Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-24 16:08:13    
Mahmoud Abbas aonesha uwezo wake wa kutatua mgogoro

cri

Hali wasiwasi kati ya Palestina na Israel iliyosababishwa na mashambulizi dhidi ya kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel imetulia dhahiri hivi karibuni. Maoni ya watu yanaonesha kuwa, kupunguzwa kwa hatua ya mwanzo kwa mgogoro huo kunatokana na mkakati wa kisiasa na hatua imara zenye unyumbufu zilizochukuliwa na mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas.

Katika siku kadhaa zilizopita, utulivu ulionekana katika ukanda wa Gaza, hali ambayo ilikuwa ni nadra kutokea, ambapo vikundi mbalimbali vya kijeshi vya Palestina viliacha kimsingi mashambulizi dhidi ya makazi ya wayahudi na miji ya kusini mwa Israel, na mazungumzo kati ya Abbas na vikundi mbalimbali yaliendelea vizuri, na huenda makubaliano ya kusimamisha vita dhidi ya Israel yatasainiwa mapema. Israel pia ilieleza kuwa, kama watu wenye silaha wa Palestina wataacha mashambulizi, jeshi la Israel halitaanzisha kwanza kampeni ya kijeshi kwenye ukanda wa Gaza, na kama hali ya mambo itaendelea kuwa tulivu, Israel itazingatia maandalizi yake kwa ajili ya mkutano wa wakuu wa Palestina na Israel, tena itapenda kuikabidhi Palestina baadhi ya madaraka ya kudhibiti usalama wa miji ya Palestina.

Mgogoro huo ulisababishwa na mashambulizi ya watu wenye silaha wa Palestina dhidi ya kituo cha ukaguzi cha jeshi la Israel. Changamoto iliyotolewa hadharani na kundi lenye msimamo mkali la Palestina na hatua kali moja baada ya nyingine za Israel zilimfanya Abbas akabiliwe na taabu kubwa. Kwa upande mmoja anapaswa kuchukua hatua imara kwenye msingi wa kutoharibu hali ya utulivu wa kisiasa wa Palestina ili kutumia nafasi ya kihistoria iliyotokea katika mchakato wa amani ya mashariki ya kati na kuboresha hali ya taabu ya kisiasa na kidiplomasia ya Palestina kwa hivi sasa; na kwa upande mwingine anapaswa kueleza msimamo wake wa lazima wakati anapokabiliwa na shinikizo za Israel na Marekani, ili kutokwenda kinyume na msimamo wa kikanuni wa Palestina na kukwepa kuathiri maslahi ya kimsingi ya wapalestina.

Bwana Abbas alichukua hatua imara na hatua laini. Kwa upande mmoja alishikilia kufanya mazungumzo na mashauri na kundi lenye msimamo mkali la Palelstina kuacha mashambulizi dhidi ya Israel bila kujali shinikizo la Israel; kwa upande mwingine alisawazisha msimamo wa vikosi mbalimbali vya usalama vya Palestina vyenye migongano mbalimbali, kutuma askari elfu kadhaa wa vikosi vya usalama vya Palelstina kwenda sehemu za mpaka kati ya ukanda wa Gaza na Israel ili kuwazuia wanamgambo wa Palestina kushambulia shabaha za Israel.

Bwana Abbas alichukua hatua hizo kutokana na uchambuzi wake sahihi kuhusu hali ya mambo. Baada ya kukumbwa na mashambulizi ya Israel kwa muda mrefu, makundi yenye msimamo mkali ya Palestina yamedhoofika vibaya. Lengo lao la kisiasa na mbinu zao za mapambano si kama tu hazilingani na hali ilivyo ya sasa, bali pia zinakwenda kinyume na nia ya raia wa Palestina na mawimbi duniani, dalili mbalimbali zimeonesha kuwa watu kadhaa wenye siasa kali wameanza kuacha msimamo wa mapambano na kupenda kutumia njia ya kisiasa; aidha raia wa Palestina wamechoshwa na migogoro kati ya Palestina na Israel, tena Jumuiya ya kimataifa inashikilia kufanya usuluhisho kati ya Palestina na Israel.

Hali ya mambo imeonesha kuwa, hatua zilizochukuliwa na Bwana Abbas ni zenye ufanisi. Baada ya mazungumzo yenye taabu, vikundi mbalimbali vya Palestina vimelainisha dhahiri msimamo wao na kukubali kusimamisha vita, hali ya Gaza imedhibitiwa vizuri. Uwezo wa Abbas umesifiwa na jumuiya ya kimataifa na pia umeishangaza Israel.

Lakini Abbas amepiga hatua ya mwanzo, na bado atakabiliwa na taabu nyingi kutoka nchini na nje.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-24