Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-24 20:10:41    
Mpango wa miaka 10 ya kupunguza maafa ya kimaumbile waandaliwa katika mkutano wa Kobe, Japan

cri

    Mkutano wa kupunguza maafa ya kimambile uliofanyika huko Kobe, Japan ulimalizika tarehe 22. Mkutano huo umeandaa mpango wa jinsi ya kupunguza maafa ya kimaumbile duniani katika muda wa miaka 10 ijayo.

    Nyaraka mbili muhimu zilizopitishwa katika mkutano huo ni "Taarifa" na "Mpango wa Utekelezaji wa Taarifa". "Mpango wa Utakelezaji wa Taarifa' umeweka malengo matano yatakayofikiwa tokea mwaka 2005 hadi 2015. Nayo ni: Kazi ya kupunguza maafa iwe moja ya kazi kuu za serikali katika kila nchi; kuongeza uwezo wa kutabiri maafa; Kuimarisha usalama na mapambano dhidi ya maafa katika kila ngazi ya jamii; Kupunguza hatari za zinazoweza kusababisha maafa; Na kuimarisha matayarisho ya mapambano dhidi ya maafa.

    "Naona mpango wa utekelezaji wa taarifa ni mzuri" naibu katibu mkuu anayeshughulikia mambo ya uokoaji wa maafa katika Umoja wa Mataifa alisema. Anaona kuwa mpango wa utekelezaji utasaidia kupunguza maafa ya kimaumbile katika muda wa miaka 10 ijayo, na kuifanya dunia iwe salama zaidi baada ya miaka 10 na inaweza kupunguza vifo vya watu kwa nusu.

     Bw. Huyo alisema kuwa tsunami iliyotokea katika bahari ya Hindi ni kama "onyo" inayokumbusha jumuiya ya kimataifa umuhimu wa suala la kupunguza maafa. Takwimu zilizotajwa katika nyaraka za mkutano huo zinasema kuwa katika muda wa miaka 20 iliyopita, kwa wastani kila mwaka watu zaidi ya milioni 200 duniani waliathirika kutokana na maafa. Kwa hiyo maafa ya kimaumbile yamekuwa tishio kubwa la dunia nzima siku hadi siku, na ni kikwazo kikubwa katika njia ya maendeleo endelevu na juhudi za kuondoa umaskini.

    Mpango wa utekelezaji wa taarifa unaona kuwa lazima utambuliwe vya kutosha uhusiano kati ya juhudi za kupunguza maafa na maendeleo endelevu na juhudi za kuondoa umaskini, na sekta zote lazima zihamasishwe na kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza hatari ya kusababisha maafa na kupunguza madhara.

    Kwenye mkutano wajumbe pia walijadiliana tsunami ya bahari ya Hindi. Wajumbe wa nchi mbalimbali waliahidi kuwa wataendelea kutoa misaada kwa nchi zilizoathirika na tsunami ya bahari ya Hindi na kupitia wakati mgumu kwa pamoja. Wajumbe pia walikubaliana kuanzisha mfumo wa utabiri wa maafa ya kimaumbile chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa ili kuongeza uwezo wa kukinga na maafa katika dunia nzima.

    Bw. Naibu katibu mkuu huyo alisema kuwa anatumai kuwa sehemu ya bahari ya Hindi ingekuwa "maabara" kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa dunia nzima wa utabiri wa maafa ya kimaumbile.

    Huo ni mkutano wa pili wa dunia wa kupunguza maafa ya kimaumbile. Mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 1994 mjini Yokohama, Japan. Kwenye mkutano huo wa siku tano wa mjini Kobe ulihudhuriwa na wajumbe 4000 kutoka zaidi ya nchi 150. Baada ya kuzingatia taarifa ya pamoja ya Yokohama na wanaona kuwa mpango wa utekelezaji wa taarifa wa mkutano huo wa Kobe ni wa makini zaidi kuliko ule wa Yokohama.

    Baada ya mkutano kumalizika, kwenye mkutano na waandishi wa habari mkurugenzi wa mkakati wa kupunguza maafa ya kimaumbile katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa Mpango wa Utekelezaji wa taarifa wa mkutano wa Kobe umezingatia "maendeleo ya haraka ya miji, mabadiliko mabaya ya mazingira, na mabadiliko ya hali ya hewa kuwa joto duniani."

    Waziri wa mambo ya raia wa China alitoa mapendekezo ya kuanzisha mfumo wa utabiri wa maafa kwenye sehemu ambazo ni rahisi maafa ya kimaumbile kutokea. Mapendekezo yake yaliungwa mkono na wajumbe wote.

Idhaa ya Kiswahili 2005-01-24