ni mwongo, watu wote wa familia yetu ni waongo. Hivyo tunakwenda kuwaeleza mambo halisi."

    Wang Juan sasa anafanya kazi katika shule moja ya chekechea mjini Kaifeng, alisema kuwa mazingira ya kazi yake ni mazuri na anafanya kazi kwa furaha. Hivi sasa He Haihua hana kazi, yeye yuko nyumbani kumtunza mtoto wa binti yake.

    Wanapomzungumzia Wang Jindong ambaye hivi sasa anatumikia kifungo gerezani, mama na binti yake hawana wasiwasi, wanatarajia ataweza kubadilisha mawazo yake na kurejea nyumbani mapema kuishi pamoja nao. He Haihua anatarajia maisha mazuri baada ya mumewe Wang Jindong kutoka gerezani.

    Upendo na utiaji moyo wa He Haihua na Wang Juan ni nguzo ya kiroho kwa mfungwa Wang Jindong. Kutokana na kusaidiwa na serikali pamoja na watu wa familia yake, Wang Jindong amejitoa katika udhibiti wa Falungong, hivi sasa jeraha alilopata kutokana na kujichoma moto limepoka kwa jumla.

     Miongoni mwa watu waliojichoma moto katika uwanja wa Tianmen ni pamoja na mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Liu Baorong. Baada ya kurejea nyumbani kutoka Beijing ameona hali halisi ya dhehebu ovu la Falungong na kujitoa kabisa katika dhehebu hilo, hivi sasa anaishi maisha ya furaha.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-22