Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-01-25 14:13:18    
barua0125

cri
Msikilizaji wetu Mbaraka Mohammed Abucheri wa Shekhe Estate Salaam Club sanduku la posta 792, Kakamega Kenya ametuletea barua akianza kwa salamu na akitarajia kuwa hapa Beijing sisi ni wazima. Kwanza anasema angependa kutufahamisha kuwa amepokea barua yetu iliyo na ratiba ya vipindi vya Radio China kimataifa tuliyomtumia hivi karibuni, hivyo anatushuruku sana kwa kumuorodhesha miongoni mwa wasikilizaji wa Radio China kimataifa.

Anaona hii ni heshima kuu tuliyomtunuku, sio tu kwake binafsi bali hata kwa klabu ambayo imebuniwa kwa lengo la kuwasiliana na kusalimiana na mashabiki wapenda salamu kote duniani. Anasema anaichukulia nafasi hii kama ni dhahabu kwake. Hivyo ataitumia bila kuchoka, kuhofu na kuwa na dosari yoyote.

Anasema anatarajia kujenga uhusiano thabiti na wa kudumu na marafiki wasikilizaji kutoka China na mataifa mengine duniani. Anasema anaishukuru Radio China kimataifa.

Pia anasema lengo lake la pili la kutuandikia barua hii ni kuhusu mapendekezo yake aliyoyaandika kwenye barua yake ya tarehe 8 Oktoba mwaka 2004 kuhusu kubuniwa kwa vipindi vingine kadhaa kama vile maoni ya wasikilizaji, ukumbi wa mashairi, mashujaa wasikilizaji wa Radio China kimataifa, vijana na maendeleo, Dunia leo, Tabasamu, Tafakari, kipindi cha kupokea visa vya kufurahisha na kuchekesha na vyenye mafunzo toka kwa wasikilizaji. Yeye hapo ameambatanisha kwenye barua hii visa vyake mbalimbali vyenye mafunzo vya Tabasamu na Tafakari ili kuwa mfano bora kwa wale wasikilizaji wenye heri njema kutuma maoni yao na makala yao.

Anasema anaomba kwa hisani na heshima yetu kuu kutoa nafasi na fursa kwa wasikilizaji kama yeye ambao wana vipaji mbalimbali kuchangia maendeleo na ufanisi wa Radio China kimataifa kwa kutoa elimu na mapendekezo ili kuimarisha Radio China kimataifa kufikia upeo wa juu katika vipindi na utoaji huduma bora zenye uhakika na kuvuita na zenye kuleta taswira na kupendeza kote duniani.

Anasema anatarajia mapendekezo yake tutayachukulia kwa umuhimu mkubwa na kuyatumia kikamilifu. Pia anatukumbusha tumtumie vitabu na magazeti, beji ya Radio China kimataifa na kalenda ya mwaka 2005 ya Radio China kimataifa. Anatutakia baraka na ufanisi kwenye kazi zetu za kutoa huduma.

Tunamshukuru sana kwa maoni na mapendekezo yake msikilizaji wetu Mbarak Abucheri. Tunafurahi kuona kuwa kweli anafuatilia sana vipindi vyetu na kukutoa maoni na mapendekezo hayo yenye umuhimu mkubwa, hapa tunataka wasikilizaji wetu wote waitikie mwito wake ili kuchangia katika maendeleo na ufanisi wa Radio China kimataifa. Tuna imani kuwa ingawa juhudi zinazofanyika siku hadi siku haziwezi kuleta ufanisi haraka, lakini kama tunashikilia kufanya juhudi siku hadi siku, na tunatumia kuwa juhudi hizo zitaongeza mafanikio. NA mapendekezo uliyotutumia kama kawaida tutayafanyia kazi.

Idhaa ya kiswahili 2005-01-25